Mtandao wa barabara za lami alizojenga Mstaafu Kikwete katika kipindi chake cha uongozi

Mtandao wa barabara za lami alizojenga Mstaafu Kikwete katika kipindi chake cha uongozi

Usijisahaulishe kuwa waziri wa Ujenzi alikuwa Magufuli ambaye alikuwa anaenda kudai bajeti yake kibabe mkimkatalia anasogeza miwani yake kwa kidole kimoja akaunti inasoma.

Sasa twambie hiyo kasi imeishia wapi kwa waziri Mbarawa
Kwa hiyo kama waziri ndo mjenzi,awamu ya 5 waziri wa ujenzi alikuwa magufuli?kwo hakufanya kitu ktk awamu yake sasa
 
Kumbuka JPM ni miaka mitano 5! Marudio ya barabara ya Isaka - Rusumo ni enzi ya Magufuli! Ukiweka miradi yote JPM amewapiga bao la uhakika hao matutusa!
Alijengea mdomoni sana kuliko uhalisia.Jk na Samia hawaongei sana,ni vitendo tu
 
Mmoja hapo kakaa miaka mitano mwingine 10 ila unaona wote wana grounds sawa za kupambanishwa.
 
Hii wizara ilikuwa haiendeshwi na raisi la sivyo Kawambwa angeweza kuonyesha ufanisi kama Magufuli.
Kama siyo ubunifu wa JPM kuifungua Dar kwa fly overs na barabara mbili sasa hivi Posta - Tegeta, posta-Kimara tungekuwa tunaitembea kwa siku nzima.
Sukuma gang mna tatizo kwenye ubongo sio Bure.Wakati wa JK mnakataa kazi za JK eti Kwa kuwa magu alikuwa waziri wa ujenzi.Kwa hiyo magu ktk awamu yake yeye pia alikuwa waziri wa ujenzi?
 
Manyoni- Itigi-Tabora, 2015 December,nimepita ikiwa ni vumbi barabara yote,..kama hili umedanganya,ninaamini zipo barabara nyingi umetaja kwa kudanganya maana lengo lako ni kumpaisha mtu flani dhidi ya mwingine..

Kwa kuwa unajua upo uwezekano wa sisi sote tulioko humu, hatukupita kwenye barabara zote ulizotaja hadi kufikia November 2015, unadhani utatudanganya kirahisi tu
Wewe ndo muongo.Barabara ilianza kujengwa na JK,Magu akaja kuimalizia
 
Huyo mwizi mkubwa mali za umma wala sio wa kusifia.

1. Akunywa gesi yote
2. Mambo ya Epa
3. Tegeta ..escrow
4. Kashfa aliyomtoa Lowasa kafara, mzee wa watu mgonjwa hadi leo.

5. Kujilimbikizia ardhi nchi nzima kwa kumtumia Riz1.

Jamaa ni bonge la jambazi, hata hii DPW yeye ndiye Injinia wa mchoro mzima, jamaa hataki kustaafu ksbisa..

Huyu kikizaliwa kizazi chenye akili makaburi ya ukoo wake na yeye yatapigwa kiberiti.
Fuatilia vzr ww.IPTL ulikuwa ya mkapa.Sema JK alikuwa mwingi wa busara.Aliyabeba kama yake.Huyo magu wenu kama alikuwa msafi Kwa nini alimfukuza kazi CAG ASAD?Kwa nini hakuuweka wazi mkatava wa ununuzi wa ndege, ujenzi wa SGR?Acheni chuki za kijinga.Kwa Sasa JK is the best.Labda aje kufunikwa na Samia
 
atakufa tu, atalipa damu alizomwaga na yote aliyodhulumu ataacha hapahapa
 
Mhavile Flyover ipo sehemu gani Mkuu?
Unamchukia JPM lakini hizo Barabara unazozitaja yeye ndiyo alisimamia kama Waziri wa Ujenzi,unapoongelea masuala ya miundombinu Tanzania, Magufuli ndiyo icon.
Samia kumsifia bado sana, ndiyo kwanza kashaharibu mambo na DP World yake!

Hutaki hamia Burundi!
Kwa hyo magu ktkt awamu yake yeye pia alikuwa waziri wa ujenzi?
 
We mpuuzi unaleta ushindani usiokua na maana kujifanya Magu hakufanya chochote.

Njombe-Makete ile lami umeijenga wewe????

Barabara alizojenga unaemshabikia hazijamaliza hata miaka kumi zimefumuliwa zinajengwa upya.
Ref, Dodoma-Iringa
Kwo ulitaka barabara idumu milele wkt inatumika co?Mbona ya magu(usagara-kisesa) imeshaanza kuharibika?
 
Usijisahaulishe kuwa waziri wa Ujenzi alikuwa Magufuli ambaye alikuwa anaenda kudai bajeti yake kibabe mkimkatalia anasogeza miwani yake kwa kidole kimoja akaunti inasoma.

Sasa twambie hiyo kasi imeishia wapi kwa waziri Mbarawa
Upo sawa kabisa, mpaka boss wake aliwahi mwambia apunguze ukali naye akajibu mie nilikuja bungeni kama mbunge, uwaziri si kitu hata ukichukuliwa.
 
Kumbuka JPM ni miaka mitano 5! Marudio ya barabara ya Isaka - Rusumo ni enzi ya Magufuli! Ukiweka miradi yote JPM amewapiga bao la uhakika hao matutusa!
Kama mto wami daa ulikuwa mfupa wa nguruwe ule ila JPM kaumaliza
 
We mpuuzi unaleta ushindani usiokua na maana kujifanya Magu hakufanya chochote.

Njombe-Makete ile lami umeijenga wewe????

Barabara alizojenga unaemshabikia hazijamaliza hata miaka kumi zimefumuliwa zinajengwa upya.
Ref, Dodoma-Iringa
Ile barabara ya mbagala kuu, kama jina lake utazani imejengwa enzi za mkoloni
 
Fuatilia vzr ww.IPTL ulikuwa ya mkapa.Sema JK alikuwa mwingi wa busara.Aliyabeba kama yake.Huyo magu wenu kama alikuwa msafi Kwa nini alimfukuza kazi CAG ASAD?Kwa nini hakuuweka wazi mkatava wa ununuzi wa ndege, ujenzi wa SGR?Acheni chuki za kijinga.Kwa Sasa JK is the best.Labda aje kufunikwa na Samia
Hizi ndio akili za walimu. kazi ipo
 
Siwezi kuelezea mambo yote aliyoyafanya mzee wetu mstaafu mh. sana Jakaya Mrisho Kikwete, leo napenda kuorodhesha baadhi ya barabara za lami alizojenga ktk kipindi cha uongozi wake. Nafanya hivi pengine kuwakumbubusha au kuwajulisha kwa wale ambao hawafahamu maana kuna sijui vitoto au watu wazima kwa makusudi wanamkejeli Kikwete kana kwamba hakuna lolote ila Magufuli ndiyo kafanya mambo mengi.

Watu wamejaa uwongo na upotoshaji wa hovyo. Kwa taarifa yenu Magufuli hakuna miradi ya maana alikamilisha, isipokuwa michahe sana ambayo baadhi nitaitaja vilevile.

Mzee Kikwete alijenga mitandao ya barabara zifuatazo:

Mwanza-Geita-Bukoba

Nzega-Tabora

Manyoni-Itigi-Tabora

Dodoma-Iringa

Singida-Babati-Minjingu

Minjingu-Arusha

Arusha-Namanga

Babati-Kondoa-Dodoma

Songea-Namtumbo-Tunduru-Nanyumbu-Masasi

Tanga-Mkinga-Horohoro

Himo-Holili

Himo-Marangu-Rombo-Tarakea

Songea-Mbinga

Mbeya-Sumbawanga

Sumbawanga-Mpanda

Bagamoyo-Msata

Tinde-Isaka-Kahama-Kasamwa-Ngara

Mwanza-Musoma

Baadhi ya miradi aliyokamilisha JPM

Kijazi Interchange

Mhaville Flyover

Mbezi Louis Bus Terminal

Barabara ya Mwigumbi-Maswa-Bariadi

Stand kuu ya mabasi nanenane-Dodoma

Chato International Airport

Miradi mingine mingi aliiacha chini ya 50%, SGR Dar-Moro nafikiri kwenye 80%

Anatokea mtu anasema Kikwete hajafanya kitu ila Hayati Magufuli, kiukweli Magufuli alikamilisha mambo machache sana, na hii inatokana na ukweli kuwa hakuwa na mipango mizuri, alikuwa anaanzisha miradi kwa pupa na kwa sifa ndiyo hiyo inamtesa mama mpaka sasa.

Hata yeye nafikiri anashukuru Mungu amemficha asingeweza kuikamilisha, alishaharibu mahusiano ya kimataifa pesa angepata wapi? Wajinga humu watanitukana ila message sent and delivered na ndiyo ukweli ambao wenye akili wanaujua. Huyu Rais wetu wa sasa Dr. Samia Suluhu Hassan ana akili nyingi sana, ni mjanja sana ndiyo maana anafanya maajabu makubwa usiyoweza kuyaamini. Ndiyo Rais atakayekuja kuvunja rekodi zote zilizopita, tuombeni uzima tufike 2030 tutajionea.

Mpaka sasa hivi ameshakaribia kuikamilisha miradi yote mikubwa sana ya kimkakati ya matrilioni ya pesa aliyoanzisha Magufuli kwa pupa ambayo yeye mwenyewe asingeweza kuikamilisha.

Kila eneo huyu Rais ni wonders, mi siyo chawa wala siko kwenye mambo ya siasa hata sifahamiki kokote, ila nina viungo vya kuona na kusikia.

Nimepanga siku nirushe baadhi ya mambo ambayo ameshayafanya ndani ya miaka hii miwili na ushee aliyohudumu.

Kila mtu ataandika hadithi yake Mungu amlinde rais wetu atakuja kuandika hadithi ndefu isiyo kifani.
The most corrupt President of all times, hajatokea (pamoja na drug trafficking) JK.

Rais aliyekuwa na Vision - JPM

Dumb President- Sisemi anajulikana

Huna haja ya kuyaorodhesha yote hayo
 
Alijengea mdomoni sana kuliko uhalisia.Jk na Samia hawaongei sana,ni vitendo tu
JPM alikuwa na mambo makubwa ndiyo maana mnaona kama kwenye barabara hajafanya kitu! Hebu ona, daraja la tanzanite, daraja la Busisi, Meli 2 za ziwa Victoria (1 ukarabati 1 mpyaaaaa), Meli mpya ziwa Nyasa, utitiri wa ndege za ATCL, Bwawa la umeme, SGR, Flyover kila mahali, Bomba la mafuta kutoka Uganda n.k. Hakika JPM asilinganishwe na takataka!
 
Back
Top Bottom