Pre GE2025 Mtangazaji wa ITV na Tundu Lissu hakika mmetutendea haki sisi watanzania kwenye kipindi cha dakika 45

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yeye mwenyewe yuko humu amekupata
 
Mimi namkubali sana Odemba wa Star TV mwamba anajua kuhoji maswali yenye mashiko hakupi mda wa kudanganya akikuona unaokoteza majibu anakuchapa lingine.
 
Yeye mwenyewe yuko humu amekupata
Sawa aanze hata sasa hivi kupost clip ya dakika 1 mpaka 2. Inatosha kupeleka moto 🤣🤣. Na wasanii wakitoa challenge za nyimbo mpya na yeye acheze, na masuala ya mpira na yeye ashiriki hata kutoa comment mtandaoni.
 
Nime kuelewa mkuu. Ninakubaliana na wewe moja kwa moja.
Sasa katika hali ya namna hiyo, sijui kifanyike nini ili hiki "kizazi" kiamke?
labda tumuulize jenerali ulimwengu na mh.warioba maana wamewaamsha sana hamuamki wala kutikisika, eti sasa hivi ndio mnaulizana tena nini kifanyike 🤣

nyie vijana nyie dah 🤣
 
bila michango kwanza sijui kama inawezekana 🐒
 
labda tumuulize jenerali ulimwengu na mh.warioba maana wamewaamsha sana hamuamki wala kutikisika, eti sasa hivi ndio mnaulizana tena nini kifanyike 🤣

nyie vijana nyie dah 🤣
Ukiendelea hivi, hakika tutajadili haya maswala ya nchi yetu vizuri.
Kumbe wakati mwingine akili inakurudia na kuwa sawasawa?
Basi nakuomba tafadhali baki hivyo hivyo, tutajadili kwa utulivu kabisa hatma ya nchi yetu hii.

Lakini ukweli unabaki pale pale. Samia ndiye atakuwa kiongozi wa mwisho wa CCM kama tunavyo ijuwa.
Tutaacha kumulaumu yeye, kwani amekuja kumalizia kazi tu iliyo anzishwa na watangulizi wenzake, ukiondoa waasisi wake.

"Nini kifanyike"? Unadhani hilo ni swali tena wakati huu. Mbona utakuwa umechelewa sana kuuliza swali hilo.
 
Tuendelee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kulibariki taifa hili kwa kutupa mh.Rais SSH....

Mh.Rais ni mwanadiplomasia mbobevu ambaye anaiheshimu katiba inayosema kutakuwa na vyama vingi na vyenye sauti YA UKOSOAJI.....

Mh.Rais amepata kufanya kazi kwenye ASASI ZA KIRAIA(AZAKI)...hii nayo inamuongezea wigo mpana wa UVUMILIVU NA UTHUBUTU WA KUSIKIA MAONI KINZANI....

Kwa wenye macho ya rohoni na wasio na "mbango" ,kwao Chifu Hangaya ni zaidi ya mng'ao wa jina hilo [emoji7]

#Nchi Kwanza[emoji7]
#Heshima yetu waafrika ni kwa VIONGOZI WETU ,WAKUBWA ZETU NA WAZAZI WETU[emoji7]
 
Wengi wetu tunasahau haraka sana....

Mh.Rais alishawahi kupata kusema "nikosoeni mtakavyo" ila MSITUKANE...kwani kwa waafrika matusi si uungwana na heshima ni jambo la kiutu na la lazima[emoji7]

#Nchi Kwanza[emoji7]

#Mh.Rais SSH raia nambari moja[emoji7]
 
Hiyo kazi si lazima aifanye mwenyewe. Mnaoguswa ndo fanyeni hiyo kazi
 
Na wewe pia umetutendea haki kuleta Summary hapa.
 
Peleka utumwa wako huko Porini.

This is civilized World. Huo Udikteta umewafikisha wapi?

Aliyeukazania umeona amepata faida gani?

Usitake kumhusisha Rais Dr Samia na mambo yenu ya kizamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…