#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Serikali imeanzisha program maalum ya ufundishaji wa umahiri wa marejeo ya masomo kwa njia ya TV, redio na online TV's. Ofcourse, it is a good idea lakini kuna hali ya ubaguzi fulani kwenye hii program kwa sababu siyo wanafunzi wote wananufaika nayo.

Kwanza, siyo wanafunzi wote, wazazi wao wana uwezo wa kumiliki TV au simu janja. Pili, umeme bado ni changamoto hasa maeneo ya vijijini. Tatu, masomo yanayohusisha calculations kama vile hesabu, fizikia na kemia ni ngumu kuyafundisha kwa njia ya redio wanafunzi wakaelewa. Nne, uwezo wa kununua vifurushi vya data(mb) ili kuaccess masomo hayo kwenye mtandao wa YouTube pia ni tatizo.

Kutokana na changamoto hizo ni bora shule zifunguliwe ili wanafunzi wote waendelee na masomo katika mfumo rasmi. Ukizingatia hali ya maambukizi ya ugonjwa wa corona siyo ya kutisha sana kwani tangu gonjwa hili limeingia nchini mpaka sasa ni vifo 16 tu vimeripotiwa.

Binafsi napendekeza shule zifunguliwe mwezi wa sita wanafunzi waendelee na masomo pale walipoishia. Hii itasaidia kuepusha mkanganyiko wa ratiba ya masomo siku za mbeleni endapo shule zitachelewa kufunguliwa. Kwakuwa ni miezi 3 itakuwa imepotea basi likizo ya mwezi wa 6 baada ya shule kufunguliwa isiwepo, likizo ya mwezi wa tisa pia na likizo ya mwezi wa 12 ili kufidishia miezi iliyopotea.

Pamoja na serikali kuzuia mikusanyiko bado watu wakiwemo wanafunzi wameendelea kukusanyika makanisani, misikitini, minadani, masokoni na baadhi ya wanafunzi wanaonekana magengeni na mitaani wakifanya biashara ya kuuza maandazi,mayai, karanga, ubuyu n.k. Kwahiyo ni bora shule zikafunguliwa waendelee na masomo kuliko kuwaacha wakizagaa mitaani kwa sababu huko ni hatari zaidi kuliko wakiwa shuleni.
 
Shule zifunguliwe Watoto wetu Waambukizane ili wafe si ndio??.. Ni bora mara 100% watoto wangu wawe salama, ugojwa utaisha watasoma tu ni imani yangu. Watoto ni zawadi toka kwa Mungu so kuwaexpose kwenye gojwa ili hatari ni dhambi kwa Mungu.

Watoto wangu ni wathamani kufanya politics na Maisha yao binafsi siko tayari na sitokubali. Muda si Mrefu Gojwa hili litatoweka na watoto wetu watarudi shule kuendelea na masomo lakini si kwa sasa ambapo jamiii kuna sintofahamu kubwa..
 
Kakovid19 kikibahatika kuingia boarding school,itakuwa shida sana maana mazingira ya shule zetu wote tunayajua,tusiwe na haraka sana,bora mtoto arudie mwaka kuliko kumzika,tuwe makini na maneno ya wanasiasa wetu,m7 jana kasema hafungui,Rwanda mpaka mwezi wa 9.....Tz tusijifanye wajuaji Sana tutaumbuka (japo siombei Ivyo) ila Corona ipo
 
Bora watoto wawe chini ya wazazi wao ndo watakaa salama.
Hali ya shule zetu ni risk sana.
Hata mamlaka husika inatambua hali ya maambukizi ni mbaya
 
Mawazo yako ni mazuri lakini ni vema kusubiri hili gonjwa liishe. Ingawa naona takwimu hazioneshi watoto wakiathirika lakini hili si jambo la kuwa na uhakika nalo sana.

Shule zetu nyingi hasa za msingi na sekondari za serikali bado msongamano ni mkbwa sana wa wanafunzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kufungua shule ni ngumu kama ulisikia wazo la bwana mkubwa kufungua michezo pale lengo ni kupata kodi shule hakuna kodi tutakayo kusanya zaidi ya kutoa ela serekalini only
 
Hatuigi mbinu za wengine na mpaka sasa hakuna mtoto kuanzia nursery school mpka Chuo Kikuu amesha thibitishwa kuugua corona
Kakovid19 kikibahatika kuingia boarding school,itakuwa shida sana maana mazingira ya shule zetu wote tunayajua,tusiwe na haraka sana,bora mtoto arudie mwaka kuliko kumzika,tuwe makini na maneno ya wanasiasa wetu,m7 jana kasema hafungui,Rwanda mpaka mwezi wa 9.....Tz tusijifanye wajuaji Sana tutaumbuka (japo siombei Ivyo) ila Corona ipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shule na vyuo vitafunguliwa baada ya dawa ya corona na chanjo ya corona kugunduliwa na kuthibitishwa na WHO na kisha kusambazwa duniani kote ikiwemo Tanzania. Na huo ndio utakuwa mwisho wa corona.
 
Hatuigi mbinu za wengine na mpaka sasa hakuna mtoto kuanzia nursery school mpka Chuo Kikuu amesha thibitishwa kuugua corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo akili za kijinga hizi,mbona zimefungwa? Na sina muda wa kubishana na mtu mwenye upeo mfupi kama wako.......zilipofungwa mbona kulikuwa hakuna Case yoyote ya mwanafunzi or mwanachuo si wangeendelea cos ugonjwa uliletwa toka nje? Unadhani Tz wapo smart kuliko hao wengine wanaochukua tahadhali?

Tunajiona wajuaje kumbe zero kabisa
 
Shule na vyuo vitafunguliwa baada ya dawa ya corona na chanjo ya corona kugunduliwa na kuthibitishwa na WHO na kisha kusambazwa duniani kote ikiwemo Tanzania. Na huo ndio utakuwa mwisho wa corona.
Kwa mfano chanjo isipatikane kabisa. Shule hazitafunguliwa mkuu??
 
Hakuna tofauti kati ya wanafunzi kurudishwa nyumbani na kuanza kuzagaa zagaa mitaani ovyo na wanafunzi kukusanyika mashuleni, tena mazingira ya mtaani ndio hatarishi zaidi,
 
Mpango huo wa Mass Screening tunao boss?
Sina hakika sana kwa hali inavyoonekana .


Nahii inamanisha kua, kuwaruhusu watoto Warudi mashuleni bila kujua ninkwa kiwango gan corona imedhibitiwa, ni sawa wa kuweka roho zao rehani.

Yaani hapa ni ama

Ipatikane Chanjo

Au ipatikane Tiba.

Kisha ifanyike Mass screening ndo sasa Watoto waruhusiwe kurudi mashuleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom