Moja kwa moja kwenye mada.
Hakuna shaka yoyote kuwa dunia imekumbwa na janga ambalo changamoto zake ni kubwa mno kuliko hata za vita vikuu vya pili.
Wazito wengi wa dunia hii walilielezea hili kwa ufasaha wakiitisha mataifa kujiandaa. Hii ikiwa mapema sana hata kabla ya janga hili kutufikia.
Wapo wengi tu (wakiwamo viongozi wetu wa serikali) hapa kwetu, tunaowajua kwa majina na hata kwa ID fake walilipuuzia na kudunisha tahadhari za suala hili vilivyo, ati kuwa:
1. Ni ka upepo tu katapita.
2. Hili ni gonjwa la watu weupe, weusi sisi hayo tunaugua sana magonjwa kama hayo tunapona.
3. Ni ka mafua tu.
4. Huu si ugonjwa wa nchi za hiyo.
5. Huo ni ugonjwa wa nchi za baridi nk, nk.
Yaani kila mmoja alisema lake na leo tunapopukutika wame uchuna. Wako kimya kama vile hawakuwahi kuwapo.
Matokeo yake hawakuweka mikakati yoyote madhubuti kuuzuia ugonjwa kuingia nchini.
Vivyo hivyo hata leo haieleweki wana mkakati upi kuwahami wananchi wakati ugonjwa umefikia hatua ya kusambaa na kuleta madhara kwa kasi tunayoiona.
Kenya dhidi ya uchumi waliamua kulinda watu wao:
Rwanda na Uganda waliamua kuhami watu wao dhidi ya uchumi. Kama ilivyo kwa Kenya ma amiri jeshi wao wakuu ndiyo wako mstari wa mbele kwenye mapambano kuongoza vita.
Siyo manesi kwani hii ni vita tena vita kubwa isiyo kuwa na mfano. Manesi hutunza (huuliza) wagonjwa vita hupiganwa kutokea katika command centers:
Tuelimishane wenye kufahamu:
Mkakati wetu au mikakati yetu ni ipi kututoa kwenye takwimu hizi mbaya zisizokuwa na sifa wala mwelekeo?
Hii mipasho ya kuwa rais si nesi wa kuongoza vita hivi inaweza kuwa haitusaidii sana.
Kulinda uchumi dhidi ya maisha ya watu, dhana hii ina mashiko yapi?