#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Usipende kulaumu laumu kwanza ingejiuliza why hawakufanya kama wewe unavyotaka,wabongo bwana
Acha tulipie uzembe uliosabishwa na serikali toka mwanzo ilishindwa kuonyesha reaction yoyote unashindwa funga mipaka kisa watalii nani bora kati ya mwananchi na mtalii pesa ina thamani kuliko uhai wetu

Nb: Serikali imehusika kwa uzembe ktk hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba tena Mods msiunganishe bandiko hili.

Nimekaa na kuwaza sana jinsi ya kupunguza kusaambaa kwa maambukizi ya ndani kwa ndani (local transmissions) ya COVID-19. Pamoja na watu kuendelea kuzingatia kanuni za afya, hasa dhidi ya maambukizi, uwezekano ni mdogo wa kupima watu wengi kubaini walioambukizwa.

Hivyo, basi kunahitajika mbinu nyingine ya kuwezesha kuwapima watu wenye uwezekano wa kuwa wameambukizwa. Hawa si wengine ila walio karibu sana na ambao tayari wamegundulika wana maambukizi (wagonjwa).

Kwa kuwa karibu kila Mtanzania ana simu na imesajiriwa, yeyote atakayepatikana na maambukizi, itumiwe simu yake kufuatilia na kuchambua mawasiliano yake, katika siku 14. Vivyo hivyo na hao walio wasiliana naye pia wafuatiliwe ili kubaini kama kulikuwa na "physical contact" mbali na mawasiliano ya simu tu. Hii ni kwa sababu mara nyingi mawasiliano ni baina ya watu wanaofahamiana kijamii, kisiasa au/na kiuchumi (kikazi).
 
*Kwenye issue ya Corona wala hapahitaji kuwa na degree kujua kunatumika nguvu kubwa ndani na nje ya Taifa letu kuonyesha* *kwamba Tanzania ni kama Italy yaani watu wanaumwa hovyo na kufa kama kuku wa kideli,*

*Anyway hebu tufanye utafiti mdogo tu tukianza na wewe mwenyewe jiulize mtaani kwako* *vifo vingapi???*

*Wagonjwa wangapiunaowajua???*

*Kisha rudi ndani ya familia yako kuna mgonjwa au kifo cha corona ???*

*Kisha nenda kwa rafiki zako je kuna hivyo vitu ???*

*Kisha jiulize haya tunayoambiwa yanaweza kufanyika sirini???*

*Kwa faida ya nani??*

*Je serikali ndio imeleta ugonjwa huu??*

*Akili kuambiwa changanya na zako ni aibu sana watu wazima kufikiri kama watoto*[emoji57][emoji57][emoji57]

*Sasa nasema hivi tuendelee kuchukua hatua elekezi lakini tukiwa na Imani tumeshinda hii vita ndio maana makelele mengi mnooo kama vile corona iko* *Tanzania tu*

[emoji41][emoji41][emoji41]
*Corona ni hatari lakini hofu ya wapumbavu ni hatari zaidi mkome kutisha watu*[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bado hujafikiwa ndio maana unapanua kinywa hap
 
Alishauriwa mapema kufunga mipaka kwa abiria ili kulinda taifa akawa mbishi akisema miradi itasimama, sasa miradi gani itaendelea wakati watu wanapambana na gonjwa la hatari

sasa miradi yote ndio itaenda kusimama sababu ya kutofikiria, wazungu washaogopa tayari kufanya kazi sehem isiyo na usalama hawataweza,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama bado unang'ang'ania kazi ambayo umesusa huifanyi, kwa nini usishtakiwe kwa uhujumu uchumi? Mtu yeyote anayetaka aeleweke na kuaminika hawezi kufanya mchezo huo mchafu wa kususa wakati wa vita. Ni mpiganaji gani hataki kukosolewa na kuelekezwa pale anapoona amekosea? Huyu si msaliti huyu na hastahili hata kuwa huru uraiani na sembuse kwenye msitari wa mbele?

Hawatufai hawa. wanatakiwa waondolewe na wakae mbali na uwanja maana wataendelea kutusaliti kwa akili zao finyu wakidhani wanamkomoa mkuu wao kumbe wanatuangamiza. wengine nje ya sanduku wapo wengi sana wenye nia na uwezo wa kuenda naye. Pengine hawa wameshakomaa katika mfumo taralila . Sasa hawezi kuwakunja ndiyo sababu wanagangamala.

Anatakiwa aweke watu wapyakabisa ambao hawajafanya kwenye taralila.
Labda wapo kimya kwa maelekezo ya mzee mwenyewe. Mi naona serikali imekosa cha kufanya na kuwaachia wananchi mzigo baada ya ile kauli "Mjifukize" which is not right
 
....sasa miradi gani itaendelea wakati watu wanapambana na gonjwa la hatari....
 
Nchi nzima ina Corona. Kila sehemu imepiga hodi. Tubadili mbinu ya kukabiliana nayo maana mbinu ya sasa imefeli vibaya mno. Nchi inaangamia hii. Ramani hii inaonyesha jinsi Corona alivyosambaa na hao ni walioonyesha dalili wakapimwa.
Screenshot_20200430-090402_Twitter.jpg
 
walikomaa wee na lock down wakashindwa,sasa wameamia kwenye kuwapa watu taharuki,mtu ata kama kaanguka kwa kifafa basi ni corona hiyo!!!

kwenye hili janga wanachambua vitu vibaya ndo wana vishupalia kuvitangaza kuwatisha watu.mazuri ya kuwapa watu faraja hawana haja nayo.

lengo ni kuwapa watu hofu wafe hata kabla ya hicho kijicorona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alishauriwa mapema kufunga mipaka kwa abiria ili kulinda taifa akawa mbishi akisema miradi itasimama, sasa miradi gani itaendelea wakati watu wanapambana na gonjwa la hatari

sasa miradi yote ndio itaenda kusimama sababu ya kutofikiria, wazungu washaogopa tayari kufanya kazi sehem isiyo na usalama hawataweza,

Sent using Jamii Forums mobile app

Hao waliofunga mipaka, nakuuliza, je korona iliisha kwao?? Hivi unajua kinachoendelea katika hizo nchi zilizofunga mipaka kwa sasa kuhusu raia wake wanachokisema juu ya lockdown?

Jamani, hata sisi tuna akili, kwa nini tunapenda sana kuwasikiliza wazungu tuu kwamba kila wanachosema wao ni sahihi?? Kwani vichwa vyetu vimebeba nini jamani??
 
Taarifa za Corona nchini tunazopata kutoka serikalini ni kutokana na maoni, kelele na mawazo ya wanaJF, kwa kiasi fulani ni salama zaidi kupost taarifa ambayo hata Millardayo, TBC ama ITV wanaiogopa kuipost.

Hongera sana wana JF na uongozi wote.

Reliable source nyingine ni huko Twitter ambapo tunamkuta Kigogo2014 pamoja na MangeKimambi.

Tuchukue tahadhari, corona inaua na wengi wanazikwa. Ukiangalia hii picha utagundua kuwa wanaozikwa ni wengi sana, tazama hayo majeneza yanayisubiri kuzikwa. Ndg yetu Bernard asingezikwa hivyo kama kusingekuwa na hili janga la corona
IMG_20200430_161224.jpg
 
Taifa limepoteza dira, watu wamekuwa kama wanga kila kona watu wanakata majani ya miti mbalimbali hili yajivukize... Hii si sahihi kabisa,

Virusi vya Corona hadi sasa hakuna tiba wala chanjo, huwezi pona Corona kwa mvuke wa majani ya miti ambayo kiuhalisia haujui yanatibu nini.

Mvuke ukiingia mwilini unapozwa mara moja ndo maana mtu anatoka jasho, huwezi tegemea mvuke kuchoma kirusi ndani ya cell za mwili wako na kukiua afu wewe ubaki salama, vitakufa vyote, cell na kirusi kama itakuwa hivyo.

Matangazo ya tiba asilia yamefanya watu wenye dalili za Corona kukaa nyumbani na kujivukiza pasipo kwenda hospitali kucheki kama wana Maambukizi.

Hii ni aibu kwa taifa, tufuate muongozo wa kisayansi juu ya kukinga na kupambana na Covid 19,

Tukitegemea miti shamba kutibu Corona pasipo tafiti za kisayansi tutapoteza maisha ya wanzania wengi

Serikali isione aibu, ikubali kuwabishakosea kuchukua hatua swali lakini bado tuna nafasi ya kurekebisha makosa.
 
Back
Top Bottom