Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Fungua min garage hapo dar.

Utafanya repairing haya.

1. Repairing ya matairi.

2.utajaza upepo kwa air compressor

3.utamwaga Oil na kuweka oil mpya

4. Utauzwa Oil chafu

5.Matairi chakavu

6. Utauzwa spair parts .

Hii biashara inapesa hasa kwa dar ndio plan yangu kuifungua mwakani.

Zaidi skillls ndogo za magari na pikipiki utazifanya kama kufungua hapa kukaza pale still huwezi kosa Hela kwa dar hapo
 
Mimi naona kwa hiyo hela ukiwekeza, kwenye kilimo cha umwagiliaji kinakutoa mapema sana. Aidha nitoe mfano mfupi unanunua eneo hekta 5. Kwa milioni mbili na nusu vijijini, kuchimba kisima, cha maji milioni tatu. Unaajili mtu mmoja au wawili wa kukusaidia, aidha hapa mengine ni matumizi madogo madogo. Unakuwa ukilima nyanya, tikiti, vitunguu na mahindi n.k.
 
Habari zenu wakuu.

Bila kupoteza muda ipo hivi nimekuja kwenu nahitaji ushauri wa kibiashara.

Je, 5M naweza kufungua biashara gani ikanitoa binafsi sijawahi kufanya biashara yoyote.

Ushauri wenu Wadau🙏
 
Tengeneza mkeka Weka odds za maana, Hiyo million 5 inageuka kua milion 10 baada ya dakika 90. All the best
 
Habari zenu wakuu.

Bila kupoteza muda ipo hivi nimekuja kwenu nahitaji ushauri wa kibiashara...
Kwanza unapaswa kujua wewe binafsi huwa unapendelea biashara au mradi gani?
Kisha Soma mazingira uliyopo yafaa kwa hiyo biashara au mradi unaoupendelea?

1usimamizi unauweka vipi katika mradi wako? Urasimamia mwenyewe ikiwa unao muda wa kufanya hivyo? Au 7taweka msimamizi?

Uhitaji wa nradi au bidhaa biashara au huduma unayotaka kufanya kwa maana ya wateja wako.

Utoshelevu wa mtaji.
N.k
 
Habari zenu wakuu.

Bila kupoteza muda ipo hivi nimekuja kwenu nahitaji ushauri wa kibiashara.

Je, 5M naweza kufungua biashara gani ikanitoa binafsi sijawahi kufanya biashara yoyote.

Ushauri wenu Wadau🙏
Jaribu forex broo
 
Back
Top Bottom