Huyo jamaa ameongea kwa kutumia commonsense ni kweli kwa macho ni ngumu kuona faida hiyo ya 50k/day ila kunakitu hajui kuwa kila biashara kunambinu,
Kuna waendesha bajaji ni flexible yani unakuta mtu asubuhi saa 12 yupo lami anachukua vichwa vya kuwahisha mjini watu makazini mfano nilipo mm ni 2000/head na bajaji inachukua vichwa 3 so =6000 mpaka mjini asubuhi Hii wanasolve changamoto ya wafanyakazi kuwahi offisini kukwepa foleni na Usumbufu wa daladala.
Assume kwa asubuhi tu amepiga ruote tatu =18,000/=
2 to 10 Anaingia kwenye ruote za kawaida za 700/kichwa
Jione anahama route na kuwatoa watu mjini kwenda makwao ambayo ni 1000/kichwa
Hikifika saa 4 Usiku kwa huku kwetu watu wanahama route kwenda ubungo, Ili kuwatoa ubungo kwenda nje ya jiji kwa Wale wanatoka mkoa pale ubongo akuna means ya kupata daladala mpaka kutembea to mawasiliano ni usumbufu bora kuchukua bajaji 1000/kichwa
Bado kuna madereva wanawateja wao constant wale wakupiga simu, weekend kuna jamu kubwa ya kutoa na kupeleka watu sehemu za kupendeza na kwengineko.