#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Shule na vyuo vitafunguliwa baada ya dawa ya corona na chanjo ya corona kugunduliwa na kuthibitishwa na WHO na kisha kusambazwa duniani kote ikiwemo Tanzania. Na huo ndio utakuwa mwisho wa corona.
Kujifukizia sio dawa?,
 
Mheshimiwa Rais, pamoja kuwa watu wako huru kufanya chochote kipindi hiki cha Corona, toa amri basi angalau kila mtu nchi nzima iwe ni lazima kuvaa barakoa.

Utafiti unaonesha hata barakoa ikiwa ya kitambaa husaidia mwathirika akikohoa mate yasiruke na kusambaza virusi, lakini pia huzuia uwezekano wa mtu kujigusa mdomoni, machoni na puani na kuambukizwa virusi.
 
Yeye ulishawahi kumuona amevaa? Si anasema mabeberu yameziwekea Corona.
 
Kama WHO wakiithibitisha kitaalam na vipimo vya dozi vikifanyiwa utafiti ikikubaliwa na uthibitisho wa uwezo wa dawa kama dawa inaponya kabisa basi WHO watasema kujifukiza ndio dawa rasmi ya corona.
Kuna ugonjwa unaitwa uzwazwa huu specifically kwa watanzania tu WHO watapima inawahusu mini?
 
Huyu mzee amesimama kidete katika Taifa lake, anatoa maelekezo yenye mantiki na yasiyo na mkanganyiko. Anaongea Kama mzazi Kama mlezi na Kama mtu anayetambua wazi kuwa kuishi nimara moja tu na Vita ya kupigania uhai inapewa kipaumbele kwani ukifa umeondoka.

Natamani kuwaona viongozi wa Tanzania hasa wenye dhamana wakisimama na kuelekeza mikakati waliyonayo
 
Kwa muda wa wiki 2 au 3 kwa dar pekee yake tumepoteza wachungajinkaribia 4 wenye uzoefu.

Najiuliza kuna nini?

Pamoja na hilo linakuja swala la kupoteza wabunge na viongozi wakubwa.

Siamini kama ni corona.

Wasiwasi umetanda , hapa Geita kuna mzee wa kanisa kafa ghafla, hata kanisani sasa wanaenda watu wachache sana kibishi.

Jamani Imani zinajaribiwa.

Sometimes nashika kichwa tuu, sijui wapi kwa kukimbilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom