Ninaandika uzi huu kwa masikitiko kwani masikilizano ya kindugu yaliyokuwapo nchini mwetu tokea enzi za mwalimu kwa hakika kwa sasa yametatizika sana.
Katika awamu zote za awali, kuhoji, kujadili, kushauriana nk (kwa hoja) bila kujali itikadi, yalikuwa mambo yaliyokuwa yakipembejewa vilivyo. Busara za watu wetu zilikuwa karibu, kutumika kwa manufaa ya taifa.
Leo hii wako wapi wahadhiri na maprofesa nguli ambao mada zao moto moto ziliifanya jamii isisinzie? Yako wapi magazeti na majarida yaliyokuwa yamejipambanua kuwa siyo ya udaku? Wako wapi wanasiasa waliokuwa wanalichemsha bunge likachemka vilivyo na kuwaweka viongozi katika nafasi zao halisi kama watumishi wa wananchi?
Enzi hizo hoja ipi ya manufaa ya taifa ilikosa kudadavuliwa vilivyo tukawa na msimamo wetu wa wazi kama taifa kwa kushindana kwa hoja?
Leo hii tumekabiliwa na tatizo la Corona. Tujiulize (kwenye hili) mawazo ya manguli wetu yako wapi? Mawazo huru ya magazeti, radio, nk yetu yako wapi? Mawazo ya wanasiasa wetu yako wapi?
Leo hii tunamwachia Mungu? Kweli tumefikia huku?
Roma kulikoanzia ukatoliki walishindwa kumwachia Mungu? Huko Iran je, sisi tu waislam kuliko wao?
Badala ya kukumbatia mijadala ya kutafuta mawazo muafaka tumekuwa watu wa kutishana. Hofu imewajaa watu.
Waliopaswa kusikiliza, leo wamekuwa ndiyo vinara wa kutuongoza kwenye vita hii, na ndiyo hao waliotufikisha hapa tulipo leo: "tukiwa na Corona ndani ya nchi bila ya kuwa na uelekeo wa namna ya kuitokomeza".
Tuliaminishwa kwenye awamu zote za awali kuwa taifa halina dini. Wananchi ndiyo wanye dini zao na wengine hawana hata dini. Ilikuwa mwiko kuchanganya dini kwenye masuala ya kitaifa.
Kama ilivyo wazi, vinara wa hii vita, walipewa mawazo ya namna ya kuuzuia huu ugonjwa usiingie nchini. Hawakuzingatia ushauri huo. Wakati wakituaminisha kuwa ugonjwa hautaingia nchini, ugonjwa ukaingia. Hata ka samahani tu hawakutuomba, maisha yakaendelea.
Hata ugonjwa ulipoingia, wakapewa mawazo ya namna ya kuuzuia usisambae. Kwa mara nyingine hawakuzingatia mawazo hayo, huku wakituaminisha tena kuwa hautasambaa. Leo bila ya aibu wanatuambia kuwa ugonjwa unasambaa wala hawana mikakati wa kuuzuia usiendelee kusambaa zaidi.
Katika awamu hii kwa ujumla critical thinking imeuwawa kabisa. Hakuna mwenye ujasiri wa kuhoji. Sasa hivi tuko njia kuu, moja kwa moja kwenda kwenye maambukizi mabaya zaidi ya community kwa community.
Vinara wa mapambano wapo ofisini, na kama ilivyokuwa, hakuna samahani wala mpango wa wazi walionao wa kutuvusha kutokea hapa.
Ikumbukwe 1+1=2 bila ya kujali wasiojua wangapi wanasema 1+1=4. Hakuna demokrasia kwenye mambo nyeti kama haya wala kufanya majaribio siyo option.
Hatujachelewa kuhitaji taskforce nyingine yenye mawazo tofauti na kusikiliza kwenye vita hivi ambavyo changamoto zake zimeorodheshwa kuwa ni ngumu zaidi kuliko zozote tokea kwisha kwa vita vikuu vya pili vya dunia.
Ugonjwa huu ni hatari utatumaliza tusiposimama kulazimisha ufumbuzi kama tuliowapa dhamana hawataki kusikia au kuelewa.
Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums
Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums