Kama ni order tumpime akili mtoa orderMkuu kiongozi wa Dar aletwe Mwanajeshi,.Dar iwe chini ya amri za kijeshi hadi Corona itakapoyeyuka
Huu uswahiba unatupeleka pabaya sana
kama taifa, vinginevyo tumekwisha Amen.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama ni order tumpime akili mtoa orderMkuu kiongozi wa Dar aletwe Mwanajeshi,.Dar iwe chini ya amri za kijeshi hadi Corona itakapoyeyuka
Huu uswahiba unatupeleka pabaya sana
kama taifa, vinginevyo tumekwisha Amen.
na hata akili hawana
Kukosa exposure kunaligharimu taifaNinaandika uzi huu kwa masikitiko kwani masikilizano ya kindugu yaliyokuwapo nchini mwetu tokea enzi za mwalimu kwa hakika kwa sasa yametatizika sana.
Katika awamu zote za awali, kuhoji, kujadili, kushauriana nk (kwa hoja) bila kujali itikadi, yalikuwa mambo yaliyokuwa yakipembejewa vilivyo. Busara za watu wetu zilikuwa karibu, kutumika kwa manufaa ya taifa.
Leo hii wako wapi wahadhiri na maprofesa nguli ambao mada zao moto moto ziliifanya jamii isisinzie? Yako wapi magazeti na majarida yaliyokuwa yamejipambanua kuwa siyo ya udaku? Wako wapi wanasiasa waliokuwa wanalichemsha bunge likachemka vilivyo na kuwaweka viongozi katika nafasi zao halisi kama watumishi wa wananchi?
Enzi hizo hoja ipi ya manufaa ya taifa ilikosa kudadavuliwa vilivyo tukawa na msimamo wetu wa wazi kama taifa kwa kushindana kwa hoja?
Leo hii tumekabiliwa na tatizo la Corona. Tujiulize (kwenye hili) mawazo ya manguli wetu yako wapi? Mawazo huru ya magazeti, radio, nk yetu yako wapi? Mawazo ya wanasiasa wetu yako wapi?
Leo hii tunamwachia Mungu? Kweli tumefikia huku?
Roma kulikoanzia ukatoliki walishindwa kumwachia Mungu? Huko Iran je, sisi tu waislam kuliko wao?
Badala ya kukumbatia mijadala ya kutafuta mawazo muafaka tumekuwa watu wa kutishana. Hofu imewajaa watu.
Waliopaswa kusikiliza, leo wamekuwa ndiyo vinara wa kutuongoza kwenye vita hii, na ndiyo hao waliotufikisha hapa tulipo leo: "tukiwa na Corona ndani ya nchi bila ya kuwa na uelekeo wa namna ya kuitokomeza".
Tuliaminishwa kwenye awamu zote za awali kuwa taifa halina dini. Wananchi ndiyo wanye dini zao na wengine hawana hata dini. Ilikuwa mwiko kuchanganya dini kwenye masuala ya kitaifa.
Kama ilivyo wazi, vinara wa hii vita, walipewa mawazo ya namna ya kuuzuia huu ugonjwa usiingie nchini. Hawakuzingatia ushauri huo. Wakati wakituaminisha kuwa ugonjwa hautaingia nchini, ugonjwa ukaingia. Hata ka samahani tu hawakutuomba, maisha yakaendelea.
Hata ugonjwa ulipoingia, wakapewa mawazo ya namna ya kuuzuia usisambae. Kwa mara nyingine hawakuzingatia mawazo hayo, huku wakituaminisha tena kuwa hautasambaa. Leo bila ya aibu wanatuambia kuwa ugonjwa unasambaa wala hawana mikakati wa kuuzuia usiendelee kusambaa zaidi.
Katika awamu hii kwa ujumla critical thinking imeuwawa kabisa. Hakuna mwenye ujasiri wa kuhoji. Sasa hivi tuko njia kuu, moja kwa moja kwenda kwenye maambukizi mabaya zaidi ya community kwa community.
Vinara wa mapambano wapo ofisini, na kama ilivyokuwa, hakuna samahani wala mpango wa wazi walionao wa kutuvusha kutokea hapa.
Ikumbukwe 1+1=2 bila ya kujali wasiojua wangapi wanasema 1+1=4. Hakuna demokrasia kwenye mambo nyeti kama haya wala kufanya majaribio siyo option.
Hatujachelewa kuhitaji taskforce nyingine yenye mawazo tofauti na kusikiliza kwenye vita hivi ambavyo changamoto zake zimeorodheshwa kuwa ni ngumu zaidi kuliko zozote tokea kwisha kwa vita vikuu vya pili vya dunia.
Ugonjwa huu ni hatari utatumaliza tusiposimama kulazimisha ufumbuzi kama tuliowapa dhamana hawataki kusikia au kuelewa.
Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums
Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums
Hadi Rais mjuaji ?????
Kama ni hivyo mbona sijawahi sikia vifo 600 kwa siku?
jembe afrika
Thubutu.Zile push-up nilicheka Sana Jana.... Sikumbuki kama alifikisha kumi
Sent using Jamii Forums mobile app
Mbinu rahisi na zenye gharama nafuu katika kuthibiti kusambaa kwa COVID-19 tumeshindwa kuzitumia ili kujikinga na janga hili. Kifuatacho ni machozi, njaa, usumbufu wa lod down , msukosuko kwenye mfumo wa huduma za afaya pamoja na vifo ndio gharama tunayokwenda kuilipa Kutokana na kuruhusu community spreading of this deadly disease.
Sent using Jamii Forums mobile app
wamechukua bajeti ya mwenge walitangazajembe afrika
Nawasubiri tuu waamke ili wanijibie swali langu hilo, ni kwanini kiongozi wetu anayejiita wa wanyonge, asikubali kukatwa mshahara wake ili kwenda kuwasaidia wananchi wake wanyonge, wanaoteseka na ugonjwa huu wa corona?
Tufahamu pia kuwa wizara ya afya haijapangiwa bajeti kwa janga hili la korona
Kwa hiyo ni vyema ikafahamika kuwa ugonjwa huu umekuja kwa dharula, kwa hiyo ni lazima vile vile zichukuliwe hatua za dharula ya namna ya kuukabili
Waongezee na ile bajeti ya kuwanunua wapinzani isaidie kuondosha coronawamechukua bajeti ya mwenge walitangaza