#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Bongo movies inaingiaje hapo, ww vijana wa Dar hauwajui???kuna jamaa kaenda kumkopa kinyozi amnyoe hajamlipa wiki ya pili ,nimewakuta wanadaiana lijamaa linamjibu kinyozi nikipata nitakupa hela yako au nikiokota hela lazima nikulipe usiwaze mwanangu.Kinyozi kakasirika kwa majibu ya jamaa bado kidogo wapigane shekhe wangu nkawaamulizia.
Naiona harufu ya bongo movie kwenye uzi huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaolilia lockdown ni watoto wa kishua na watu wenye uwezo sababu wao wanajijali maisha yao kana kwamba wanajua kabisa kua wao hata nchi ikifungwa miez minne, watakula na kuvaa bila shida yoyote na ni haki yao kutaka nchi ifungwe ili kujikinga na maambukizi.

Lakini vipi sisi maskini? Ndio tunajua Corona ni hatari na inaua but Corona mpaka mtu kufa unachukua mpaka mwezi, vipi njaa inayoua ndani ya wiki tu? Pia athari za njaa ni nyingi ikiwemo magonjwa ya utapiamlo na kiribatumbo.

Vipi Watanzania wenzetu mmetufikiria na sisi maskini? Ndio, tunajua ugonjwa ni hatari but njaa bado ni hatari zaidi ya Corona na kila siku njaa inaua, sio kama Corona imeanza mwaka jana tu hapa.

Serekali itabidi ichague iweke lockdown maskini wafe kwa njaa watu wenye uwezo wapone au iache shughuli ziendelee na atakayetaka kulinda maisha yake ajiweke lockdown yeye na family yake maana huwezi kusema uweke lockdown nchi kama yetu. Watu watakufa sana. Mfano wale wamama na wadada wa Buguruni wanaofanya shughuli zao kila siku, machinga wa Kariakoo ambao mitaji yao ni shilling elfu 10, yaani anauza mifuko faida ni buku jero mpaka buku mbili kwa siku ambayo ndio hela yake ya kula.

Kwa Tanzania hii hatuwezi kupambana na Corona kwa lockdown tukashinda ila tutakufa vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Kwa Tanzania hii hatuwez kupambana na Corona kwa Lock down tukashinda Ila tutakufa vibaya

Maneno huumba
 
Katika Kitabu cha Kumbukumbu ya Maisha ya Rais Mstaafu wa awamu ya 3, Mh. Benjamin William Mkapa moja ya mambo anayoshauri katika kuhitimisha ni ushauri wa nchi yetu kuwa na sera ya kudhibiti ongezeko la watu, ongezeko la watu katika taifa letu haliendani na uwezo wetu wa uzalishaji na rasilimali zetu jambo linalopelekea kundi kubwa la watu kukosa huduma muhimu, na ongezeko la ukosefu wa ajira likizidi kushamili. Hofu imetanda juu ya hatima ya maisha ya Watanzania endapo serikali itafikia uamuzi wa kupitisha zuio la kutotoka nje (Lockdown) Watanzania wataweza kumudu maisha?

Ni jambo gumu ambalo sio rahisi kuweza kutekelezeka kiurahisi hasa ukizingatia Watanzania wengi ni wale wanaofanya shughuli za kukidhi mahitaji ya msingi kama Chakula na Mavazi, Tumeona nchi nyingi za Ulaya na America zikipisha sera hii na imesaidia kupunguza kasi ya maambukizi kwa kiasi kikubwa, Uwezo wa serikali za hizi nchi ni Mkubwa lakini hata uwezo wa Mwananchi mmoja mmoja sio wa kulinganisha na nchi nyingi za Afrika.

Lakini moja ya sababu inayopelekea wenzetu kufanikiwa katika hili ni idadi ya raia kuwa himilivu kwa Rasilimali na uwezo wa Serikali, Mataifa kama Uingereza, Uhispania, Italia, Ufaranza yameongeza idadi ya watu kwa wastani wa watu milion 6 hadi milioni 10 kutokea mwaka 1980 hadi 2020, Tanzania tumeongeza wastani wa idadi ya watu Milioni 40 tokea Mwaka 1980 ambapo makadirio ya Watanzania yalikuwa ni Milioni 20, huku makadirio ya Mwaka huu yakikadiriwa kufikia idadi ya watu milioni 60.

Kuwa na idadi Kubwa ya watu sio jambo baya lakini kama taifa lazima tujitosheleze kwa majibu kuwa idadi ya watu wanao ongezeka ni himilivu kwa rasilimali zetu na uwezo wa serikali kuhudumia, Kwa zaidi ya Miaka 20 nchi yetu imekuwa na kampeni ya ujenzi wa shule na kutengeneza madawati kama ushauri wa Rais Mstaafu hautafanyiwa kazi inawezekana taifa letu likatumia miaka 50 kujenga shule, hospitali, madawati kwasababu watu wanazaliwa kila kukicha kwa kasi inayotisha sana.

Tumeona nchin Rwanda Serikali ikipita nyumba kwa nyumba kutoa misaada ya chakula, Rwanda sio nchi tajiri wala haina rasilimali nyingi kutushinda lakini nina imani idadi ya Raia wa Rwanda ni himilivu kwa Serikali jambo lililoifanya serikali kuwa na uwezo wa kutoa msaada kwa kila Mwananchi. Naamini viongozi wetu wanatamani kufanya makubwa kwaajili ya wananchi wao, na pengine wana nia njema lakini wakiwaza jinsi gani watamfikia kila Mwananchi wanajikuta uwezo huo hatuna kabisa.

Hatuna budi kukaa chini na kuunda sera madhubuti, Sera ya kudhibiti ongezeko la watu Nchini china ilianza miaka ya 1960 ambapo china ilianza kuchukua hatua madhubuti baada ya kuona idadi ya watu waliokuwa nao ilikuwa ni kubwa kuliko uwezo wa taifa lao, Leo tunashuhudia Makampuni yakija nchi za Afrika kuchukua fursa mbalimbali kwasababu hawa njia nyengine ya kuendelea kustawi bila kutoka nje na kutafuta fursa ambazo nchini kwao ni adimu kuzipata.

Ushauri wa Rais Mkapa sio wa kupuuza hata kidogo, ni ushauri unaotakiwa kufanyiwa kazi bila ya mzaha na kwa wakati ili hali isije kuwa mbaya zaidi, ninaamini viongozi wetu ni wasikivu watatumia nafasi hii kujifunza na kuweka mikakati itakayoliokoa Taifa letu kwa siku za usoni
 
Rwanda hawagawi chakula kila nyumba Ni kaya masikini tu ndio wanapewa Kama huku wanavyopewa kila mwezi kaya masikini na tassaf pili population ya Rwanda Ni 12.5 milion hizo kaya masikini zitakuwa ngapi? Sisi tuko milioni 60 tutaweza kugawa hicho chakula Cha bure tunacho kililia?
 
major mwendwa,
Hakika kiongozi aliyepo sasa hivi hataelewa kwanini watu wasizaliane kwani yeye anasema ardhi ipo, chakula kipo halafu mnazaa watoto wawili tu?

Hawezi kuona rasilimali haziongezeki na kwamba hata hao watu waliopo sasa hivi ni nzigo tayari na wanaishi chini ya kiwango cha ubinadamu.

Umaskini wa watu waliopo ameshindwa kuuondoa halafu anasema fyatueni...kweli viongozi wetu ni very irresponsible and ignorant.
 
Rwanda hawagawi chakula kila nyumba Ni kaya masikini tu ndio wanapewa Kama huku wanavyopewa kila mwezi kaya masikini na tassaf pili population ya Rwanda Ni 12.5 milion hizo kaya masikini zitakuwa ngapi? Sisi tuko milioni 60 tutaweza kugawa hicho chakula Cha bure tunacho kililia?
Chukua iyo population ya Rwanda gawa kwa annual national income. Alafu chukua annual national income ya tz gawa kwa idadi ya raia wake. Ukipata jibu lazima swali la kwanza utakalojiuliza ni "Tanzania tunafail wapi?"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rwanda hawagawi chakula kila nyumba Ni kaya masikini tu ndio wanapewa Kama huku wanavyopewa kila mwezi kaya masikini na tassaf pili population ya Rwanda Ni 12.5 milion hizo kaya masikini zitakuwa ngapi? Sisi tuko milioni 60 tutaweza kugawa hicho chakula Cha bure tunacho kililia?

Kwani sisi kama donor kantri tutashindwaje kugawa chakula kwa wananchi wetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani sisi kama donor kantri tutashindwaje kugawa chakula kwa wananchi wetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa donor kantri sio hoja zipo nchi ulaya ni donor kantri na hazijagawa chakula Cha bure lakini chadema wakizidi kupigania hiki chakula kinaweza kutolewa [emoji16][emoji1][emoji2960]
 
Kuwa donor kantri sio hoja zipo nchi ulaya ni donor kantri na hazijagawa chakula Cha bure lakini chadema wakizidi kupigania hiki chakula kinaweza kutolewa [emoji16][emoji1][emoji2960]
Matajiri leo tunalalamika 80% ya wananchi wetu ni maskini,hahah Ccm bana.
Screenshot_2019-12-21-09-59-03-1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wadau,
Nimeona nianzishe hii mada niliyoipa jina la ushauri wangu kwa Serikali kuhusu ugonjwa wa CORONA au COVID 19( Corona Viruse Diseases of 2019)

Lengo la kuanzisha mada hii kama kichwa cha mada kinavyoeleza ni kuishauri serikali kuhusu ugonjwa huu katika maeneo yote, ikiwemo eneo la Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa, Teknolojia n.k

Kuna ushauri umetolewa na watu wengi kuhusu ugonjwa huu ila haujatolewa katika mpangilio mzuri sababu mtu katoa ushauri kwenye mada juu ya mada hivyo inakuwa vigumu kuupata huo ushauri au mawazo hayo vizuri.

Nimeanzisha hii mada, lakini lengo ni kushirikiana na watu wote wa Jamii Forum na Tanzania kwa ujumla, Taasisi zote, Jumuia za serikali na zisizo za serikali, Vyama vya siasa n.k ili kuweza kutoa ushauri na mawazo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweza kuchukua hatua ili kuokoa Taifa la Tanzania, Afrika na Dunia kwa kwa ujumla, pia kuokoa kizazi chetu kutoka katika huu ugonjwa.

Ningependa niweke angalizo kwamba katika kutoa ushauri au mawazo tuache itikadi za kisiasa, kidini, kikabila n.k bali tutoe ushauri na mawazo kama watoto wa baba na mama mmoja ambae ni Tanzania.

Lengo lingine la hii mada pia ni kuachana na mawazo ya kutegemea wazungu na Asia 100% kama ndio suruhisho la huu ugonjwa, ninajua kwamba Ulaya, Amerika, Asia n.k wameendelea kwenye tiba za kisasa ila tusiwategemee sana kama ndio suruhisho la huu ugonjwa sababu pia hatujui agenda zao za siri kuhusu huu ugonjwa.

Naomba kama moderators wataiacha hii mada iwe inajitegemea ili tuweze kuwa na sehemu maalumu ya kutoa ushauri au mawazo yetu kwa Serikali.

Nitaanza na mimi kwa kutoa ushauri ufuatao

1. Nimeona nchi nyingi zimefunga mipaka na nyingine kwa Afrika kama South Africa, Rwanda n.k wamechukua hatua ya lockdown kwa maana ya kusimamisha shughuli nyingi za wananchi na kuwasisitiza wananchi kutotoka ndani ya nyumba zao, hivyo sababu nasi jana tumepata kifo kimoja cha kwanza kilichotokana na huu ugonjwa
Hivyo nitashauri utaratibu huu wa lockdown sababu inawezekana na sisi hali ikiwa mbaya itabidi serikali isimamishe wananchi kufanya shughuli yeyote.

Kwa hali za kiuchumi za watanzania wengi ni ngumu sana kufanya total lockdown, sababu watakufa au watapata shida kubwa na vitu vingine kama njaa, magonjwa mengi n.k
Hivyo nitashauri Serikali ifanye half lockdown, inawezekana half lock down ni msemo mpya ila katika half lockdown nitashauri serikali ifanye mambo yafuatayo

a. (1)Kupunguza muda wa kazi kwa taasisi zote binafsi na serikali.
Kupunguza masaa ya kazi Kutoka masaa yaliyopo sasa hadi nne, lengo la kupunguza muda wa kazi ni kuwawezesha wafanyakazi kuchelewa kuingia ofisini na kuwawezesha wafanyakazi Kutoka ofisini mapema mfano. Kuingia ofisini saa nne na kutoka saa nane.
Dhumuni la kupunguza muda wa kazi ni kupunguza msongamano wa watu kwenye usafiri sababu hiyo ndio sehemu kubwa ambayo ni rahisi watu wengi kuambukizana huu ugonjwa haraka na ikikumbukwa serikali imetoa tamko kwa daladala kupakia level siti hivyo tabu ya usafiri ni kubwa sana, hivyo kitendo cha kupunguza muda wa kazi kitawawezesha wafanyakazi kusafiri bila pressure za Kuwai usafiri asubuhi au kuchelewa usafiri jioni.

(2) Njia ya pili kuhusu wafanyakazi, serikali inaweza kuanzisha utaratibu wa kufanya kazi kwa shift kama ilivyo hospital, polisi, bandari, TRA kwa baadhi ya department n.k
Lengo ni lile lile kupunguza pressure za usafiri asubuhi na jioni sababu eneo la usafiri ndio eneo ambalo rahisi sana watu kuambukizana
Izingatiwe kuwa tatizo la usafiri limekua kubwa sana asubuhi na jioni kwa karibu mikoa yote Tanzania , serikali imeanzisha utaratibu wa kuziambia daladala ziwe na level siti, ila utekelezaji wake ni hafifu hasa nyakati za jioni na usiku watu wakiwa wengi na traffic police hawapo barabarani.

2. (a)Serikali iweke akiba ya kutosha ya chakula kitakachotosha nchi kwa Miezi sita hadi mwaka sababu, nchi karibu zote duniani zimeathirika na huu ugonjwa hivyo ni ngumu sana kwa nchi moja kutoa msaada kwa nchi nyingine ikiwa kila nchi ina tatizo la njaa

(b) Ikiwezekana serikali ifunge mipaka kuuza mazao ya chakula nje ya nchi, ili kuwezesha nchi kuwa na akiba ya kutosha ya chakula, sababu tunaona jirani zetu Kenya wameshaanza kuchukua hiyo hatua hivyo ni vizuri nasi tukaiga ilo jambo zuri.

3. (a)Serikali kuanzisha utaratibu wa lazima kwa watu wote kuvaa mask ( Barakoa) kwenye mikusanyiko ya watu kama sokoni, kwenye vyombo vya usafiri vya jumuia n.k lengo ni kupunguza maambukizi ya huu ugonjwa kwa njia ya hewa, sababu tumeona hili kosa hata kwa Mheshimiwa Raisi mwenyewe anasalimiana na watu kwa kugonganisha miguu lakini ajavaa mask (barakoa) na wakati huu ugonjwa unaambukiza hata kwa njia ya hewa.

(b) Pia serikali kushauri wananchi kuvaa nguo zinazoficha sehemu kubwa ya mwili hasa suruali na mashati marefu kwa wanaume na wanawake au nguo za aina yeyote zinazoficha sehemu kubwa ya mwili

Karibuni kwa ushauri na mawazo mbalimbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom