#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Ugaidi wenyewe ni ugonjwa wa kutengeneza kama corona, kwa hivyo kwanza unaiwachia corona kutekeleza malengo yake. Ikimaliza ugaidi utachukua nafasi yake katika jamii. Waswahili tunasema 'lila na fila hazitangamani.'
 
Mawazo yangu,

Kwa reference ya nchi kama Italy , ni wazi kua Corona sasa imefika peak, na idadi ya vifo na maambukizi yatazidi kushuka:

1- Wiki tatu za mwanzon za mwezi wa nne ndo zitashuhudia vifo vingi zaidi.

2- Idadi ya vifo kwa Afrika nzima haitafika 1500 mpaka huu ugonjwa unaisha kabisa, vifo vingi kwa Afrika vitatoka juu katika Jangwa la Sahara, huku vifo kwa nchi zilizo chini ya jagwa la Sahara havitazidi 500.

3- Bila shaka USA, Italy, UK, Spain, Ufaransa na Ubeligiji ndo nchi zitakazokua zimeathirika zaidi na tatizo. Ambapo USA Atakua na vifo vingi zaidi kuliko nchi yoyote.

4- Uchumi utakua sawa na kuimarika na maisha ya kawaida (kama ilivyokua kabla ya Corona) kwa dunia nzima kuanzia mwaka 2023 hasa kwa sekta ya utalii na biashara za kimataifa.
 
haszu,
Waafrika tunafia majumbani bila kufika hospital, sisi suala la homa na mafua huwa tunalichukulia kawaida mtu atanunua dawa na kuztumia bila kwenda hospital na hata huko hospital tufaa ya kutoka kituo kidogo kwenda hospital kubwa haswa maeneo ya vijijini hautaipata utaambiwa tu meza dawa mafua hayo utapona
 
Wakuu kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali yetu kupambana na covid 19 hakika kama ingekuwa ni janga basi Watanzania tungekwisha tupukutike!

Shughuli zingine zote zinaendelea, shule na vyuo tu ndio vimesimama, sioni ulazima wa vyuo na shule kufungwa kwa kuepuka corona kama janga kwa nchi yetu.

Corona ipo kwaajili ya wazungu huko Ulaya, ni zamu yao sasa wacha iwanyooshe. Huku Africa tunapambana na majanga yetu ya maralia, njaa, ebola na mengine mengi. Wazungu wanataka kulazimisha janga lao liwe la dunia nzima. Haiwezekani.

PM Majaliwa tunaomba usiongeze muda wa kufunga shule na vyuo, watoto warudi kusoma kuanzia tarehe 17 Aprili.
 
Back
Top Bottom