#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Ndugu zangu nafikiri, mwelekeo na msimamo wa Serikali umeshawekwa bayana.

Aidha, Wizara imeshatuweka wazi kuwa maambukizi ya ndani (community transmission) yameanza. Maana yake chepe imeshapata kokoto.

Nafikiri sisi individually na kwa ujumla wetu tuchukue tu tahadhari na kuzingatia Maelekezo ya Wizara ya Afya.

Changamoto tuliyonayo kwa Sasa ni kwamba tunatakiwa tule na kupata mahitaji yetu binafsi na familia zetu, wakati huo huo tukitakiwa kuhakikisha kwamba hatuambukizwi kutoka maeneo tukakotafutia riziki zetu.

Yaani ni kama tunalazimishwa kusolve "X& Y" kwa wakati mmoja, hata kama zile hesabu za "Simultaneous Equation" zilitupita kushoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si wameshawaambia mchukue tahadhari; au mnataka wawachape viboko ndio mtie akili?
Kama wanasema tuendelee kuchapa kazi na kazi yangu niya kuuza nguo pale mtaa wa Congo au viatu pale Karume au mie ni konda wa daladala au bodaboda naendelea kupiga kazi. Sasa wewe ungenisadia, kwa kazi zangu hizo kunawa mikono kuna nisaidia Nini?
 
Sasa rais kazi yake nini?Kama hawezi kuongoza wananchi wake kwenye kipindi kigumu Kama hiki na kutoa mipango ya serikali ilivyojipanga kutuvusha
Lofa wewe, Rais aongee na aeleze mala ngapi? lini Rais kila anapoongea hajatoa maelekezo?

Chini ni moja ya chapisho la serikali lenye maelezo ya nini cha kufanya kujikinga na maambukizi, mfano umeambiwa kaa mita moja hadi mbili apart, makanisa na misikiti haijafungwa, ukikuta watu weshajaa na hakuna hiyo nafasi maana yake rudi nyumbani, vivyo hivyo sokoni na sehemu zote zenyemikusanyiko.

Serikali na Rais keshafanya part yake na sasa ni wajibu wetu kujilinda, Rais hatokuja kukulinda wewe na familia yako, ni wajibu wenu kujilinda kwa kufuata maelekezo ya Serikali.
IMG_20200411_163847.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sumve 2015,
Mkuu pole sana,Mimi muuza mitumbs wa karume na Congo street au dereva wa daladala au abiria daladala na mwendokasi au mabasi ya mkoa au muumini wa gwajima huo mwongozo uchwara unanisadia nini wakati unanihimiza nipige kazi?
 
Hakuna kipindi kigumu kinachoboa kama hiki, hasa pale unapokuwa na jambo furani unataka kulifanya/tekeleza alafu limekwamishwa na Corona sasa unaposubiri Corona iishe au hali itulie nawakati iyo Corona haijasema itaiasha lini.

Imagine wale walikuwa wanafanya shughuli zao kwenye taasisi ambazo zimesimama kazi kuipisha Corona hapa sio tatizo tatizo ni pale uyo Corona ajasema anatoweka lini.

Subira ambayo hujui deadline yake inakereketa sana.
 
Mwezi huu nilipanga nitoe mahari,nimuoe rasmi mchumba wangu,tumedumu miaka 6,tungelioana mwaka jana tukaafikiana tujenge kwanza tufikie kwetu,basi mwezi March nilijipanga kuanza harakati nitoe mahari kisha mwezi July tufunge ndoa tuishi officially, corona katibua mipango,kazi zimesimama hela niliyoanza kuandaa ya mahari imebidi itumike kununua mahitaji mhimu na kutunza akiba ya dharura yeyote.
CORONA nenda sasa umetosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwezi huu nilipanga nitoe mahari,nimuoe rasmi mchumba wangu,tumedumu miaka 6,tungelioana mwaka jana tukaafikiana tujenge kwanza tufikie kwetu,basi mwezi March nilijipanga kuanza harakati nitoe mahari kisha mwezi July tufunge ndoa tuishi officially, corona katibua mipango,kazi zimesimama hela niliyoanza kuandaa ya mahari imebidi itumike kununua mahitaji mhimu na kutunza akiba ya dharura yeyote.
CORONA nenda sasa umetosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
duh hatarii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1586643983652.png


Corona imetusaidia kupigia mstari tatizo la uhaba wa maji yanayotiririka katika jamii yetu. Hii ni kero tunayoiimba kila mwaka wa uchaguzi na waheshimiwa sana wakishaapishwa huwa na vipaumbele mbadala.

Ni wazi Waziri Ummy pia amefahamu kuwa si mikono wala vijijini watu wanahitaji madumi ya kunawia mikono. Masumura haya yasingepatikana pasi gonjwa hili kutokea.

Hata baada ya mlipuko wa corona kumalizika maisha yetu hayatakuwa kama yalivyokuwa za nani. Kunawa mikono litabaki kuwa Jambo la muhimu. Usije kushangaa kuona chupa za sanitizer katika chumba cha hoteli mbali na beseni la kunawia mikono.

Kama Kuna wenye uwezo wa kutengeneza taulo za karatasi. Hii ni bidhaa itakayo simu kuwa muhimu kwa miaka ijayo. Ni rahisi kutumia karatssi na kutupa kuliko vikausho vya umeme.
 
Please, NO mandatory vaccines. Everyone should be able to choose their own healthcare.
 
Karibia makundi yote ya ugaidi yanafadhiliwa na hao hao wanaojifanya wanapinga na kuzuia ugaidi...

Kwa sasa wapo busy kuzia Covid19...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom