#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Waje tu la ukifika unap
elekwa kempinski halafu ujilipie kwa siku 14
 
Najiuliza tu waungwana hawa watanzania walioko nje ya nchi kipindi hiki cha mapambano ya Corona je wabakie huko huko?

Rais wa Uganda mh Museveni amefanya maamuzi magumu ya kuwazuia waganda walio nje ya nchi kurejea nchini hadi pale ugonjwa wa Corona utakapodhibitiwa.

Je, uamuzi wa mh Yoweri unafaa kuigwa?

Maendeleo hayana vyama!
Waje tu Mungu yuko nasi.
 
Haturudi mpaka country bumpkin na Mkolomije waondoke kwanza.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Najiuliza tu waungwana hawa watanzania walioko nje ya nchi kipindi hiki cha mapambano ya Corona je wabakie huko huko?

Rais wa Uganda mh Museveni amefanya maamuzi magumu ya kuwazuia waganda walio nje ya nchi kurejea nchini hadi pale ugonjwa wa Corona utakapodhibitiwa.

Je, uamuzi wa mh Yoweri unafaa kuigwa?

Maendeleo hayana vyama!
Serikali ya JMT imeshatoa tamko kuwa wakija hapa Tz watawekwa karantini kwa muda wa siku 14 kwa gharama zao. Sasa mnataka tamko gani tena? Wenyewe wajiongeze tu wabaki huko kama ilivyokuwa China. Maana unaweza kuja hapa Tz alafu una dola 500 ukashindwa hata kujihudumia hizo siku kumi na nne.
 
Ni ngumu kuzuia raia wako kurejea kwenye nchi yao. Hata leo nimekuwa KIA kuna watalii kibao wanarudi makwao.
Trump jana aliwapa deadline Wamarekani wote walioko nje ya nchi warudi nyumbani haraka iwezekanavyo. Wasipofanya hivyo kabla ya deadline hiyo basi waendelee kukaa nje ya Marekani indefinitely kwa kuwa hawataruhusiwa kuingia Marekani. Hii ni kutokana na kufunga mipaka ya nchi yake ili kudhibiti Corona. Kwa kuwa Rais wa Marekani amesema hivyo, tunaipokea tu taarifa hiyo. Rais Magufuli akisema hivyo inakuwa nongwa.
 
Najiuliza tu waungwana hawa watanzania walioko nje ya nchi kipindi hiki cha mapambano ya Corona je wabakie huko huko?
Rais wa Uganda mh Museveni amefanya maamuzi magumu ya kuwazuia waganda walio nje ya nchi kurejea nchini hadi pale ugonjwa wa Corona utakapodhibitiwa.
Je, uamuzi wa mh Yoweri unafaa kuigwa?
Maendeleo hayana vyama!
Muse7 katishwa katishika, sisi kwetu ni tusitishane, Watanzania wote walioko ughaibuni karibuni sana nyumbani, njooni tulijenge taifa.

Provided wakitua nchini, watakaa 14 days compulsory quarantine.

Tanzania ni hapa kazi tuu, hatutishiki.
P
 
Trump jana aliwapa deadline Wamarekani wote walioko nje ya nchi warudi nyumbani haraka iwezekanavyo. Wasipofanya hivyo kabla ya deadline hiyo basi waendelee kukaa nje ya Marekani indefinitely kwa kuwa hawataruhusiwa kuingia Marekani. Hii ni kutokana na kufunga mipaka ya nchi yake ili kudhibiti Corona. Kwa kuwa Rais wa Marekani amesema hivyo, tunaipokea tu taarifa hiyo. Rais Magufuli akisema hivyo inakuwa nongwa.
Yes nimeona safari nyingi zimekuwa cancelled watu wanarudi kwao. Tatizo pia huku wanaacha janga kampuni nyingi za utalii zinafanya retrenchment (redundancy) hali ni tete.
 
Hili nalo neno hawa wasingeruhusiwa kurudi wapigwe kalantini huko huko walikokuwa tusingekuwa na mgonjwa.
 
Kifupi hizi ndizo options ambazo mtu wa kawaida anakumbana nazo. Fikiria ndugu zangu ambao wanaishi kwa suluhu (draw) umepata hela ya kula, kesho utafute yingine ili ule, na hela inaishia kwenye kula tu. Hata ukiumwa inabidi ujikaze au utumie mitishamba maana hela ya dawa mtihani.

Ndugu zangu wabeba zege, bodaboda, wauza visheti kwa watoto wa shule. Nazungumzia hawa waliokuwa nje ya mfumo rasmi wa ajira. Na ndio waliowengi nchini, wanaotafuta kipato kwa jasho jingi sana, kuosha magari, pikipiki, nk.

Hawa kwa gonjwa hili wanabaki na option mbili tu, kubaki ndani ili wafe njaa, au waende nje wakakutane na corona. Tumejipangaje?

Zitto alitoa mawazo kuwa serikali itoe stimulus package kwa wafanyabiashara, lakini wako wengi wanaoathirika, wasanii, washereheshaji, project planners nk, je nao walipwe? Na wakulima tuache wafe?

Na kila mtu inabidi alipwe, atalipwaje kwa serikali ambayo bajeti yake inategemea mikopo, misaada na grants, tena ukizingatia pato la ndani litapungua kwa kupungua kwa shughuli za kuiingizia serikali hela, je tutakopa hela ili tuwape watu wetu!

Patamu hapo, anyway, Pick up your poison, chagua kufa njaa au kufa kwa corona

Signed

Oedipus
 
Hii issue inafikirisha sana, kuna jamaa mmoja alileta wazo la kufanya total lockdown

yaani tukae ndani bila kutoka

nafkiri hakuwaza ulichoandika hapa

NB:Mungu atatuponya tu, maana anajua hatuwezi kukabiliana na gonjwa hili.
 
Corona imepata umaarufu sio tu kwa vile haina tiba wala kinga bali kwa njia ambavyo inasambaa inahatarisha maisha na usalama wa wakuu na matajiri.

Matajiri na wakuu wa dunia wamekuwa makini katika kupambana na Corona katika mwamko na gharama ambazo kama wangefanya hivyo kwa umasikini ungekuwa umeishafutika au kupungua ambao licha ya kuwa na tiba na kinga lakini umasikini ndio unaoongoza kuua watu wengi kuliko kitu chochote.

Kwa mfano: Ukimwi hauui mtu bali unadhoofisha mwili na kuuliwa na magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu, malaria, pneumonia, n.k.

Hivyo hivyo UMASIKINI hauui bali usababisha madhara yenye mauti nyemelezi kama ajali kutokana na msongo wa mawazo, vitendeakazi vibovu na dhaifu, magonjwa, ugomvi, visasi, njaaa, n.k.

Maisha hayana huruma kabisa kila mtu anajitengenezea ngome kwa kutumia nafasi aliyonayo katika jamii kwa ubinafsi zaidi kuliko tunavyodhania! Hili ni somo la kujifunza kutoka kwa Corona kumtaka kila mtu apambane na hali yake.
 
Jamani kila kitu mnalalamika mbona mambo yote yana ufumbuzi?.umaskini jitahidi ujikwamue kutoka huko kwa kufanya kazi, Ukimwi achana na ngono zembe kama ww ni kijana,lakini labda kama ulizaliwa nao hapo utasikitika.
Naongelea attention na uzito uliochukulowa na viongozi wakuu wa dunia kwa Corona! Tatizo sio kwa vile unaua! Kama ni kuua yako magonjwa mengi yanaua kuliko Corona!

Tatizo ni njia ambayo unasambaa na kuhatarisha maisha yao! Kiongozi wa Ujerumani Angel Michael yuko kwenye quarantine! Ona sasa! Wataachaje kupambana nao? Lakini Ebora? No one gives a shit about it! Life is struggle for existence and survival for the fittest!
 
Wakati wewe unalala usingizi. Nchi tajiri zije zikupambanie uondokane na umasikini.
 
Back
Top Bottom