#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
I wish tungekua na well functioning election commission.... Hii ndio ingekua mwisho wa utawala wa hii familia
 
Kwenye hili la korona mashule yamefungwa ,vyuo na makolegi kitambo sana kila duka ama biashara na maofisi hatua stahik za kujikinga sinachukuliwa, hususani kwenye vyombo vya usafiri na mipakani bado hali ni mbaya pamoja na yote hayo swali ni je tatizo ni uzembe wa wabongo au serikali ya wabongo
Ni tatizo la uzembe wa Serikali ya Wabongo na wabongo wenyewe kwa kukubali kuongozwa na wabongo wasiokuwa na uwezo. Viongozi hao wanatumia wingi wa umma ulio kama wao kuficha udhaifu wao katika kila nyanza kwa mafanikio makubwa. Wanazungumza sana bila vitendo kuwavutia watu lakini mara nyingi hakuna cha maana wanachosema na mbinu hiyo ikishindikana wanaamua kukaa kimya bila kuonekana wakiacha wananchi wakiulizana kulikoni. Wakati huu mgumu wa hili gonjwa, Viongozi wetu wa Serikali na wa Chama Tawala wako wapi, wanafanya nini na wanasema nini? Ndivo walivyo!
 
Tuliambiwa watalii wasipokuja nchi haina pesa bajeti haitakwenda ndio maana ni Tanzania pekee haijafunga mipaka. Mpka pale safari zilipojifunga zenyewe na sio nchi kufunga inamaana tulipiga pesa nyingi kwani tulikuwa wenyewe sokoni na watalii duniani.

Kwa kutofunga mipaka ndio tulipoingiza wagonjwa nchini huku tukitarajia kupata kodi na tozo mbalimbali kuendesha nchi bila shaka tumezikusanya za kutosha.

Inakuwaje tumeukaribisha ugonjwa na kupata fedha za kutosha lakini hatuna vifaa vya kukabuliana na ugonjwa huo mpka tusubiri misaada?

Nchi hii inasubiri ihudumiwe na raia wake badala ya serikali kufanya wajibu wake kama wakusanya kodi.

Je nikweli sisi ni matajiri na tuna pesaya kujiendesha kwa miezi 6 bila kufanya kazi? Kwanini hata mwezi mmoja umetushinda kama nchi?

Ni kweli kutofunga mipaka imeisaidia nchi au imeuwa nchi hasa nguvu kazi ya taifa?
Kutofunga mipaka imekusaidia wewe, Mimi na wengine kuwa na nguvu na uwezo wa kuingia mitandaoni vinginevyo Hali ingekuwa mbaya zaidi kiuchumi,,,,,lakini kumbuka nchi moja ikifunga mpaka na ina maana hata ile ambayo haijatangaza mufunga nayo automatically mpaka wake unakuwa umefungwa,,,,wewe mwenzetu ulitaka serikali ifanye ili uridhike nafsi yako???
 
Summary tafadhali amesemaje?
Sina embii za kupakua
Amesema ametumia tangawizi na limao, limao amekata katikati kipande kimoja kakamua kingine kakiweka hivyohivyo, tangawizi kaichemsha pia katumia vitunguu swaumu, ushauri wake ukipata korona kaa ndani usitoke kusambaza kwa wengine
 
Ahsante mkuu nguvu
 
Tuliambiwa watalii wasipokuja nchi haina pesa bajeti haitakwenda ndio maana ni Tanzania pekee haijafunga mipaka. Mpka pale safari zilipojifunga zenyewe na sio nchi kufunga inamaana tulipiga pesa nyingi kwani tulikuwa wenyewe sokoni na watalii duniani.

Kwa kutofunga mipaka ndio tulipoingiza wagonjwa nchini huku tukitarajia kupata kodi na tozo mbalimbali kuendesha nchi bila shaka tumezikusanya za kutosha.

Inakuwaje tumeukaribisha ugonjwa na kupata fedha za kutosha lakini hatuna vifaa vya kukabuliana na ugonjwa huo mpka tusubiri misaada?

Nchi hii inasubiri ihudumiwe na raia wake badala ya serikali kufanya wajibu wake kama wakusanya kodi.

Je nikweli sisi ni matajiri na tuna pesaya kujiendesha kwa miezi 6 bila kufanya kazi? Kwanini hata mwezi mmoja umetushinda kama nchi?

Ni kweli kutofunga mipaka imeisaidia nchi au imeuwa nchi hasa nguvu kazi ya taifa?
Kigwangala anapendekeza herd immunity, yaani tuache ugonjwa uenee, watu wafe, watakaobaki ndio hao wanatosha! Na ndivyo kinachofanyika sasa. na kwa ugonjwa kama huu, hata 90% ya watu wanaweza kufa kabla ya kufikia hiyo herd immunity. He is very stupid indeed!
 
Na lenyewe litakufa kama ndivyo anataka
 
Kutokana na serikali kuruhusu kuendelea kwa shughuli za wananchi na kutoa maelekezo ya kujikinga ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, huku mitaani hasa kwenye vijiwe vya bodaboda nimeshuhudia vijana wanapiga story tu huku wakiwa wamejazana kwenye benchi bila kuvaa barakoa.

Pia nimeshuhudia kuongezeka kwa abiria wanaopanda daladala bila kuwa na barakoa. Kwa maana nyingine wabongo wameshaona janga limeanza kupoa, wanaanza kuchukulia kirahisi.

Ni katika mazingira haya ndo tutajikuta tunawasha moto ambao tunaweza kushindwa kuuzima huko mbeleni.
 
Kuna msemo mmoja unasema hapa duniani kila kitu ni siasa lakini sio Katika maisha(uhai)naona serikali inafanya mzaha katika maisha ya watu haijali uhai wa watanzania kwa kujali fedha .huu ugonjwa tungeweza kuudhibiti mapema tuu kwa kufunga mipaka kipindi ugonjwa umepamba Moto maelfu ya watalii wanamiminika.

Huko Uganda kila siku madreva wa malori wanagundulika kuwa na virusi .hii inaonesha Hali halisi ya kuwa ugonjwa u meshasambaa .nadhani munashuhudia wakubwa wengi wanafariki kwa Sana kwanni vifo vya wakubwa vimekuwa vingi Sasa hujiulizi?

Hi inatokana na serikali kufanya siasa na maisha ya watu hii inaweza kuleta athari mbaya Kama ugonjwa utaendelea kwa muda mrefu Sasa hv pale Wuhan hakuna kisa Cha ugonjwa .Wamefanya Kazi kubwa mpaka kufikia pale .sio kuleta siasa zisizo na maana .Kila kitu ni siasa lakini sio katika maisha ya watu. Stay home , stay safe.
 
Back
Top Bottom