Pre GE2025 Mtangazaji wa ITV na Tundu Lissu hakika mmetutendea haki sisi watanzania kwenye kipindi cha dakika 45

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Acha uchonganishi wewe..hakuna kituo Cha TV kinashirikiana na serikali ya awamu ya sita Kama ITV ukiondoa TBC..ni mtazamo wangu lakini..hata hiyo Jana tu Naibu Waziri mkuu alikuwa hapo ITV kudhihirisha dhana ya mashirikiano mazuri Kati ya serikali na IPP media..na jumatatu ijayo nadhani anaweza kuwa kwenye Dakika 45 na Farhia
 
Hili ni wazo zuri sana, kazi hiyo Lissu mwenyewe haiwezi ila anaweza kuisimamia hata kwa muda mchache aupatapo. Cha kufanya ni kwa Chadema kwa vile ina vijana mahiri sana na wenye akili, iundeTEAM ya watu kama 20 hivi watakao fanya kazi hiyo kwa uratibu maalumu wa kumuuza Lissu na kazi zake katika mitandao ya jamii na uratibu wa vyombo vya habari.
Kazi hiyo iwe maalum na walipwe vizuri vijana hao waaminifu na wenye uelewa mkubwa na mapenzi mema kwa nchi, Chadema na hususani kwa Lissu mwenyewe. ITALIPA!
 
Wewe ndugu Kiranja wa jamii ni strategist mzuri sana kwa haya maoni yako.
Nami naamini kabisa hivi ndivyo inapaswa kufanywa.

Kongole sana.
 

View: https://youtu.be/ZL2V3hUw5Hg
 
Hii strategy kaitumia Trump, ameingia TikTok hivi karibuni ili kuwafikia vijana wengi. TL anahitaji timu maalumu kufanya haya.
 
Lissu aje na hoja mpya sio Kila siku hizo hizo
Fafanua hoja mpya zikoje, jadili ili nasi tupate kujifunza ili tusije tukawachosha na hoja za kizamani, akili ya binadamu inahifadhi kila kitu tunacho kiona na kusikia ama kujifunza na uwezo wa kutafsiri tulivyo hifadhi kwenye ubongo ndiyo akili zenyewe, nafahamu kwamba binadamu ana akili sana na binadamu huyo huyo ni mvivu wa kufikiri, lakini pia wale ambao tunadhani wana akili kuahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data
 
Hamna hoja hapo
Kuelewa hoja ni lazima uwe na uwezo, yaani uwe na akili iliyopevuka. Ukikosa, watu wanaweza kuwa wanaongea mambo ya msingi, lakini kitokana na wewe kukosa uelewa, unaona kama wanapoteza muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…