#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Nahisi kama nimpe mtu flani kwa makusudi IP address yangu ili anidhibiti kabisa kiranga cha kutaka kuchangia nyuzi za COVID-19 kuanzia leo tarehe 17/05/2020 na siku chache zinazofuata.
 
Nimekaa nikatafakari kwa kina sana, nikagundua kwamba, dawa ya ugonjwa kama Corona inaweza ikawa ni kutouzungumzia kabisa, utashangaa ugonjwa unayeyuka wenyewe na hata wagonjwa wanapotea kabisa, hii phenomena bado naifanyia utafiti, nitatolea andiko la kina sana.
"Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwakujidanganya kuwa hayapo." JK Nyerere
 
Nimekaa nikatafakari kwa kina sana, nikagundua kwamba, dawa ya ugonjwa kama Corona inaweza ikawa ni kutouzungumzia kabisa, utashangaa ugonjwa unayeyuka wenyewe na hata wagonjwa wanapotea kabisa, hii phenomena bado naifanyia utafiti, nitatolea andiko la kina sana.

Naibu waziri wa ameondoka tutaachaje kuzungumzia hilo siku ya leo?
 
Wakuu habari

Mimi binafsi nimekuwa nikitafakali kuhusu hili janga la corona linalotesa dunia kwa sasa, japo naona WHO wanaona kabisa sio ugonjwa wa kuisha, tutaendelea kuishi nao.

Nikiangalia hali ya mtaani, na mitandaoni kuhusu huu ugonjwa wa corona nabaki mdomo wazi, sijajua kwanini

Kwanza kabisa huu ugonjwa haueleweki, wataalamu wanaongezea na kusema virusi vinajibadili.

Mtu anaweza kuwa na ugonjwa na asioneshe dalili (hili ni tatizo kubwa), tena anadunda kama kawaida, anafanya kazi zake, hakohoi, joto halipandi, kifua hakibani, hakuna dalili yeyote, sasa huyo anakuwa mgonjwa au ni fix!

Mtu anaweza ugua na kupona mwenyewe (sasa hapa mtu anapata wapi morali ya kwende kupima)

Ugonjwa unamiezi zaidi ya miezi 9, ila hata huko ulipoanzia hawauelewi .

Sasa hiki ni kitu gani.

Inafika hatua watu wanaanza kuchukulia poa.

Uzi tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naibu Rais Daud Bashite wameachia watu waache kunawa mikono wakae vijiweni vibarazani makanisani misikitini misibani waambukizane kwa wingi wafe kwa wingi ili wapate kisingizio cha kuahirisha uchaguzi mkuu
Nilijua tu lazima umtaje basha wako wa zamani
 
Nasubiri kuona km hadi December kila Nchi zitakuwa zinatangaza maambukizi mapya
Hahaaa, hataree sana, ugonjwa unafunga mechi za mpira zisichezwe, shule na mavyuo kufungwa, maduka na Bar, kukaa ndani, viungo vya nje kuwa sehemu za siri nk... Dah viumbe siie wadhaifu sana. Ugonjwa usioua bodaboda😀😀😀😀
 
Hata mafua, wengine wanapiga chafya, wengine homa kali na wengine yanaishia ndani kwa ndani.

Virusi hivi vya mafua vya covid vinanguvu maradufu. Naamini nguvu yake itaenda na kuisha baada ya miaka kadhaa hatutakuwa navyo milele kama HIV.

Mfano wa mafua makali kama haya yalochakaza dunia ni Spanish flu miaka mia ilopita. Haya yalidumu kwa miaka mitatu na kupotea yenyewe hakukuwa na kinga wala dawa.

Spanish flu inakadiriwa iliambukiza watu million 500 na kuua takribani asilimia 10 ya hao.

Kumbuka hata mafua ya kawaida aghalabu wengi wetu hatutumii dawa yoyote na hupotea yenyewe. Kwa covid ndivyo hivyo kwa asilimia 60 hadi 70 ya wanaoupata hupona bila kujua. Kinachogomba ni kasi yake ya maambukizi na vifo kwa wale wenye kinga dhaifu.

Tuendelee kuishi kwa taadhari, maisha yaendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajiuliza hivi wanaokufa kwa corona ni watu gani?
Bodaboda wapo imara,mamantilie wapo imara husikii hata mtu kuumwa

Ila ukiingia Jamii forum na Twitter Ndio kuna watu wanadeka sana mara hivi mara vile
Hahaaa, hataree sana, ugonjwa unafunga mechi za mpira zisichezwe, shule na mavyuo kufungwa, maduka na Bar, kukaa ndani, viungo vya nje kuwa sehemu za siri nk... Dah viumbe siie wadhaifu sana. Ugonjwa usioua bodaboda😀😀😀😀
 
Corona ni mafua tu Sema kuna watu walijazwa uwoga na media za Mabeberu
Hadi rais mwanzo alisema ni kaugonjwa tu ila sijui nae alisikiliza mabeberu ghafla akabadili gia na kusema huu ugonjwa ni hatari wakutuokoa ni Mungu pekee kwahiyo tusali na tupige....
 
Wakuu habari

Mimi binafsi nimekuwa nikitafakali kuhusu hili janga la corona linalotesa dunia kwa sasa, japo naona WHO wanaona kabisa sio ugonjwa wa kuisha, tutaendelea kuishi nao.

Nikiangalia hali ya mtaani, na mitandaoni kuhusu huu ugonjwa wa corona nabaki mdomo wazi, sijajua kwanini

Kwanza kabisa huu ugonjwa haueleweki, wataalamu wanaongezea na kusema virusi vinajibadili.

Mtu anaweza kuwa na ugonjwa na asioneshe dalili (hili ni tatizo kubwa), tena anadunda kama kawaida, anafanya kazi zake, hakohoi, joto halipandi, kifua hakibani, hakuna dalili yeyote, sasa huyo anakuwa mgonjwa au ni fix!

Mtu anaweza ugua na kupona mwenyewe (sasa hapa mtu anapata wapi morali ya kwende kupima)

Ugonjwa unamiezi zaidi ya miezi 9, ila hata huko ulipoanzia hawauelewi .

Sasa hiki ni kitu gani.

Inafika hatua watu wanaanza kuchukulia poa.

Uzi tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
Tungekuwa tunapata takwimu sahihi hapa Tz tungejua kwamba corona ni hatari au la. Serikali inafanya makosa makubwa kutotoa takwimu sahihi.
 
Back
Top Bottom