#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Namba 6 kwa wauza soko apo umezingua

Wanaojaza soko sio wauzaji, ni sisi tunaoenda kuemea

Wauza soko wote kila mtu ana meza yake na social distance imezingatiwa

Labda sisi tunaoenda kufanya manunuzi ndo tuwekewe ratiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namba 6 kwa wauza soko apo umezingua

Wanaojaza soko sio wauzaji, ni sisi tunaoenda kuemea

Wauza soko wote kila mtu ana meza yake na social distance imezingatiwa

Labda sisi tunaoenda kufanya manunuzi ndo tuwekewe ratiba

Sent using Jamii Forums mobile app

Yote ni mawazo mazuri kuwa kuwe Na mtu mmoja kwa kila muuza soko mmoja .. that what’s I mean
 
Hizo.mask za kutowa bure 40M @$2 kwa kila mask kwa rate ya sasa hela ipo?
 
mkuu unayajua majeshi ya kiafrika...............ustarabu zero.....elimu chini so tegemea uonevu......
 
Kuweka Dar yote kwenye Karantini ni zoezi Gumu Na expensive ingawa linawezekana.. kupanga ni kuchagua .. lakini bado tunaweza kuweka Karantini maeneo kwa maeneo badala ya Dar yote .. pia kufanya mapendekezo niliyatoa ili kupunguza maambukizi
Sawa Mkuu nakubaliana na wewe kuwa litakuwa jambo gumu kidogo kuiweka Dar yote kizuizini lakini bora kinga kuliko tiba.

Dar ni jiji ambalo lina watu zaidi ya 2000 kutoka katika kila mkoa na mimi nina imani kuwa kuna watu wengi ndani ya Dar ambao wamepata maambukizi lakini bado hawajaonesha dalili.

Sasa hatari zaidi itapatikana pale ambapo mtu atakapoamua kuondoka Dar kwenda mkoani kwa lengo La kukimbia maambukizi wakati tayari ameshapata maambukizi pasi na kufahamu unafikiri hali itakuaje?

Ndio maana nikapendekeza Dar iwekwe kizuizini kabla ugonjwa haujasambaa zaidi mikoani hali itakuwa mbaya sana hasa ukizingatia ubora wa huduma zetu za afya.
 
Mawazo yako mengi mazuri, ila hili LA kutumia jeshi siungi mkono.
mi katika comments zangu mada nyingi za Corona niliomba all points of entry kote nchini wawepo wanajeshi ili kukamata wageni wanaoingia kwa kuhonga au kwa njia za panya na pia wanajeshi wawepo vituo vya karantini kuzuia wanaotoroka karantini na kutuletea mauti mitaani ila nadhani wahusika na wasomi kama wewe mna mbinu bora zaidi kuzuia au kupunguza community transmissions!

Hii ni vita na watu wanakufa hakuna utani na kubembelezana kwenye kifo. tukiwaomba jeshi kutusaidia mapambano ya Corona watatutendea haki! Italy , India na kila nchi ni majeshi tu yanahusika sana.

Pia serikali iombe msaada nje kununua madawa yanayohusika kama Paracetamol or ibuprofen na chloroquine
 
Meko's effect jeshi jeshi jeshi!!! mkuu akil za meko zimekuingia kiasi cha kuamin jeshi linaweza kuondoa corona
 
Mapendekezo ambayo Mr President anatakiwa kufanya .

1. Kwa kuwa ugonjwa umeshafika kwenye community stage transimission , Ningeshauri ile mikoa ambayo case chache zimepatikana.. kungeagizwa test kits za kutosha ili kubaini ukubwa wa Tatizo, Pili kila anayepatikana positive apelekwe kwenye vituo vya karantini.

2. Kwa kuwa ventilator zime prove low rates healing 50% compare to Hydroxychlotoquine + Zinc , pia ni very expensive .. ningeshauri Tanzania itowe order kwa ndugu zetu wa India Watutengenezee hydroxy Ch.. Zinc mseto mara moja na tutume ndege kwenda kuchukua ili zitumike kwa waliotest positive ..

3. Kiwanda cheti cha pharmaceutical kama kinaweza tengeneza mseto huo basi ni wakati mwafaka wa kufanya hivyo.

4. Kwa wagonjwa wenye mild symptoms na wenye ku prove self karantini waruhusiwe kijitibu Nyumbani.

5. Mabaa na Shughuli zote zamikusanyiko isiyo ya lazima zipigwe marufuku.

6 . Wauza masoko wapunguzwe au wauze kwa zamu.. Kuwepo Na mita 2 toka muuza soko mmmoja mpaka mwingine .

7. Serikali ingize barakoa za kutosha Na kutumia wanajeshi kugawa kwenye maeneo mbalimbali na baada ya week mbili iwe ni marufuku kutembea bila barakoa.

6. Mabasi ya mikoani.. yaagizwe kubeba mtu mmoja kwa siti ya watu wawili.. kupunguza kukaribiana kwa Abiria .

7 . Dalaldala kubeba abiria nusu ya idadi ili abiria wakae kwa nafasi Na zoezi hili lisimamiwe Na jeshi.

8 . Kusiwe Na total Lockdown , watu warujusiwe kufanya kazi , pale maeneo ya kazi yatakapokuwa ni hatarishi, basi eneo hilo tu ndio lifungwe.

9: Stendi za mabasi zisimamiwe Na Jeshi Na wale wapiga debe waondolewe wote kupunguza msongamano usio Na lazima .

10. Hospital maalaum za Korona zisifanye kazi y huduma zingine za kawaida ili kupunguza maambukizi.

11. Ibada ziendelee lakini waumini waingie kwa zamu na kuwepo kwa umbali wa mita 2 toka muhimini mmoja Na mwingine Na Usafi wa kutosha ufanyike kila baada ya Ibada moja kuisha kabla ya kuingia Nyingine.

12. Wanajeshi wapelekwe mtaani ili kuangalia maeneo ya kazi ambayo yataonekana kuwa hatarishi basi yafungwe .

13. Shughuli za kilimo na mifuko ziendelee kama kawaida Na wakulima waelimishwe namna ya kujikinga Na kuweka mita 2 toka mkulima mmoja mpaka mwingine.

14 . Wenye viwanda pia wao observe mita 2 toka mtu mpaka mtu Na uvaaji wa mask.

....
Badala ya kutumia wanajeshi serikali itumie ma bwana afya wa ngazi zote. Kuanzia ngazi ya mtaa, kijiji, kitongoj, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi taifa kulingana na uhitaji.
 
Naunga mkono, kila point, labda kwa kujazia.

1. Dar,iwe kizuizini ila huduma muhimu za kuingia na kutoka kama magari ya dawa na vyakula visizuiwe.

2.Kwenye kuvaa barakoa, iwe hivi, hairuhusiwi kwenda sehemu hatarishi bila ya barakoa, kama masokoni,hospital au kuingia katikati ya jiji.

3.Serikali itumie wataalam wa afya kuangalia kama tunauwezo wa kutengeneza barakoa hata zenye efficay ya asilimia fulani, kutumia vitambaa sponges, bila kusahau viwanda vyetu vya nguo pia kuangalia uwezekano wa ku produce vitambaa barakoa.


Alexander The Great
 
Nawasalimu wanaJF, wote na nafikiri mnaendelea vizuri pia poleni kwa janga hili la CORONA linaloendelea kuitikisa duniani kote nafikiri hiki ni kipindi cha mpito tutakivuka

Napenda niende moja kwa moja katika mada husika hapo juu ninayokusudia kuitoa kuhusu maoni au ushauri kwa nchi yangu Tanzania juu ya kupambana na hili janga la Corona ambalo limekuwa tatizo duniani kote

Napenda kuishauri serikali ya Tanzania kuwapa LOCKDOWN watanzania wote kuwe hakuna ruhusa ya kutoka nje kwa siku 14 na watanzania wote tuchukuliwe vipimo ili kutambua kiurahisi nani ana huu ugonjwa

Kwa maana huu utaratibu wa kutafuta wagonjwa hadi wajitokeze au kuonekana na dalili hizi ndiyo wafanyiwe vipimo sioni kama huu utaratibu utasaidia kukabiliana na hili janga

Kwa maana hiyo na kwa jinsi watanzania hatuna utaratibu kama ambao wazungu wanao wa kwenda kuangalia afya zao kila wiki au kila mwezi maana sisi kuviona vituo vya afya hadi hali iwe mbaya kiasi kwamba mtu ushindwe kutembea ndiyo uende kituo cha Afya

Je ni watanzania wangapi wana hizo dalili za COVID-19 na wanachukulia kama homa ya kawaida na kutumia tu dawa za kawaida majumbani kwao?

Naweza kusema mfano wa maisha yetu watanzania tunayoishi ni kuwa mtu ukijisikia kichwa kuuma ni unatumia tu dawa ya kutuliza maumivu kisha tunaendelea na shughuli kama kawaida sasa chukulia mtu kapata maambukizi haya na kuoneyesha baadhi ya dalili kwa maana huwezi kupata dalili zote kwa pamoja je kwa system yetu ya kupima afya mpaka uzidiwe utaenda kweli hospital ingali bado unajiona una nguvu

Napenda kuwasilisha ushauri wangu huu kwa maana mimi ni mtanzania na pia naipenda nchi yangu TANZANIA
 
SAWA MKUU TUMEKUSIKIA
ILA KUMBUKA CORONA INAUA ILA NJAA INAUA ZAIDI, TUKIWEKEWA LOCK DOWN KWA HALI ZETU SISI WATANZANIA UNATEGEMEA TUTAJIMUDU KWELI KWENYE SUALA LA CHAKULA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Embu toa mapendekezo matatu tuu katika hiyo orodha yako. By the way hivi Katibu mkuu wa Wizara ya Afya ni Daktari wa binadamu kwa taaluma yake? nikipata jibu nitauliza swali gumu
Nadhani ni daktari
 
Namba 6 kwa wauza soko apo umezingua

Wanaojaza soko sio wauzaji, ni sisi tunaoenda kuemea

Wauza soko wote kila mtu ana meza yake na social distance imezingatiwa

Labda sisi tunaoenda kufanya manunuzi ndo tuwekewe ratiba

Sent using Jamii Forums mobile app
Hajazingua kasema kweli, labda kwa baadhi ya masoko ndio ipo unavyosema. mengi unakuta meza moja kuna wauzaji hata watatu, na haina ukubwa wa hata mita 5.
 
Nadhani ni daktari
Hana mbinu za kukabiliana na majanga? Ningepewa fursa ya kushauri, ningeshauri Mh. Mbatia aongezwe kwenye kamati ya taifa ya kukabiliana na CORONA labda fani inaweza kutusaidia kipindi hiki kama taifa
 
Hana mbinu za kukabiliana na majanga? Ningepewa fursa ya kushauri, ningeshauri Mh. Mbatia aongezwe kwenye kamati ya taifa ya kukabiliana na CORONA labda fani inaweza kutusaidia kipindi hiki kama taifa
Mbatia ni daktar wa binadamu??
 
Back
Top Bottom