#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Hilo jua la kishindo unalosubiri Njombe, Makete huko pia litakuwepo???
Waulize wakazi wa huko! Hao ndio wanatakiwa sasa hivi wadhibiti movement za watu wanaotoka kwenye mikoa yenye maambukizi ili wabaki salama!
 
Lugha gani ya hovyo imetumika?
Tangu corona imeanza kusikika umewahi bahatika kumuona kwa macho mgonjwa wa corona aliyehoi bin taabani Tanzania?
Hao waliyokufa tunaambiwa walikuwa na maradhi mengine na sijasikia wakitangaza kwamba kuna wagonjwa wenye wenye hali mbaya wa corona,utasikia wagonjwa wanaendelea vizuri mara unasikia kifo cha corona.
 
Wakuu kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali yetu kupambana na covid 19 hakika kama ingekuwa ni janga basi Watanzania tungekwisha tupukutike!

Shughuli zingine zote zinaendelea, shule na vyuo tu ndio vimesimama, sioni ulazima wa vyuo na shule kufungwa kwa kuepuka corona kama janga kwa nchi yetu.

Corona ipo kwaajili ya wazungu huko Ulaya, ni zamu yao sasa wacha iwanyooshe. Huku Africa tunapambana na majanga yetu ya maralia, njaa, ebola na mengine mengi. Wazungu wanataka kulazimisha janga lao liwe la dunia nzima. Haiwezekani.

PM Majaliwa tunaomba usiongeze muda wa kufunga shule na vyuo, watoto warudi kusoma kuanzia tarehe 17 Aprili.
Ungeweza tu kufungua shule yako.
 
Nawasalimuni Watanzania wenzangu.

Bila kupoteza wakati niende moja kwa moja kwenye suala lililonifanya kufungua uzi huu.

Unajua tangu serikali itangaze kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza wa COVID19 nchini, kumeibuka mambo mengi sana ya uongo na ukweli na mengine ya kiuchonganishi na ya kutishia amani.

Katika kipindi hiki, kila mtu amekua daktari na nabii. Utasikia mara teknolojia ya 5G ndio imeleta Corona, mara ilitabiriwa na manabii itatokea, mara marekani ametengeneza ili aitawale dunia. Mara ugonjwa umeundwa na wazungu ili wauze dawa.

Mbaya zaidi, nchini sasa kumeibuka mtindo mi nauita wa kipumbavu eti watu wawili wakifa kwa kuachana muda mfupi, na ikionekana walikuwa karibu, basi watu wanahitimisha ni corona. Huu ni ujinga wa hali ya SG, laiti kama Ruge na Kibonde wangekufa kipindi hiki, najua midomo michafu ingesema Clouds media imevamiwa na Corona.

Wanasiasa na viongozi wa dini, msichukulie janga hili kama fursa ya kujiimarisha kiuchumi na kisiasa. Waambieni watu wenu wajikinge. Msijifanye wasemaji wa mienendo ya ugonjwa huu, sio jukumu lenu.

Huu ni wakati wa kuwa bega kwa bega na serikali ili kukabiriana na janga hili.

Serikali tuiache ifanye majukumu yake, ushauri ni muhimu ila utolewe kwa nidhamu na bila unafiki wowote. Kumbuka serikali ni chombo kilichobeba watu mbalimbali, wasomi na wabobezi wa mambo mengi na wengi wanekuzidi mbali na hiyo degree au masters yako.

#TUCHUKUE TAHADHARI CORONA NI HALISI ILA TUTASHINDA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS
Sure mzee Baba,hali ni tete...
 
IMG_20200411_044022.jpg

Serikali hii ndio imejaza wasomi na wabobezi?
Jamani nishikeni naanguka,
Chii...chii...chiiii....chiniiiiiii!

HABARI : Mwana JF azimia kwa mshtuko...
 
Nawasalimuni watanzania wenzangu.

Bila kupoteza wakati niende moja kwa moja kwenye suala lililonifanya kufungua uzi huu.

Unajua tangu serikali itangaze kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza wa COVID19 nchini, kumeibuka mambo mengi sana ya uongo na ukweli na mengine ya kiuchonganishi na ya kutishia amani.

Katika kipindi hiki, kila mtu amekua daktari na nabii. Utasikia mara teknolojia ya 5G ndio imeleta Corona, mara ilitabiriwa na manabii itatokea, mara marekani ametengeneza ili aitawale dunia. Mara ugonjwa umeundwa na wazungu ili wauze dawa.

Mbaya zaidi, nchini sasa kumeibuka mtindo mi nauita wa kipumbavu eti watu wawili wakifa kwa kuachana muda mfupi, na ikionekana walikuwa karibu, basi watu wanahitimisha ni corona. Huu ni ujinga wa hali ya SG, laiti kama Ruge na Kibonde wangekufa kipindi hiki, najua midomo michafu ingesema Clouds media imevamiwa na Corona.

Wanasiasa na viongozi wa dini, msichukulie janga hili kama fursa ya kujiimarisha kiuchumi na kisiasa. Waambieni watu wenu wajikinge. Msijifanye wasemaji wa mienendo ya ugonjwa huu, sio jukumu lenu.

Huu ni wakati wa kuwa bega kwa bega na serikali ili kukabiriana na janga hili.

Serikali tuiache ifanye majukumu yake, ushauri ni muhimu ila utolewe kwa nidhamu na bila unafiki wowote. Kumbuka serikali ni chombo kilichobeba watu mbalimbali, wasomi na wabobezi wa mambo mengi na wengi wanekuzidi mbali na hiyo degree au masters yako.

#TUCHUKUE TAHADHARI CORONA NI HALISI ILA TUTASHINDA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Endelea kuosha mikono
Acha kujitia jeuri
 
Kwa taarifa za maambukizi kwa ujumla na vifo vya jumla na nchi moja moja. Ili uifaidi ukishafungua kupitia browser hasa crome ingia kwenye vidot vitatu vilovyoupande wa juu kulia kisha nenda sehemu iliyoandikwa "add to home screen" kisha itakaa kama app kwenye simu.
Kuingia gusa hapa Corona Virus Live Tracker

Baadhi ya vifupisho na maana zake.

C - confirmed
D- Death

C-today - confirmed today
D -today - deaths reported today
 
Mmh wanatoa taarifa za hapa nchini zinazofanana naza ummy au zao zinaingia akilini na kukaa
 
Kila mmoja anaona hatari iliyopo mbele yetu, Sishawishiki kuwa Magufuli kama halioni hilo. Ugonjwa wa milipuko unaanza kidogo kidogo kama Epidemic halafu ukishika kasi ndiyo tunapoanza kusikia neno Pandemic.

Dunia hii siyo ngeni kwa magonjwa makubwa ya milipuko, tulikuwa na kipindupindu (Bado kipo nchini mwetu ila huwa ina kawaida ya kutulia kama kunakuwa na usafi hivyo hao Vibrio cholerae wanapungua au wanakuwa inactive), Yellow fever, bubonic plague nk.

Historia ya dunia inaonyesha kuna kipindi Spanish Influenza iliyotokea mwaka 1918-1920 iliua watu kati ya Millioni 17 hadi Milioni 50, Bubonic plague ambayo nadhani tuliita tauni, iliyobebwa na nzi kutoka kwa panya iliua watu zaidi ya 150 Milioni ikapunguza idadi ya watu duniani.

Haya magonjwa yanakuja na kupita kwa muda fulani, kwa mfano kukiwa na mlipuko wa Kipindu pindu au Cholera, watu tunawekewa quarantine, hatusalimiani au hatukusanyika kwa sababu ya nature ya hao bacteria (Contagious). Cholera ilishaua watu wakaribiao Millioni 1 katika nchi za Africa Magharibi, Asia na Mashariki ya mbali na hata Tanzania imetusumbua miaka ya 1978, 1980, na 1982.

Kuhusu Corona, hawa virus wanakaa kwenye hewa kwa masaa manane na sehemu zingine kama kwenye maboksi, majani, miti na vyuma anakaa muda mrefu zaidi.

Ugonjwa huu ni hatari, kwa vile unaua haraka haraka sana kwa sababu unashambulia njia ya upumuaji (respiratory systems) hivyo waathirika mara nyingi mapafu yanaharibika hivyo kunatokea "Respiratory distress" hakuna asiyejua jinsi magonjwa ya kupumua yalivyo na changamoto hasa kwa nchi maskini kama yetu isiyo na ventillators au hata zile ambazo zipo zinakuwa za zamani ambazo ufanisi wake umekuwa mdogo.

Uwezo wa hospitali zetu ni mdogo na wataalamu wetu ni wachanga kukabiliana na majanga kutokana na kutokuwa na uzoefu mkubwa. Iwapo kutatokea matatizo makubwa madaktari wetu na wauguzi bado ni dhaifu kwenye kupambana na majanga....Vifaa vipo vichache tunategemea tupewe msaada na hao hao wachina ambao ugonjwa umeanzia kwao!

Inavyoelekea sasa kuna maambukizi makubwa....Kuna watu waliotembelea Tanzania wakarudi kwenye nchi zao wakakutwa na ugonjwa...Je hao wameambukiza watu wangapi?
Mazingira ya watu waliokufa juzi wametoka ofisi moja na hilo linatia shaka....Hiyo community transmission anayosema waziri wa afya mbona ilishaanza kable waziri hajalitangaza?

Ukweli ni kwamba tunaingia kwenye kipindi kigumu kwa sababu inaonekana tayari mlipuko umeshakua (Sijui kwa kiasi gani...lakini uwezekano ni mkubwa). Mungu atusaidie
Magonjwa ya Milipuko yanapita na kurudi yanachukua muda mrefu, lakini kipindi hicho cha matatizo kama hatua hazijachukuliwa huwa unasababisha vifo vingi.

Kama mwananchi ninayelitakia mema taifa hili ningemshauri Magufuli asikilize anachoambiwa na wataalam wa Afya, WHO kuhusu umuhimu wa kuzuia mikusanyiko kwani hiyo ndiyo njia kuu ya kueneza ugonjwa (Contact, Airborne transmission).

Ugonjwa utapita na watu wataendelea na shughuli zao kama kawaida kama ilivyo kwenye mji wa Wuhan katika jimbo la Hubei ulikoanzia ambako umerudi kwenye hali ya kawaida na shughuli za biashara na uchumi zimeanza.

Suala la kuwa tumezungukwa na nchi nane (8) zinazotutegemea halina tija. Kwani shughuli za usafirishaji mizigo unaendelea...Kinachozuiwa ni movement of people na hilo haliathiri biashara yoyote.

HUU NI USHAURI TU.
 
Wakuu tunatishana sana.

Kaugonjwa haka ni kadogo sana tunakakemea kwa Jina la Yesu Kristo kanapotelea huko
Tena haka ni kakukakemea kwa Jila la Yesu.

Yaani hapa ndio ulimwengu unahitaji Yesu Kristo alie hai. Karibuni kwa Yesu nafasi bado zipo huku bhana kuishi ni faida kufa ni Kristo.
 
Back
Top Bottom