#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Ninaandika uzi huu kwa masikitiko kwani masikilizano ya kindugu yaliyokuwapo nchini mwetu tokea enzi za mwalimu kwa hakika kwa sasa yametatizika sana.

Katika awamu zote za awali, kuhoji, kujadili, kushauriana nk (kwa hoja) bila kujali itikadi, yalikuwa mambo yaliyokuwa yakipembejewa vilivyo. Busara za watu wetu zilikuwa karibu, kutumika kwa manufaa ya taifa.

Leo hii wako wapi wahadhiri na maprofesa nguli ambao mada zao moto moto ziliifanya jamii isisinzie? Yako wapi magazeti na majarida yaliyokuwa yamejipambanua kuwa siyo ya udaku? Wako wapi wanasiasa waliokuwa wanalichemsha bunge likachemka vilivyo na kuwaweka viongozi katika nafasi zao halisi kama watumishi wa wananchi?

Enzi hizo hoja ipi ya manufaa ya taifa ilikosa kudadavuliwa vilivyo tukawa na msimamo wetu wa wazi kama taifa kwa kushindana kwa hoja?

Leo hii tumekabiliwa na tatizo la Corona. Tujiulize (kwenye hili) mawazo ya manguli wetu yako wapi? Mawazo huru ya magazeti, radio, nk yetu yako wapi? Mawazo ya wanasiasa wetu yako wapi?

Leo hii tunamwachia Mungu? Kweli tumefikia huku?

Roma kulikoanzia ukatoliki walishindwa kumwachia Mungu? Huko Iran je, sisi tu waislam kuliko wao?

Badala ya kukumbatia mijadala ya kutafuta mawazo muafaka tumekuwa watu wa kutishana. Hofu imewajaa watu.

Waliopaswa kusikiliza, leo wamekuwa ndiyo vinara wa kutuongoza kwenye vita hii, na ndiyo hao waliotufikisha hapa tulipo leo: "tukiwa na Corona ndani ya nchi bila ya kuwa na uelekeo wa namna ya kuitokomeza".

Tuliaminishwa kwenye awamu zote za awali kuwa taifa halina dini. Wananchi ndiyo wanye dini zao na wengine hawana hata dini. Ilikuwa mwiko kuchanganya dini kwenye masuala ya kitaifa.

Kama ilivyo wazi, vinara wa hii vita, walipewa mawazo ya namna ya kuuzuia huu ugonjwa usiingie nchini. Hawakuzingatia ushauri huo. Wakati wakituaminisha kuwa ugonjwa hautaingia nchini, ugonjwa ukaingia. Hata ka samahani tu hawakutuomba, maisha yakaendelea.

Hata ugonjwa ulipoingia, wakapewa mawazo ya namna ya kuuzuia usisambae. Kwa mara nyingine hawakuzingatia mawazo hayo, huku wakituaminisha tena kuwa hautasambaa. Leo bila ya aibu wanatuambia kuwa ugonjwa unasambaa wala hawana mikakati wa kuuzuia usiendelee kusambaa zaidi.

Katika awamu hii kwa ujumla critical thinking imeuwawa kabisa. Hakuna mwenye ujasiri wa kuhoji. Sasa hivi tuko njia kuu, moja kwa moja kwenda kwenye maambukizi mabaya zaidi ya community kwa community.

Vinara wa mapambano wapo ofisini, na kama ilivyokuwa, hakuna samahani wala mpango wa wazi walionao wa kutuvusha kutokea hapa.

Ikumbukwe 1+1=2 bila ya kujali wasiojua wangapi wanasema 1+1=4. Hakuna demokrasia kwenye mambo nyeti kama haya wala kufanya majaribio siyo option.

Hatujachelewa kuhitaji taskforce nyingine yenye mawazo tofauti na kusikiliza kwenye vita hivi ambavyo changamoto zake zimeorodheshwa kuwa ni ngumu zaidi kuliko zozote tokea kwisha kwa vita vikuu vya pili vya dunia.

Ugonjwa huu ni hatari utatumaliza tusiposimama kulazimisha ufumbuzi kama tuliowapa dhamana hawataki kusikia au kuelewa.

Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums
 
Kama kufa watakufa wengi maana ndio nia yao..serikali inajua kabisa kupambana na huu ugonjwa hawawezi alafu wanashindwa kufunga mipaka gonjwa lisiingie nchini..wamefanya makusudi ili kuwauwa wananchi wake.naona sasa watakuwa na furaha malengo yao yanaenda kama walivyo panga..
 
Kabla ugonjwa COVID-19 haujaingia Tanzania Nilipata wasaa wa kuishauri Serikali ya Tanzania kuchukua hatua za mapema za kuzuia Safari za kutoka na kuingia Tanzania ili kuliepusha Taifa dhidi ya virusi vya CORONA Ingawa kwa masikitiko makubwa Sana ushauri huu haukuzingatiwa,

Haimaye Tanzania ilidumbukia katika mshike mshike wa kukimbizana na ugonjwa huu ambao mpaka Sasa umekita mizizi nchini hasa katika jiji la Dar es Salaam.

Kama Serikali itanshindwa Tena kuchukua hatua za haraka za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivi ndani na nje ya Dar Basi wiki chache zijazo tutashuhudia visa kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Ushauri wangu Tena kwa Serikali " Serikali isitishe safari za kutoka na kuingia katika jiji la Dar es Salaam Hadi hapo itakapojiridhisha kuwa maambukizi yamekwisha kabisa.

Kama Serikali haitafanya hivo basi ijiandae kupiga mchakamchaka wa kukimbizana na KORONA katika mikoa yote ya Tanzania.
Ni hayo tu wapendwa.
Ushauri wangu kwa serikali kabla ya korona kuingia nchini unaweza kuupata hapa chini.

Njia pekee ya kuzuia CORONA Tanzania Ni kuzuia watu kuingia na kutoka nchini - JamiiForums

CORONA: Kama Bunge letu lingekuwa na meno, ilikuwa Ni muda mwafaka wa kumtoa Rais madarakani - JamiiForums
 
Museven anawashauri watu wake Mazoezi wafanyie majumbani mwao, haina haja kwa wale wanaopenda Mazoezi kwenda kufanyia Mazoezi nje.

Kuonesha kuwa na yeye ni miongoni mwa wanaofanya Mazoezi nyumbani, imebidi aoneshe Mazoezi yake.

Hizo pushapu alizokuwa akipiga Museven!

Badala ya kunyanyua na kushusha kifua, yeye alikuwa ananyanyua na kushusha tumbo
Zile push-up nilicheka Sana Jana.... Sikumbuki kama alifikisha kumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliacha kazi nikaenda shule lakini mwanaume niliyenae ndiye aliyenifanya niende shule! Jana mwanamke wake kanitafuta kaniambia niachane nae kwani ye ndo yupo nae saiz jamani nina maumivu makali nilishaenda shule corona imenirudisha naiona likizo ya corona chungu kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Njoo PM tuyajenge jinsi ya ku canseliana na shule..
Pia tupeane moyo.
Mi ni mwanafunzi kama wewe tu..!!!

#YNWA

Wrote from Anfield..!!
 
Kama dawa ni kunawa na sabuni nasi nashauri pawe na mkakati wa kupiga maji ya povu mji mzima kila siku usiku watu wakirudi majumbani mwao ili kiwaua virus wa Korona wanabaki kwenye sehemu walizoshika waathirika.

Na wananchi wakitoka majumbaniwao asubuhi wanawe mikono na sabuni . Wakifika kwenye maeneo ya kazi zao pia wanawe.
Iwe ni kwa miji yote mpaka virusi visambaratike kabisa nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vifo vimefika 3 na waliopona kabisa 5 na wagonjwa wamefika 32

Namba inaongezeka kimchezo mchezo, Trump alichulia simple Sana covid 19. Saivi anacheza sebene

Tuendelee kizingatia ushauli wanaotoa wataalamu wa afya kupitia serikali yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kufa watakufa wengi maana ndio nia yao..serikali inajua kabisa kupambana na huu ugonjwa hawawezi alafu wanashindwa kufunga mipaka gonjwa lisiingie nchini..wamefanya makusudi ili kuwauwa wananchi wake.naona sasa watakuwa na furaha malengo yao yanaenda kama walivyo panga..

Ugonjwa ulikuja kwa ndege tokea nje ya Tanzania. Haukuja kwa bus wala Meli. Kwa nini ndege hazikuzuiliwa kuingia? Nani aliyehusika na kuachia business as usual airports.

Huyu ndiye alikuwa wa kuanza naye kuliko hata ya bwana ninja.

Yote walielezwa well before hand.
 
Tumesha chelewa....Corona ilikuwwpo Tanzania kabla ya December 2019,na imeshasambaa nchi nzima, sema tu vipimo ni vichache...vingekiwepo kila hospital ya wilaya/mkoa ungeshangazwa na Takwimu...!

Tuendelee kuchukua tahadhari tu.....na principle ya Natural Selection ifanye kazi, wakaufa atakufa,wa kupona atapona na wakubaki atabaki. Serikali yetu sio tu inauwezo mdogo wa kifedha, na hata akili hawana.
Kabla ugonjwa COVID-19 haujaingia Tanzania Nilipata wasaa wa kuishauri Serikali ya Tanzania kuchukua hatua za mapema za kuzuia Safari za kutoka na kuingia Tanzania ili kuliepusha Taifa dhidi ya virusi vya CORONA Ingawa kwa masikitiko makubwa Sana ushauri huu haukuzingatiwa,

Haimaye Tanzania ilidumbukia katika mshike mshike wa kukimbizana na ugonjwa huu ambao mpaka Sasa umekita mizizi nchini hasa katika jiji la Dar es Salaam.

Kama Serikali itanshindwa Tena kuchukua hatua za haraka za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivi ndani na nje ya Dar Basi wiki chache zijazo tutashuhudia visa kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Ushauri wangu Tena kwa Serikali " Serikali isitishe safari za kutoka na kuingia katika jiji la Dar es Salaam Hadi hapo itakapojiridhisha kuwa maambukizi yamekwisha kabisa.

Kama Serikali haitafanya hivo basi ijiandae kupiga mchakamchaka wa kukimbizana na KORONA katika mikoa yote ya Tanzania.
Ni hayo tu wapendwa.
Ushauri wangu kwa serikali kabla ya korona kuingia nchini unaweza kuupata hapa chini.

Njia pekee ya kuzuia CORONA Tanzania Ni kuzuia watu kuingia na kutoka nchini - JamiiForums

CORONA: Kama Bunge letu lingekuwa na meno, ilikuwa Ni muda mwafaka wa kumtoa Rais madarakani - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bongo kila mtu ni mjuaji

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuwepo wajuaji haikuwa taabu. Kuuwa critical thinking na kuwafagilia wajinga imewaengua werevu.

1+1=4 ni sahihi ati kwa sababu wajuaji hao wameshinda kwa kwa kura.

Kwa case hii wa kulaumiwa ni establishment inayowaendekeza wajinga (wasiojua) hao ambao aghalabu hawajui kuwa hawajui.
 
Tumesha chelewa....Corona ilikuwwpo Tanzania kabla ya December 2019,na imeshasambaa nchi nzima, sema tu vipimo ni vichache...vingekiwepo kila hospital ya wilaya/mkoa ungeshangazwa na Takwimu...!

Tuendelee kuchukua tahadhari tu.....na principle ya Natural Selection ifanye kazi, wakaufa atakufa,wa kupona atapona na wakubaki atabaki. Serikali yetu sio tu inauwezo mdogo wa kifedha, na hata akili hawana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa mkuu
 
Zimeundwa kamati, nasikia 3, za kupambana na gonjwa hili hata hazijulikani.

Nina wasiwasi kama kuna wajumbe kutoka sekta binafsi. Kimsingi hili suala kama tunavyoona watu na makampuni yanavyojitolea kuchangia mapambano haya, ningetamani kuona serikali ikiratibu mapambano ila kamati ziundwe na serikali na wajumbe kutoka ndani na nje ya serikali.

Napendekeza askari toka jwtz awekwe kuwa kiongozi wa taskforce kupambana na ugonjwa huu.

Hii ni vita, kubwa kuliko yoyote tuliyowahi kupigana.

Hii si vita ya kuongozwa na kina Ummy wanaoangalia zaidi matumbo yao
 
Back
Top Bottom