#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Hii imekuingia!
Dogo Jifunze kutumia lugha nzuri unapowasiliana na wengine uwe unawafahamu au huwafahamu!
Hii ni JF unaruhusiwa kutumia lugha Kali ila sio kutusi wazazi wa MTU
Tu najua ninyi ni wasukuma mliochoka kuchunga kipindi hiki mnataka mrudi chuo mkarelax but sisi wazazi tunaojali wanetu tu najua bado risk mtoto kwenda chuo kwa hali iliyopo saivi

Najua hujui ila mtaka radhi my sweet mam kwa kumuita mpumbavu ilihali alishaacha upumbavu na anamiliki PhD yake
 
Hahaha eti "pombe sanitizer"...wee jamaa una mzaha
Sanitizer ni pombe sasa wewe unabisha nn?
Screenshot_20200410-060648_1586489357785.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali yetu kupambana na covid 19 hakika kama ingekuwa ni janga basi Watanzania tungekwisha tupukutike!

Shughuli zingine zote zinaendelea, shule na vyuo tu ndio vimesimama, sioni ulazima wa vyuo na shule kufungwa kwa kuepuka corona kama janga kwa nchi yetu.

Corona ipo kwaajili ya wazungu huko Ulaya, ni zamu yao sasa wacha iwanyooshe. Huku Africa tunapambana na majanga yetu ya maralia, njaa, ebola na mengine mengi. Wazungu wanataka kulazimisha janga lao liwe la dunia nzima. Haiwezekani.

PM Majaliwa tunaomba usiongeze muda wa kufunga shule na vyuo, watoto warudi kusoma kuanzia tarehe 17 Aprili.
Covid19 ni janga mkuu,nakumbka italy ilianza na visa vi2 tu vya corona lakini kwa sasa ni shida,tuna watu Tz wanakinga dhaifu wakiupata ni shida.
 
Awamu ya kikwete alianza kuwekeza kwenye TEHAMA hasa kwa walimu kwenda kujifunza kwa njia ya semina na kwa shule kuletewa Kompyuta nyingi zaidi,,lengo lilikuwa kila shule lifundishe SOMO la kompyuta kwa kila mwanafunzi lakini baada ya awamu hii ya kizalendo kuingia program zote za mafunzo kwa walimu zikafyekwa hakuna tena,ndoto za kuanzisha somo la kompyuta kwa wanafunzi ili wasome halisikiki tena ni kama limekufa kabisa.
Watanzania tujiulize kwa umakini zaidi maana dunia ya sasa ni ya kiteknolojia kwa kila kitu sasa kama bado tunaishi katika kipindi cha giza wakati wenzetu wanaishi kipindi cha mwanga tusitegemee mabadiliko ya haraka hata siku moja.
 
kandamatope, Mimi nakuunga mkono kwa 100%
Na anayebisha hatakuwa na akili sawasawa. Kwajinsi Watanzania tulivyo careless sisi tungekuwa nchi ya kwanza kwa Maambukizi na vifo.

Hakuna hatua zile kali ambazo serikali zimechukua ni hatua za kawaida tu. Hii nchi kuna watu wanaomba sana. Na hilo kwanzia Mw.

JPM anafahamu na katu hawezi pinga watu wasiende misikitini na Makanisani kutokana akifanya hivyo kwa siku tunaweza anguka 1000.
Mimi naweza sema ni Mungu anatulinda na kama huamini nahisi hata kama ni profesa jua ww ni Mbumbumbu wa mwisho.

Unaishi kutokana na mgongo wa wanaomuomba Mungu
 
Naomba huu uzi usiufute, baada ya mwezi kuanzia leo turejee hizi PUMBA zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna na haitotokea na kama ikitokea itakuwa kwako.
Nyie msioamini ndo mnaturetea uchuro. Hivi unataka kuniambia Tz ni smart kuliko Marekani, Italy , S.A basi tusiende mbali hapo kenya wametuzidi Mbali mno unajua kwanini wanakufa , wamehisi Corona ni Mkubwa kuliko Mungu wakafunga Makanisa na Misikiti watu wakashindwa kumuomba Mung hapo tu
 
Watanzania tusilizike na matamko ya wanasiasa kwamba serikali inatoa elimu bure,,tujiulize je!elimu bure hii inayohubiliwa na hawa viongozi inamuandaa mtoto kuwa nani?kwa maarifa yepi? Inamfanya awe mshindani duniani au Watchers ya kile kinachoendelea duniani? Watanzania wanasiasa sio rafiki zetu huuata kidogo hawapo kwa ajili ya shida zetu hebu angalia yanayoendelea toka awamu hii ilipoingia madarakani muda wote wanahangaikia uchaguzi ujao,akina polepole wanabema maburungutu ya fedha kwenda kulipa faini ya watuhumiwa wa mauaji yakubumba wakati wanafunzi hawana vitabu,hawana madawati,shule hazina maabara za kutosha,walimu wanadai madeni lukuki na wanajibiwa serikali haina fedha jifikirie mtoto wako masikini atafundishwa ipasavyo na mwalimu mwenye kinyongo? Rudi kwenye miundombinu ya shule kuna baadhi ya shule ni magofu hayatamaniki hata kidogo,madarasa yamechakaa haswa lakini watu wanabeba pesa kwenda kulipia faini za kijinga kabisa huku wakiacha mambo ya msingi yakijiendesha bila kusimamiwa ipasavyo. Tanzania nchi yangu
 
sidhani kuna mzazi atafurahia kurudisha shule wanae sasa, it is too soon!! at least tuone kwanza data zetu for a month more, na hasa hawa wagonjwa wanaotibiwa sasa wakipona itakuwa safi sana. turudi zero with extremely tight entry to Tanzania, mimi bado siamini sana kama tumedhibiti ipasavyo uingiaji wa waleta Coronavirus mipakani na Airport hadi nisikie JWTZ wamechukua kazi hiyo, but wenyewe wakiamua shule zifunguliwe tutawapeleka shingo upande!
 
Black kule wanatelekezwa hawapatiwi tiba sahihi ndiyo maana wanakufa wengi kuliko weupe!
Yaani hata manyeusi wenzao hawawatibu? Kuwa serious mkuu.Nina jamaa yangu pale Minneapolis Minnesota ni daktari na juzi juzi alikuwa ananiambia anataka aende The Empire state kuchukua zile dollsr 10,000 kwa wiki zilizotangazwa na meya wa Empire state
 
Watanzania tusilizike na matamko ya wanasiasa kwamba serikali inatoa elimu bure,,tujiulize je!elimu bure hii inayohubiliwa na hawa viongozi inamuandaa mtoto kuwa nani?kwa maarifa yepi? Inamfanya awe mshindani duniani au Watchers ya kile kinachoendelea duniani? Watanzania wanasiasa sio rafiki zetu huuata kidogo hawapo kwa ajili ya shida zetu hebu angalia yanayoendelea toka awamu hii ilipoingia madarakani muda wote wanahangaikia uchaguzi ujao,akina polepole wanabema maburungutu ya fedha kwenda kulipa faini ya watuhumiwa wa mauaji yakubumba wakati wanafunzi hawana vitabu,hawana madawati,shule hazina maabara za kutosha,walimu wanadai madeni lukuki na wanajibiwa serikali haina fedha jifikirie mtoto wako masikini atafundishwa ipasavyo na mwalimu mwenye kinyongo? Rudi kwenye miundombinu ya shule kuna baadhi ya shule ni magofu hayatamaniki hata kidogo,madarasa yamechakaa haswa lakini watu wanabeba pesa kwenda kulipia faini za kijinga kabisa huku wakiacha mambo ya msingi yakijiendesha bila kusimamiwa ipasavyo. Tanzania nchi yangu
Bado mfumo wa elimu THEORY ORIENTED hausaidii sana
 
sidhani kuna mzazi atafurahia kurudisha shule wanae sasa, it is too soon!! at least tuone kwanza data zetu for a month more, na hasa hawa wagonjwa wanaotibiwa sasa wakipona itakuwa safi sana. turudi zero with extremely tight entry to Tanzania, mimi bado siamini sana kama tumedhibiti ipasavyo uingiaji wa waleta Coronavirus mipakani na Airport hadi nisikie JWTZ wamechukua kazi hiyo, but wenyewe wakiamua shule zifunguliwe tutawapeleka shingo upande!
Watoe taarifa mapema ili wazazi waanze kuandaa na wengine kukopa nauli
 
Taifa kutofundisha wanafunzi, walimu, manesi, madaktari, maengineer, madereva, walinzi kwa Mwaka mzima Ni janga.nashauri shule Na vyuo vifunguliwe Mara moja.maeneo ya shule Na taasisi za elimu huduma za Afya ziboreshwe.nje ya hapo tunaenda kuangamiza taifa.
 
Jamaa umeandika mada bilayakufikiria kabsa
Kwanza swala la smartphone/computer si kila mwanafunzi wa chuo anayo na hivi vitu vinaenda sambamba unaweza kutumia smartphn peke yake ila kwa computer lazma uwe na router au simu kwaajili ya tathering hotspot so iko hivo
Pili hata hao wenye smartphone hali ni ngumu sasa kwa wanafunzi wengi unakuta hata mb ni shida mtu kuwa online kwa week ni mara moja pesa ya bando hamna sasa kwa hali hiyo mtu atasomaje online
Tatu mitandao yetu haiko reliable hasa vijijini huko hii ni changamoto
Mm ni mwanafunzi pia so nazungumzia nayoyaona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Wewe inaonekana unekulia mjini na kila kitu unakichukulia poa sana,kuna maeneo simu kushika hadi upande juu ya mti,harafu wewe unarahisisha tu,ajira yangu ya kwanza ilikuwa ni Lindi liwale ,amini kunasehemu ili uwasiliane na ndugu zako hadi mtu asubiri mwisho wa mwezi anapokuja kuchukua mshara,baada ya hapo hadi next month,na hadi naandika hivi bado maeneo hayo hayana network,sasa wewe unapojenerolaizi sijui unamaanisha nini

Pili kuna maeneo yana mtandao rakini hauruhusu INTERNET na wala hata kusoma E nu shida sasa hawa unawasaidiaje?

Tatu simu ,unapokuwa na simu wewe usidhani kila mwanachuo ana smartphone,kuna wafanya kazi wako ajirani for 20+ years hawazijui smartphone ,sasa hao unawasidiaje?

Sidhani kama kuna sehemu hakuna network, HALOTEL ndo mpango mzima hadi huko nanjilinji. Kuhusu simu, wananzo kama hana smart, sidhani kama kuna kijiji hakina mtu mwenye smart, watz ni wazalendo tunaazimana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi hata mitandao ya kufundishia tunayo?

hizo mb za kuunga unga za makampuni ya simu utaweza kuona lecture ya saa nzima?

Hatuna miundombinu ya kufanya hayo. Sisi mitandao yetu ni ya kutongozana na kuandika siasa na Clips ndogo ndogo za dakika tano.

kufundisha online kunahitaji internet ya nguvu. TTCL wameshindwa kazi ya kujenga mtandao wenye tija kwa wananchi wote.

Nashauri shule na vyuo viendelee kufungwa lakini kwa upande wa vyuo vikuu, wakufunzi waanze kufundisha kwa njia ya mtandao.

Hii inawezekana hasa kwa masuala ya theory, na practical zinaweza kufanyika siku wakirejea vyuoni. Tutumie mitandao kuwafundisha kwa vile wapo majumbani.

Kwa kuanzia, kuna wawakilishi wa wanafunzi (CRs) na viongozi wa wanafunzi vyuoni, hawa wanaweza kutumiwa notes na wakufunzi kwa mtindo wa SLIDES na VIDEOS na kusambaza kwa wenzao na hivyo muhula wa masomo kuendelea kama kawaida.

Kwa wale wenye mikopo (BOOM) wanaweza kupewa nusu kwa mfano sh.250,000/= ili zingine wapewe wakirudi vyuo baada ya kusaini.

Nimeshuhudia vyuoni baadhi ya wanafunzi hawahudhurii darasani ila wanachukua slides na kujisomea na wamekuwa wakifaulu hata kuzidi wale wanaohudhuria.

Vyuo vitakapofunguliwa, wakufunzi wanaweza ku-HIGHLIGHT kile walichofundisha na baadae kutoa TEST ONE.

Ili kiepusha msongamano, usumbufu katika vituo vya mabasi, na kukosa usafiri, siku shule zikifunguliwa, wapishane kwa wiki moja. Kwa mfano, wanaweza kutangulia wa shule za msingi na sekondari na baada ya wiki moja wafuatie wa vyuo vya kati na vyuo vikuu.

Wanafunzi wa vyuo vikuu wana viherehere hasa wakati wa uchaguzi, hivyo si vyema uchaguzi ukawakuta wakiwa vyuoni.
 
hivi hata mitandao ya kufundishia tunayo?

hizo mb za kuunga unga za makampuni ya simu utaweza kuona lecture ya saa nzima?

Hatuna miundombinu ya kufanya hayo. Sisi mitandao yetu ni ya kutongozana na kuandika siasa na Clips ndogo ndogo za dakika tano.

kufundisha online kunahitaji internet ya nguvu. TTCL wameshindwa kazi ya kujenga mtandao wenye tija kwa wananchi wote.
Sisi tunaweza siasa za kukomoana tu basi mengine sio kipaumbele chetu kabisa,,kuendesha nchi unahitaji mikakati thabiti sio longolongo za akina Polepole and the like
 
Back
Top Bottom