Nipo Dar es Salaam, eneo la Karakata karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius K. Nyerere. Sakata la Corona linavyosemwa mitandaoni na kwenye media lipo tofauti sana na uhalisia wa maisha yetu huku. Mass media zinaongeza presha zaid kwa wananchi kuliko ilivyo kawaida ktk uhalisia, Corona inasemwa tu midomon na tunasikia sikia mambo mengi kuhusu corona kila siku lakin hata hivyo shughuli zinaendelea kama kawaida, na misikitin tunakusanyika. Waislamu tuna tabia ya kusalimiana kwa kushikana mikono au hata kukumbatiana, na wakat mwingine misikiti inajaa sana kias cha kubanana, hivyo hatukai mbali mbali na hili linaendelea kama kawaida wala hatuna khofu ya corona zaid ya kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu. Ukitazama watu wanavyoishi huku ni kama corona haipo, maisha yanakwenda bila khofu. Watoto wanatoka pia kuhudhuria ibada na magengeni tunawatuma. Suala la biashara huhusisha zaid mabadilishano ya fedha mkono kwa mkono, hili linafanyika vizuri bila khofu yoyote na wala hakuna anayevaa hizo mask isipokuwa hunawa kwa.sabuni na maji safi tu. Ikiwa haya yanawezekana, tusemeje kuhusu shule ambazo ni mikusanyiko ile ile kama ilivyo ktk ibada, masokoni, magengeni, bungeni, kwenye PS watoto wanakocheza games n.k? Kuna mambo mengine yameshakadiriwa, alilopanga Mwenyezi Mungu likufikie hata uende wapi au ujifungie ndani miaka 10 na uwe unapatiwa huduma zote bure bado litakufika tu. Kikubwa watu wachukue tahadhari zisizoleta athari kubwa ya kuendesha maisha yao wakat huo huo wakimtegemea Mungu kama mlinzi wao. Corona si chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Maamuzi kama hayo wazungu wanajuta na wanakufa zaid ktk majumba yao. Jiulize Corona inafikaje ktk nyumba zao? Kila kitu na Qadar. Serikali isichukue maamuz ya kukopi kutoka kwa wazungu pasina kujua athari zake kubwa. Siku ikipitisha kauli et watu wakae ktk majumba yao na asitoke yeyote na kila shughuli ifungwe basi tutarajie vifo vingi zaid kutokea kuliko ilivyo sasa, najua wazi vifo hivyo itasingiziwa Corona pejee ndo imepelekea na si maamuzi yao mabovu.

Tuwe makini sana ndugu zangu, kila.mtu anazungumza lake pasina kuleta fikra sahihi mbele kuna nini au kutatokea nini.

Acheni kuwaabudu wazungu kwa fikra zao, kila kitu wakifanya au wakisema nyie mnashika tu yan hata hamfikirii, na media zinatia preaha zaid, huu ni msiba mkubwa sana. Afrika bado tunatawaliwa kifikra na si kiuchumi pekee kama wengi waonavyo.
 
huu uzi ulianzishwa na mtu wa PRAISE TEAM
 
Exactly what I was thinking tufanye inter regional lockdown. Tufunge communication between mikoa.hakuna kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Jeshi lisimamie hili kama sisi wa dar kwakuwa tushafanya uzembe umeingia basi tukomae nao tu peke yetu tuokoe wengine.


Waziri asiombe watu kutotoka dar atoe amri watu wasitoke wala kuingia dar na amri isimamie na Jeshi LA wananchi ( JWTZ). Ili watu wawe scared hata kujaribu kupinga amri


Kama maswala ya chakula uwekwe utaratibu maalumu kwa kila atakae toka na kuingia ( watu wachache na wapimwe kabla na baada ya kuondoka).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi watu wanaotumia mbaka badala ya mpaka wananiudhi kweli kweli
 
Hii dhana na mungu kuwaadhibu wazungu kwa kuwa hawana dini nashindwaga kuelewa ukizingatia kuwa kwa upande wa wakristo hao wazungu ndio wameleta hiyo dini.

Na wao wazungu wakise waafrika wanakufa kwa ukimwi sana kwa kuwa mungu anawaadhibu kwa uzinzi uasherati na umalaya watakuwa wamekosea ama?
 
We are too late broo kwa saivi hatuna chakufanya tusubiri kifo tuu

Tuendelee kusintizer mikono na mask huku tukijua kifo kiko around
 
Watakuambia Korona haijaletwa na serikali. Ni natural disasta.
 
Naunga mkono hoja.

Nina nyongeza katika hili.

1. Wakizuia kutoka na kuingia Dar, wajitahidi kuchukua vipimo nyumba kwa nyumba hapa Dar. Hii itasaidia kupata uhalisia wa maambukizi kwa Dar.

2. Kama wataalam wa afya wa kiraia hawatoshi basi waazime kutoka kwenye Majeshi yetu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
We mjamaa wewe yaani simple hivyo kweli??? hiyo itakuwa sio COVID-19.
 
Movements za kipindi cha pasaka zitaisambaza corona mpaka vijijini, Dar iwe ya kwanza kupigwa lockdown
 
 
Wakikusikia na kutekeleza mshukukuru Mungu.
Yule raisi wa jiji anaweza kuwakusanya tena RAIA wake stendi mojawapo na kuwaambia wapige Nazi.
Bora ukose mali, upate akili.
 
UKO SAHIHI 100%
 
Hawawezi kukusikiliza.
Wanataka sana pesa ya kutoka imf ya misaada ya covid19.
Kiufupi serikali ipo Kwenye mikono ya wapumbavu
 
Mkuu kiongozi wa Dar aletwe Mwanajeshi,.Dar iwe chini ya amri za kijeshi hadi Corona itakapoyeyuka
Huu uswahiba unatupeleka pabaya sana
kama taifa, vinginevyo tumekwisha Amen.
 
Kama ni hivyo mbona sijawahi sikia vifo 600 kwa siku?
 
Hii serikali inaonekana imechoka kabisa anatangazwa vifo tu na wagonjwa,nyuso aa viongozi zinamashakamashaka as if they know how to do uwezo hawana,ni peas hamna au order ya boss imewafunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…