Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Inategemea upo wapi mjini au nje ya mji, mashambani au mijini, ziwani au porini.
 
Dili ya direct tairi chakavu kwa mtaji wa nusu ya hiyo hela.. Masoko yapo machaka ya kupata mzigo yapo
Dili nyingine ya moja kwa moja oil chafu.. Faida yake haina hasara hata siku moja
Oil chafu unauzia wapi na inatumika kufanyia nini
 
Kuna viwanda sasa hivi vinakamua mafuta toka kwenye tairi chakavu huo mchakato unaitwa pyrolysis.

Na mafuta yanayokamuliwa yanaitwa IDO(Industrial Diesel Oli) haya yana soko kubwa sana kwenye viwanda vyote vinavyotumia mfumo wa BOILERS kama chanzo cha NISHATI

Tairi moja chakavu unainunua kati ya 1000 na 2000 nawe unaenda kuuza tani moja (approximately tairi 16 kwa laki moja.. Ukitoa mtaji na usafiri hukosi 50,000 faida kwa kila tani

Tairi kwa wingi zinapatikana kwenye mayard makubwa yenye kampuni za usafri
Viwanda vyenye kuhitaji hiyo malighafi hivi hapa
Mvuti Chanika
Kibada Kigamboni
Madafu Kibaha
Bagamoyo
Tegeta Dar

Naamini nimetoa maelezo ya kutosha sana
TATIANA
aliyetegwa
 
Duka kubwa la dawa na vipodozi, tafuta sehemu ambayo mji unakuwa na kuna changamoto ya huduma ya afya au huduma za dawa, yenye watu wengi...soko ni watu woote, changamoto ni wakaguzi wasumbufu kipindi hiki na kama sio mtu wa kada ya afya itabidi ujifunze sana kuijua inavyoenda, faida ni nzuri kwa asilimia kubwa ya bidhaa...kuanzia 50% hadi 200%.
 
Duka kubwa la dawa na vipodozi,tafuta sehemu ambayo mji unakua na kuna changamoto ya huduma ya afya au huduma za dawa,yenye watu wengi...soko ni watu woote,changamoto ni wakaguzi wasumbufu kipindi hiki na kama sio mtu wa kada ya afya itabidi ujifunze sana kuijua inavyoenda,faida ni nzuri kwa asilimia kubwa ya bidhaa...kuanzia 50% hadi 200%.
Ni sawa pia ila changamoto itakuwa kwenye vibali na nyaraka na wafanyakazi
 
Back
Top Bottom