Kwanza tukupongenze kwa namna ulivolipokea na kulishughulikia tatizo LA Corona,hukuruhusu hofu, ukamtanguliza Mungu, ukauona ni ugonjwa ambao hautofautiani sana na magonjwa ya kawaida ya Waafrika ambayo hayawapi shida sana katika maisha yao ya kila siku kama vile Mafua makali lakini pia hukupuuza taratibu za kitaalamu.

Vilevile umeheshimu na kuthamini utamaduni wetu wa mitishamba ambayo ina nafasi kubwa sana katika mchango wa afya za watanzania na kwanza hata madawa mengi ya kizungu hutokana na Miti ya asili.

kwa namna ulivolishughulikia tatizo hili,umelishughulikia kishujaa kama ambavyo unapotaka kushinda changamoto yeyote njia ya kwanza ya ushindi ni kupokea changamoto hiyo ukiwa umeishinda tayari, siyo kama imekushinda kwa hiyo ili technique hiyo itimie ni lazima usiwe na hofu,uibeze na upambane nayo kwa kutumia jitihada zozote,hata siraha ambazo unadhan ni hafifu kama mikuki, rungu, mundu, jambia nk we tumia so lazima mabomu ndo upambanewaweza shangaa siraha duni kama hizo zikawa na mafanikio makubwa kuliko madawa yanayocheleweshwa kwa kufanyiwa tafiti huku watu wakiangamia.

Na sasa umetamka unafikiria kifungua michezo ili iendelee,sisi tunasema hayo ni maono mazuri si michezo tu fikiria na mengine zaidi wakati wizara ya afya inatekeleza yafuatayo, katika kambi za karantini kuwepo na program kabambe za kujifukizia, hizo dawa za wenzetu wa Madagascar zitakapofika zisambazwe vizuri ktk kambi za karantin na zitumike vyema na wagonjwa watolewe hofu tuna imani kwa techniques hizo watu watakuwa wakifikishwa karantini na kuruhusiwa kurudi katika familia zao wakiwa wamepona kabisa.Tunakutakia mapambano mema tukikuombea kwa Allah akutangulie uwavushe watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una mwandiko mbaya sana Eni wei huyo unayemsifia hakuna cha maana chochote alichokifanya zaidi ya kukumbia kama Mwizi tu.

Tuwe humble alafu tujifunze kutosifia ujinga
 
Wanabodi,Fikiria watoto wako, Familia yako itasaidiwa na nani au itaishi vipi kama hutachukua tahadhari

Watu sasa wameamua kuvua barakoa na kujichanganya mitaani, Hii ni hatari tena kubwa, Vijiwe vina Endelea kama kawaida huku watu wakirushiana mate

Tuache siasa, Maisha ni ya mtu binafsi, Kurahisisha sana itatugharimu kama Brazil Leo wanaishiwa majeneza ya kuzikia

Nchi ya Brazil, Wao walipewa morali na wao wakazidi kula bata na kuacha kuchukua tahadhari Leo serikali yao hata kuzika Raia imechoka

Tufanye kazi, lakini fikiria familia yako na watoto wako kwanza, Wewe ukiondoa Pengo lako linazibika muda huo huo

Wengi hapa mapengo yao kwenye biashara au ofisi yalishazibwa unasubiriwa tu uondoke Halafu nafasi apewe mtu

Sasa ukipita mitaani watu wanakaa kwenye magenge na vibaraza, Hofu hakuna tena, Maisha ni wewe jikinge, Chukua tahadhari

STAY HOME STAY SAFE, kama unaweza kufanya kazi ukiwa nyumbani fanya kazi ukiwa nyumbani

Kama unaweza kumaintain social distance fanya kama viongozi wanavyofanya kwa sasa hawamsogelei mtu
 
Kwenye siasa mwenye thamani ni wewe uliye hai, marehemu hapigi kura, hivyo hawanasababu ya kujali wanaokufa.
 
Wakuu corona haikwepeki, mpaka pale chanjo itakapo patikana. Hivyo ukitaka uwe safe kaa nyumbani usitoke wala kukitana na mtu yeyote yule hadi pale utakapo chanjwa, kama chanjo itapatikana.

Hata hizi mbinu za social distancing ni mbinu za kujaribu kuchelewesha watu wengi wasiambukizwe kwa mara moja. Ndo maana wanaita flarterning the curve...yaani kufanya wanaogoa kwa wakati mmoja wakawa nearly costant ili kuwezesha kupata huduma za kitabibu pale wanapohitaji.
 
Haiwezekani mwanafunzi asisome miezi 5 then ahame darasa, Ni Bora wakakalili madalasa na wizara ijipange tayari kwa hilo.

NB: watoto bado hawalindwi vya kutosha kipindi hiki, mtaani wapo tu na hawapewi barakoa, hivi zile kampeni za mataulo kwa wasichana haziwezi hamishiwa kwa barakoa kwa watoto wote kugawiwa bure maana naona hatari kwa watoto 😪
 
hii ndio likizo ambayo watoto wa kike(wanafumzi)wamefanywa sana matusi kuliko kipindi chochote tangu dunia iumbwe,subirini miezi mitatu ijayo muanze kusikia idadi ya visa vya mimba,naamini itakuwa kubwa kuliko mkasa wote wa Corona..
 
Ili kupunguza msongamano kwenye usafiri wa umma nashauri bus aina ya tata youtong na zongtong ndio zitumike na ziwe na seat za 2x2 na hakuna kusimama abiria, ziwe na sanitizer mlangoni na kila abiria avae barakoa muda wote wasafari.

Ili hili litekelezike Ni vizuri nauli za buses zitakazotoa huduma hizi ziangaliwe upya. Napendekeza nauli iongezwe kutoka Mia nne/tano Hadi elfu moja. Nauli hii Ni rafiki kwani ndio iliozoeleka kwenye Bajaj na bodaboda.
 
Bila shaka wewe utakuwa dereva au kondakta wa daladala,unataka kufidia level seat!
 
Bei ya mafuta imeporomoka sisi ndio kwanzaaa nauli zipande!!
Kuweni na huruma
Alieturoga hii nchi alishakufa, maana ni mtafaruku kuanzia bungeni mpaka viongozi serikalini mpaka viongozi wa dini. Wamekaa kinafiki kinafikiiiiii tu na uongo uongoooo.

Wala si jambo la kushangaa au kujiuloza kwanini COVID-19 inawawinda "VIONGOZI" kwa kasi. Maana si viongozi wa dini wala bungeni walivojaa "UNAFIKI".
 
Nahitaji ufafanuzi mpana kwa jinsi magu anavyolibeba hili janga na akiendelea kutuhamasisha tuondoe hofu na tujifunze namna ya kuishi na ugonjwa wa huu corona!

Swali:

Kuna jinsi watu wanaweza kujifunza jinsi ya kuishi na ugonjwa wa mripuko zaidi ya kuudhibiti ukaisha??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…