Pre GE2025 Mtangazaji wa ITV na Tundu Lissu hakika mmetutendea haki sisi watanzania kwenye kipindi cha dakika 45

Pre GE2025 Mtangazaji wa ITV na Tundu Lissu hakika mmetutendea haki sisi watanzania kwenye kipindi cha dakika 45

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
hashim rungwe alisema hakuna vikao vya maridhiano ni kitchen party tu wanakula ubwabwa wanaondoka na posho kwenye bahasha, sasa huyu lissu kakaa mwaka mzima akivuta posho na kula wali wa abdul halafu anasema eti mazungumzo yamekwama, wameona wasipotengeneza amshaamsha november watatoka mikono mitupu
 
Tuache ushabiki pembeni, mtangazaji wa ITV alijipanga vyema sana katika kufyatua maswali ya msingi yenye kumuweka kwenye kona Lissu, na Lissu aliweza vizuri sana kukabiliana nayo moja kwa moja bila kukwepa, kuzunguka mbuyu au kulipua lipua.

Hakika ulikuwa mjadala mzuri wenye kusisimua na kuvutia kuufuatilia. Kwa uchache, hoja hizi ziligusiwa.

1. Rushwa ndani ya Chadema

2. Fununu za Lissu kutaka kuondoka CHADEMA ili kuanzisha chama kipya.

3. Lissu kuletewa hongo na mtoto wa rais

4. Misuguano ya viongozi ndani ya Chadema

5. Ruzuku kwa vyama vya siasa

6. Utata wa kisheria katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

7. Dhana ya Chadema kuleta uchochezi.

8. Demokrasia ndani ya vyama vya siasa.

9. Mpango wa Lissu kutaka kugombea urais.

10. Taswira nzima ya uendeshaji wa chaguzi za serikali za mitaa.
Naunga mkono hoja
 
Kusema cha ukweli,kwa tulipofikia midahalo haisaidii,sisi watu wa kizazi hiki hatuna attention span ya lisaa lizima wala hatuwezi kudadavua mambo kiundani
Jisemee wewe, mimi muda huo nnao.
 
Back
Top Bottom