Mkuu kiongozi wa Dar aletwe Mwanajeshi,.Dar iwe chini ya amri za kijeshi hadi Corona itakapoyeyuka
Huu uswahiba unatupeleka pabaya sana
kama taifa, vinginevyo tumekwisha Amen.
Kama ni order tumpime akili mtoa order
 
Mbinu rahisi na zenye gharama nafuu katika kuthibiti kusambaa kwa COVID-19 tumeshindwa kuzitumia ili kujikinga na janga hili. Kifuatacho ni machozi, njaa, usumbufu wa lod down , msukosuko kwenye mfumo wa huduma za afaya pamoja na vifo ndio gharama tunayokwenda kuilipa Kutokana na kuruhusu community spreading of this deadly disease.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukosa exposure kunaligharimu taifa
 
Kama tunavyofahamu kuwa Ulimwengu mzima umetikiswa hivi sasa na ugonjwa huu hatari wa corona unaosababisha vifo vingi sana

Ugonjwa huu umekuja kwa kustukiza na kwa bahati mbaya sana, ugonjwa huu hadi hivi sasa haujapata tiba wala chanjo

Nchi mbalimbali zinachukua hatua kali ya namna ya kukabiliana nao

Nchi za jirani zetu kama vile Kenya, Rwanda, Malawi na hata Afrika Kusini, viongozi wake wamejitolea kukatwa mishahara yao, ili ziende kusaidia kuthibiti ugonjwa huu wa corona

Tumejionea wenyewe namna Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto walivyokubali kukatwa mishahara yao kwa asilimia 20 ili ziende wizara ya afya, zikasaidie kupunguza kasi ya maambukizi ya corona

Tumejionea vile vile nchi ya Rwanda ikichukua hatua zinazofanana na hizo, kwa Rais wake Paul Kagame na baraza lake lote la mawaziri wakikubali kukatwa mishahara yao yote ya mwezi huu wa April iende kusaidia janga hili la corona

Tumeshuhudia vile vile nchi ya Malawi, ambayo nayo viongozi wake wa juu nchini humo wamechukua hatua kama hizo, ambapo Rais wake Peter Mutharika na Baraza lake la mawaziri, wamekubali kukatwa asilimia 10 ili ziende kusaidia kutokomeza ugonjwa huu wa corona

Vile vile nchini Afrika Kusini nako Rais Cyril Ramaphosa na Baraza lake la Mawaziri nao wamekubali kukatwa theluthi moja toka kwenye mishahara yao ili ziende kusaidia janga hili la corona

Swali ninalojiuliza ni kwa vipi hapa kwetu ambapo Rais wetu Magufuli, ambaye amekuwa akijiita kuwa ni Rais wa wanyonge, ni kwanini basi hajachukua hatua walizochukua majirani zake hao ya kukatwa mshahara wake ili ziende kusaidia wananchi wake wanyonge ambao wanateseka kwa maumivu ya ugonjwa huu hatari wa corona?

Swali langu ni hilo, ambalo nategemea kujibiwa kwa hoja na wala siyo kwa mihemuko kutoka kwa wale wapambe wa "bukusaba" wa Lumumba
 
Ngoja waamke bado wamelala

Sent using Jamii Forums mobile app
jembe afrika
Nawasubiri tuu waamke ili wanijibie swali langu hilo, ni kwanini kiongozi wetu anayejiita wa wanyonge, asikubali kukatwa mshahara wake ili kwenda kuwasaidia wananchi wake wanyonge, wanaoteseka na ugonjwa huu wa corona?

Tufahamu pia kuwa wizara ya afya haijapangiwa bajeti kwa janga hili la korona

Kwa hiyo ni vyema ikafahamika kuwa ugonjwa huu umekuja kwa dharula, kwa hiyo ni lazima vile vile zichukuliwe hatua za dharula ya namna ya kuukabili
 

Majuto ni mjukuu. Yote waliambiwa wakapuuzia.
 
Awamu hii ya tano kweli unaamini wakikatwa mishahara, hizo pesa zitatumika kupambana na Covid-19? Mkuu unaniangusha sana!
 
wamechukua bajeti ya mwenge walitangaza
 
Mkuu kumbuka tu ya kwamba hakukuwa na nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma kipindi cha takribani miaka minne toka Mheshimiwa aingie madarakani. Labda wanafanya "general assumptions of paying in kind instead of cash". Kwa kuwa ktk awamu hii lolote lile linawezekana, inatarajia tu nani amezungumza nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mimi nasikia nchi hiyo ya maziwa na asali ni donor kantri, sasa mishahara wakatwe ya nini?


It is never to late to begin. Start now
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…