Shida iko sehemu moja mkuu, Wenye nyumba wakipunguza Kodi je na wao Serikali imewapunguzia Kodi? Maana unaweza kupunguza Kodi harafu ukakosa pesa ya kulipa Kodi ya Serikali
 
Nimewaza tu jinsi tulivyoelekezana kitaani kutengeneza sanitaiza, kwa uchumi wetu huu wa hand to mouth inafikirisha sana ,kikubwa tumwombe Mungu tu,

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Mkuu ninakushauri usimini sana taarifa za Covid19 kutoka Kenya. Viongozi wao wengi ni wapiga dili, wanaweza kuandaa taharuki ili waibie wananchi. Vilevile usiamini DR Congo, Sudan, South Sudan, Ethiopia na nchi nyingi ambako rushwa ni kama jadi yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana tunaendelea kuwa masikini hutujiongezi kutafuta tusiyoyajua kwenye uchumi/sayansi....
tunasubiri kukopi tu.
 
Bashite aoneshe mfano kwa kupunguza bei za dawa kwenye Phamacy zake badala ya kutaka wenye nyumba wasitoze. Kodi!!

Bashite inaelekea hajui kuwa wenye nyumba wanalipa kodi za viwanja kwa serikali kila mwaka zinazotokana na kodi za pango; sasa kama anaona ni busara wenye nyumba kusitisha kutoza kodi basi angeshauri na serikali isitishe kodi za viwanja!!!
 
Ili kupata projection ya uhalisia wa athari za Corona nchini kwetu kwa siku za usoni, ninaishauri serekali iwe ina monitor hii kitu inaitwa "Fatality Rate" ambayo inapatikana kwa ku calculate idadi ya vifo gawanya kwa jumla ya maambukizi.

Kwa kigezo hiki, takwimu hadi leo asubuhi zinaonyesha kuwa Tanzania ina "COVID-19 Fatality Rate" kubwa kuliko nchi zote katika EAC block, kama hesabu hizi hapa chini zinavyothibitisha:

Tanzania 1/20 = 5.0%
Kenya 3/110 = 2.7%
Rwanda 0/84 = 0%
Uganda 0/45 = 0%
Burundi 0/3 = 0%

Ili tuweze ku improve kwenye score hii, inabidi tuongeze uwezo (in terms of testing centres & equipment) wa upimaji ili tuwe na sample size kubwa.
 
Tahadhari hii ni ya muhimu sana.

Katika mambo ya kisayansi,data hutoa picha na kutumika kama dira.

Tunakushukuru umekuja na hoja ya msingi sana.
tatizo chini ya awamu hii kila kitu ni siasa siasa siasa.

hakuna kiongozi yoyote chamani na kwenye kabineti (hata maprofesa) anayeushughulisha ubongo wake.
wote naona wamegeuzwa kuwa ni roboti tu huku mwenye rimoti akiwa kule Chato!
 
Ili iweje?

Anza kujikinga mwenyewe kwanza, kwa kufanya hivyo utakuwa umeikinga na jamii.
 
Kwa kigezo hiki, takwimu hadi leo asubuhi zinaonyesha kuwa Tanzania ina "COVID-19 Fatality Rate" kubwa kuliko nchi zote katika EAC block,
Duh.. !. Mkuu Mbabe, tusutishane.
Imeelezwa vifo vya Corona vinatokana na udhaifu mwingine uliokuwepo mwanzo, Corona ikaja kukusindikiza tuu.
Please please please, tusitishane!.
P
 
Kile kimama ummy kije hapa kijifunze kitu kinachoweza isaidia nchi kupambana na huu ugonjwa sio kinakuja na idadi ya ndoo na cock za maji utadhani kibibi maji
Ummy ndiyo alikuletea Corona?

Anza Kwa kujikinga mwenyewe usitegemee Ummy au mwengine yeyote kuwa anaweza kujikinga na maambukizi kama wewe mwenyewe huchukuwi tahadhari.

Kumbuka tu, kujikinga na tahadhari zako zote hakumaanishi kuwa ikiwa wa kufa kwa Corona basi kuna cha kuzuwia.

Moja ya tahadhari ni kujitayarisha kisaokolojia kuwa corona yupo na unaweza kumzuwia asikupate na akikupata basi hatokuwa na madhara makubwa kwako na kwa jamii inayokuzunguka Kwa kuwa umejiandaa na kujitahadhari nae vya kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…