#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Makaratasi Yale wanayobadilishana mule Bungeni ni hatari sana kwenye kusambaza Covid -19.so kwa mtu anayejijari kila baada ya kushika kitu toka kwa mtu mwingine hata Kama ni pesa ni muhimu kunawa mikono kwa sabuni au kutumia sanitizer
Hapo kwenye pesa watashikwa wengi..
 
Huu ugonjwa ni hatari sana umegharimu maisha ya watu duniani mpaka sasa Usa pamoja na kujinadi kuwa ni taifa lenye uwezo kwa kila kitu lakini takribani 70000+ wamefariki.

Hapo juzi FDA ya Usa wameruhusu dawa aina ya Remdesivir ianze kutumika kwa ajili ya matibabu. Hii ni kwa sababu dawa hii imeonyesha uwezo wa kutibu mtu aliye mahututi kwa haraka sana. Kwa mujibu wa Cnn wataalamu waliohojiwa wanasema dawa hii inauwezo wa kutibu mgonjwa wa Covid-19 aliyehoi ICU na akapona ndani ya siku tano.

Habari njema kwa mujibu wa Cnn ni kuwa kwa nia njema kabisa taasisi ya Giliaed ambayo iligundua dawa hii imetoa kibali kwa kampuni mbali mbali ili iweze kutengenezwa kama copy ili watu waweze kutibiwa.

Hivyo hata serikali yetu pamoja kuwa na nia nzuri ya kutaka kuagiza dawa toka Madagascar huu pia ni wakati mzuri wa kuomba kibali hii dawa iweze kutengenezwa hapa na iweze kuwasaidia wagonjwa wa Covid-19.

Ni ombi tu kwa serikali yangu ili tunusurike na hili janga. Maana ni lazima tujaribu kila namna ili tujinusuru.
 
Kumekuwa na tabia ya kuhusisha vifo vingi vinavyotokea wakati huu na ugonjwa wa Corona kiaso cha kupotosha ukweli.

Tunapaswa kufahamu kuwa kuna watu ambao clinic zao zilikuwa India, Afrika ya Kusini n.k kutokana na maradhi yanayowasumbua na kwa kuwa wakati huu usafiri wa ndege umezuiwa katika maeneo mengi hivyo wanakosa huduma muhimu na wakiaga Dunia sidhani kama ni sawa kusema ni Korona.

Kuna vigogo wengi wanaumia sana wakati huu kutokana na kusimama kwa usafiri wa anga ,tujaribu kuona na hili pia ili tusije tukajipandikizia imani potofu zaidi.
 
Katika wale waliofariki so far unaweza kutaja wangapi ambao wamefariki sababu ya kushindwa kwenda clinic India au Afrika kusini sababu ya magonjwa mengine?

Kama hutaki kutaja majina hebu taja idadi tu
 
Katika wale waliofariki so far unaweza kutaja wangapi ambao wamefariki sababu ya kushindwa kwenda clinic India au Afrika kusini sababu ya magonjwa mengine?

Kama hutaki kutaja majina hebu taja idadi tu
Logically wapo kwa sababu hali hiyo ipo.
 
Wanaokufa ni wachache hivyo sisi tumeamua watakaondoka waondoke na watakaobaki wapige kazi!
 
Umesema kweli, wazee tulikuwa tunaenda kuchaji battery low zetu Asia na Europe huko, sasa hali imebadilika hofu imetanda, twafwaaa.
Mungu aturehemu hakika.
 
Yaelekea watu tumeingiwa na hofu ya maambukizi ya COVID-19 kiasi tunaogopa kwenda hospitali kwa tiba ya magonjwa mengineyo, kuogopa kugundulika na maambukizi. Matokeo yake watu wa aina hii wanahatarisha maisha yao.

Ninao ushahidi wa baadhi ya watu ninaowafahamu ambao ni wagonjwa wa maradhi tofauti na COVID-19 ambao wameamua kujitibia nyumbani. Chonde chonde usihatarishe maisha yako, nenda hospitali.

Unayesoma ujumbe huu, kama unamfahamu mtu wa aina hiyo mshauri aende hospitali, ikiwa vipi mlazimishe. Si kila homa, mafua au kikohozi ni ambukizo la COVID-19.

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE UWAPENDAO.
 
.
IMG_20200428_172243~2.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom