#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Jamani kila kitu mnalalamika mbona mambo yote yana ufumbuzi?.umaskini jitahidi ujikwamue kutoka huko kwa kufanya kazi, Ukimwi achana na ngono zembe kama ww ni kijana,lakini labda kama ulizaliwa nao hapo utasikitika.
Sio wote wenye ukimwi waliupata kwa ngono zembe..wengine waliletewa,,wengine walibakwa. Wengine waliupata kazini, wengine waliupata kwenye ajali. Malejendari wachache sana waunaupata kwa kwa ngono zembe.
 
Siwezi kufa kwa njaa nikiogopa kutoka kwenda kufanya kazi nipate hera ya kununua chakula ni mara 100 nife kwa Corona niliyoipata nikiwa kweny mihangaiko ya kutafuta ugali wa family yangu, kufa kwa njaa eti unaogopa Corona ni ufara wa kiwango cha rami
 
Nipo ndani nimejifungia na mtoto ambae jana tumelalia uji na tumeamkia uji, mchana pia uji usiku pia uji. Mungu tusaidie. Hata maji ya kununua ndoo sh mia nashindwa kununua.
Njaa ikiuma mda mrefu hadi kichwa kinauma.
 
Naongelea attention na uzito uliochukulowa na viongozi wakuu wa dunia kwa Corona! Tatizo sio kwa vile unaua! Kama ni kuua yako magonjwa mengi yanaua kuliko Corona! Tatizo ni njia ambayo unasambaa na kuhatarisha maisha yao! Kiongozi wa Ujerumani Angel Michael yuko kwenye quarantine! Ona sasa! Wataachaje kupambana nao? Lakini Ebora? No one gives a shit about it! Life is struggle for existence and survival for the fittest!
Sawa kabisa. Basi haya ya umaskini na ebola ni maswala yetu huku wacha wapambane huko na yao maanaa imewashika pabaya. Tuombe Mungu atuepushe ipite kwetu kama mafua ya kawaida
 
Yaani Usemacho Ni Sawa na:

Wakati Maywether anapambana ulingoni anapigwa anatoka manundu wewe uko busy kufuatilia mademu.

Akipata pesa Unataka UPEWE MSAADA na unaona kabisa ni HAKI YAKO
 
hii issue inafikirisha sana, kuna jamaa mmoja alileta wazo la kufanya total lockdown

yaani tukae ndani bila kutoka

nafkiri hakuwaza ulichoandika hapa

NB:Mungu atatuponya tu, maana anajua hatuwezi kukabiliana na gonjwa hili.
Alikurupuka kabisa mkuu .
 
Mawazo haya ni sawa na kusema kwamba, "nikiokoa godoro naacha nyumba iteketee."
 
Nipo ndani nimejifungia na mtoto ambae jana tumelalia uji na tumeamkia uji, mchana pia uji usiku pia uji. Mungu tusaidie. Hata maji ya kununua ndoo sh mia nashindwa kununua.
Njaa ikiuma mda mrefu hadi kichwa kinauma.
Aisee pole sana, hii hali wala sio nyepesi kama wengi wanvyodhania
Pole sana miminimama
 
~ serikali haina uwezo wa kusaidia kwa chochote zaidi ya kukupa matumaini kwa mbali ,bora ufe kwa corona kuliko kufa kwa njaa.

Kule Wuhan serikali ilivyopiga marufuku watu kutoka ndani ilikuwa inawasambazia chakula RAIA wake mitaani...sasa sisi kupiga marufuku safari za kuingia na kutoka imekuwa ngumu, kutokana na kuhofia uchumi kuanguka.
 
Nipo ndani nimejifungia na mtoto ambae jana tumelalia uji na tumeamkia uji, mchana pia uji usiku pia uji. Mungu tusaidie. Hata maji ya kununua ndoo sh mia nashindwa kununua.
Njaa ikiuma mda mrefu hadi kichwa kinauma.
Pole sana, kwanini sasa si utoke ukatafute kazi au biashara.. [emoji24][emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani kila kitu mnalalamika mbona mambo yote yana ufumbuzi?.umaskini jitahidi ujikwamue kutoka huko kwa kufanya kazi, Ukimwi achana na ngono zembe kama wewe ni kijana, lakini labda kama ulizaliwa nao hapo utasikitika.
Mbona wafanya ngono maarufu tubaowajua hawana ukimwi ,na makapuku wengi tunaowajua wameukwaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Direct kwenye mada...

Tunazidi kushuhudia Dunia kwa sasa iko na hali mbaya sana kutokana na virusi vya corona.

Maumivu ni makubwa sana tangu ugonjwa huu uanze kwa mara ya kwanza nchini china hadi kusambaa kwake kwa kasi mataifa mengine ya jiran na hatimae dunian kote.

Athar zimezid kuongezeka na inawezekana zikazidi kuongezeka zaidi endapo baadhi ya nchi zitashindwa kuchukua hatua madhubuti kuzuia usambaaji zaidi wa virusi hivi.

Kwa sasa dunia imetikisika,na kila nchi imeweka juhudi zake zote katika kupambana na ugonjwa huu..

Hapa ukichunguza utagundua Dunia inazungumza lugha mmoja pekee kwa sasa
Yaan lugha ya "Corona" au kwa covic-19.

Si ugaidi tena,si nuclear wala maralia,au ukimwi au Vita..
Yaan dunia yote inaongea juu ya corona!!

Je, ni nini kitatokea baada ya ugonjwa wa corona kuisha?


1.Kufanyika kwa uchunguzi na kufunguliwa kesi dhidi ya Taifa la china,na endapo ushahidi utaonyesha china inahusika,(licha ya kuwa ni kwel hadi sasa ushahid unaonyesha virus vya corona vilitengenezwa na china katika jimbo lake la wuhan),basi vikwazo vikali vya kimataifa vitaanzishwa na umoja wa mataifa kwa kushirikiana na mataifa makubwa dhidi ya China.

2.kutokana na kwamba,Dunia itakuwa imeanguka kiuchumi baada ya ugonjwa huu,basi dunia itaweka juhudi nyingi kunusuru uchumi wa dunia.

3.Asilimia kubwa ya watu watapoteza ajira,na mataifa maskini yatazidi kudidimia kiuchumi kwa kupoteza kiwango kikubwa cha mapato kutokana na ugonjwa huu.


Mengine nawaachia wadau muongezee

Nawasilisha
 
Urusi itakuwa "super power" ya dunia. Italia itajiondoa umoja wa Ulaya.
 
So china ilijitengenezea janga lake..??
Hivi hata wewe ukigundua kwamba serikali yako imetengeneza ugonjwa ili kuwaangamiza Nani ataiamini..?
Sidhani Kama china inaweza jiharibu yenyewe kihivyo kwa hii hoja mwe!
 
Back
Top Bottom