Habari wadau,
Nimeona nianzishe hii mada niliyoipa jina la ushauri wangu kwa Serikali kuhusu ugonjwa wa CORONA au COVID 19( Corona Viruse Diseases of 2019)
Lengo la kuanzisha mada hii kama kichwa cha mada kinavyoeleza ni kuishauri serikali kuhusu ugonjwa huu katika maeneo yote, ikiwemo eneo la Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa, Teknolojia n.k
Kuna ushauri umetolewa na watu wengi kuhusu ugonjwa huu ila haujatolewa katika mpangilio mzuri sababu mtu katoa ushauri kwenye mada juu ya mada hivyo inakuwa vigumu kuupata huo ushauri au mawazo hayo vizuri.
Nimeanzisha hii mada, lakini lengo ni kushirikiana na watu wote wa Jamii Forum na Tanzania kwa ujumla, Taasisi zote, Jumuia za serikali na zisizo za serikali, Vyama vya siasa n.k ili kuweza kutoa ushauri na mawazo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweza kuchukua hatua ili kuokoa Taifa la Tanzania, Afrika na Dunia kwa kwa ujumla, pia kuokoa kizazi chetu kutoka katika huu ugonjwa.
Ningependa niweke angalizo kwamba katika kutoa ushauri au mawazo tuache itikadi za kisiasa, kidini, kikabila n.k bali tutoe ushauri na mawazo kama watoto wa baba na mama mmoja ambae ni Tanzania.
Lengo lingine la hii mada pia ni kuachana na mawazo ya kutegemea wazungu na Asia 100% kama ndio suruhisho la huu ugonjwa, ninajua kwamba Ulaya, Amerika, Asia n.k wameendelea kwenye tiba za kisasa ila tusiwategemee sana kama ndio suruhisho la huu ugonjwa sababu pia hatujui agenda zao za siri kuhusu huu ugonjwa.
Naomba kama moderators wataiacha hii mada iwe inajitegemea ili tuweze kuwa na sehemu maalumu ya kutoa ushauri au mawazo yetu kwa Serikali.
Nitaanza na mimi kwa kutoa ushauri ufuatao
1. Nimeona nchi nyingi zimefunga mipaka na nyingine kwa Afrika kama South Africa, Rwanda n.k wamechukua hatua ya lockdown kwa maana ya kusimamisha shughuli nyingi za wananchi na kuwasisitiza wananchi kutotoka ndani ya nyumba zao, hivyo sababu nasi jana tumepata kifo kimoja cha kwanza kilichotokana na huu ugonjwa
Hivyo nitashauri utaratibu huu wa lockdown sababu inawezekana na sisi hali ikiwa mbaya itabidi serikali isimamishe wananchi kufanya shughuli yeyote.
Kwa hali za kiuchumi za watanzania wengi ni ngumu sana kufanya total lockdown, sababu watakufa au watapata shida kubwa na vitu vingine kama njaa, magonjwa mengi n.k
Hivyo nitashauri Serikali ifanye half lockdown, inawezekana half lock down ni msemo mpya ila katika half lockdown nitashauri serikali ifanye mambo yafuatayo
a. (1)Kupunguza muda wa kazi kwa taasisi zote binafsi na serikali.
Kupunguza masaa ya kazi Kutoka masaa yaliyopo sasa hadi nne, lengo la kupunguza muda wa kazi ni kuwawezesha wafanyakazi kuchelewa kuingia ofisini na kuwawezesha wafanyakazi Kutoka ofisini mapema mfano. Kuingia ofisini saa nne na kutoka saa nane.
Dhumuni la kupunguza muda wa kazi ni kupunguza msongamano wa watu kwenye usafiri sababu hiyo ndio sehemu kubwa ambayo ni rahisi watu wengi kuambukizana huu ugonjwa haraka na ikikumbukwa serikali imetoa tamko kwa daladala kupakia level siti hivyo tabu ya usafiri ni kubwa sana, hivyo kitendo cha kupunguza muda wa kazi kitawawezesha wafanyakazi kusafiri bila pressure za Kuwai usafiri asubuhi au kuchelewa usafiri jioni.
(2) Njia ya pili kuhusu wafanyakazi, serikali inaweza kuanzisha utaratibu wa kufanya kazi kwa shift kama ilivyo hospital, polisi, bandari, TRA kwa baadhi ya department n.k
Lengo ni lile lile kupunguza pressure za usafiri asubuhi na jioni sababu eneo la usafiri ndio eneo ambalo rahisi sana watu kuambukizana
Izingatiwe kuwa tatizo la usafiri limekua kubwa sana asubuhi na jioni kwa karibu mikoa yote Tanzania , serikali imeanzisha utaratibu wa kuziambia daladala ziwe na level siti, ila utekelezaji wake ni hafifu hasa nyakati za jioni na usiku watu wakiwa wengi na traffic police hawapo barabarani.
2. (a)Serikali iweke akiba ya kutosha ya chakula kitakachotosha nchi kwa Miezi sita hadi mwaka sababu, nchi karibu zote duniani zimeathirika na huu ugonjwa hivyo ni ngumu sana kwa nchi moja kutoa msaada kwa nchi nyingine ikiwa kila nchi ina tatizo la njaa
(b) Ikiwezekana serikali ifunge mipaka kuuza mazao ya chakula nje ya nchi, ili kuwezesha nchi kuwa na akiba ya kutosha ya chakula, sababu tunaona jirani zetu Kenya wameshaanza kuchukua hiyo hatua hivyo ni vizuri nasi tukaiga ilo jambo zuri.
3. (a)Serikali kuanzisha utaratibu wa lazima kwa watu wote kuvaa mask ( Barakoa) kwenye mikusanyiko ya watu kama sokoni, kwenye vyombo vya usafiri vya jumuia n.k lengo ni kupunguza maambukizi ya huu ugonjwa kwa njia ya hewa, sababu tumeona hili kosa hata kwa Mheshimiwa Raisi mwenyewe anasalimiana na watu kwa kugonganisha miguu lakini ajavaa mask (barakoa) na wakati huu ugonjwa unaambukiza hata kwa njia ya hewa.
(b) Pia serikali kushauri wananchi kuvaa nguo zinazoficha sehemu kubwa ya mwili hasa suruali na mashati marefu kwa wanaume na wanawake au nguo za aina yeyote zinazoficha sehemu kubwa ya mwili
Karibuni kwa ushauri na mawazo mbalimbali
Sent using
Jamii Forums mobile app