Lugumgya
JF-Expert Member
- Dec 10, 2019
- 629
- 2,006
Ndugu zangu nafikiri, mwelekeo na msimamo wa Serikali umeshawekwa bayana.
Aidha, Wizara imeshatuweka wazi kuwa maambukizi ya ndani (community transmission) yameanza. Maana yake chepe imeshapata kokoto.
Nafikiri sisi individually na kwa ujumla wetu tuchukue tu tahadhari na kuzingatia Maelekezo ya Wizara ya Afya.
Changamoto tuliyonayo kwa Sasa ni kwamba tunatakiwa tule na kupata mahitaji yetu binafsi na familia zetu, wakati huo huo tukitakiwa kuhakikisha kwamba hatuambukizwi kutoka maeneo tukakotafutia riziki zetu.
Yaani ni kama tunalazimishwa kusolve "X& Y" kwa wakati mmoja, hata kama zile hesabu za "Simultaneous Equation" zilitupita kushoto.
Sent using Jamii Forums mobile app