masikinitajiri
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 275
- 131
Nipo Dar es Salaam, eneo la Karakata karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius K. Nyerere. Sakata la Corona linavyosemwa mitandaoni na kwenye media lipo tofauti sana na uhalisia wa maisha yetu huku. Mass media zinaongeza presha zaid kwa wananchi kuliko ilivyo kawaida ktk uhalisia, Corona inasemwa tu midomon na tunasikia sikia mambo mengi kuhusu corona kila siku lakin hata hivyo shughuli zinaendelea kama kawaida, na misikitin tunakusanyika. Waislamu tuna tabia ya kusalimiana kwa kushikana mikono au hata kukumbatiana, na wakat mwingine misikiti inajaa sana kias cha kubanana, hivyo hatukai mbali mbali na hili linaendelea kama kawaida wala hatuna khofu ya corona zaid ya kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu. Ukitazama watu wanavyoishi huku ni kama corona haipo, maisha yanakwenda bila khofu. Watoto wanatoka pia kuhudhuria ibada na magengeni tunawatuma. Suala la biashara huhusisha zaid mabadilishano ya fedha mkono kwa mkono, hili linafanyika vizuri bila khofu yoyote na wala hakuna anayevaa hizo mask isipokuwa hunawa kwa.sabuni na maji safi tu. Ikiwa haya yanawezekana, tusemeje kuhusu shule ambazo ni mikusanyiko ile ile kama ilivyo ktk ibada, masokoni, magengeni, bungeni, kwenye PS watoto wanakocheza games n.k? Kuna mambo mengine yameshakadiriwa, alilopanga Mwenyezi Mungu likufikie hata uende wapi au ujifungie ndani miaka 10 na uwe unapatiwa huduma zote bure bado litakufika tu. Kikubwa watu wachukue tahadhari zisizoleta athari kubwa ya kuendesha maisha yao wakat huo huo wakimtegemea Mungu kama mlinzi wao. Corona si chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Maamuzi kama hayo wazungu wanajuta na wanakufa zaid ktk majumba yao. Jiulize Corona inafikaje ktk nyumba zao? Kila kitu na Qadar. Serikali isichukue maamuz ya kukopi kutoka kwa wazungu pasina kujua athari zake kubwa. Siku ikipitisha kauli et watu wakae ktk majumba yao na asitoke yeyote na kila shughuli ifungwe basi tutarajie vifo vingi zaid kutokea kuliko ilivyo sasa, najua wazi vifo hivyo itasingiziwa Corona pejee ndo imepelekea na si maamuzi yao mabovu.
Tuwe makini sana ndugu zangu, kila.mtu anazungumza lake pasina kuleta fikra sahihi mbele kuna nini au kutatokea nini.
Acheni kuwaabudu wazungu kwa fikra zao, kila kitu wakifanya au wakisema nyie mnashika tu yan hata hamfikirii, na media zinatia preaha zaid, huu ni msiba mkubwa sana. Afrika bado tunatawaliwa kifikra na si kiuchumi pekee kama wengi waonavyo.
Tuwe makini sana ndugu zangu, kila.mtu anazungumza lake pasina kuleta fikra sahihi mbele kuna nini au kutatokea nini.
Acheni kuwaabudu wazungu kwa fikra zao, kila kitu wakifanya au wakisema nyie mnashika tu yan hata hamfikirii, na media zinatia preaha zaid, huu ni msiba mkubwa sana. Afrika bado tunatawaliwa kifikra na si kiuchumi pekee kama wengi waonavyo.