Mdaiwa-Sugu
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 284
- 912
Serikali imeanzisha program maalum ya ufundishaji wa umahiri wa marejeo ya masomo kwa njia ya TV, redio na online TV's. Ofcourse, it is a good idea lakini kuna hali ya ubaguzi fulani kwenye hii program kwa sababu siyo wanafunzi wote wananufaika nayo.
Kwanza, siyo wanafunzi wote, wazazi wao wana uwezo wa kumiliki TV au simu janja. Pili, umeme bado ni changamoto hasa maeneo ya vijijini. Tatu, masomo yanayohusisha calculations kama vile hesabu, fizikia na kemia ni ngumu kuyafundisha kwa njia ya redio wanafunzi wakaelewa. Nne, uwezo wa kununua vifurushi vya data(mb) ili kuaccess masomo hayo kwenye mtandao wa YouTube pia ni tatizo.
Kutokana na changamoto hizo ni bora shule zifunguliwe ili wanafunzi wote waendelee na masomo katika mfumo rasmi. Ukizingatia hali ya maambukizi ya ugonjwa wa corona siyo ya kutisha sana kwani tangu gonjwa hili limeingia nchini mpaka sasa ni vifo 16 tu vimeripotiwa.
Binafsi napendekeza shule zifunguliwe mwezi wa sita wanafunzi waendelee na masomo pale walipoishia. Hii itasaidia kuepusha mkanganyiko wa ratiba ya masomo siku za mbeleni endapo shule zitachelewa kufunguliwa. Kwakuwa ni miezi 3 itakuwa imepotea basi likizo ya mwezi wa 6 baada ya shule kufunguliwa isiwepo, likizo ya mwezi wa tisa pia na likizo ya mwezi wa 12 ili kufidishia miezi iliyopotea.
Pamoja na serikali kuzuia mikusanyiko bado watu wakiwemo wanafunzi wameendelea kukusanyika makanisani, misikitini, minadani, masokoni na baadhi ya wanafunzi wanaonekana magengeni na mitaani wakifanya biashara ya kuuza maandazi,mayai, karanga, ubuyu n.k. Kwahiyo ni bora shule zikafunguliwa waendelee na masomo kuliko kuwaacha wakizagaa mitaani kwa sababu huko ni hatari zaidi kuliko wakiwa shuleni.