Wakuu habari
Mimi binafsi nimekuwa nikitafakali kuhusu hili janga la corona linalotesa dunia kwa sasa, japo naona WHO wanaona kabisa sio ugonjwa wa kuisha, tutaendelea kuishi nao.
Nikiangalia hali ya mtaani, na mitandaoni kuhusu huu ugonjwa wa corona nabaki mdomo wazi, sijajua kwanini
Kwanza kabisa huu ugonjwa haueleweki, wataalamu wanaongezea na kusema virusi vinajibadili.
Mtu anaweza kuwa na ugonjwa na asioneshe dalili (hili ni tatizo kubwa), tena anadunda kama kawaida, anafanya kazi zake, hakohoi, joto halipandi, kifua hakibani, hakuna dalili yeyote, sasa huyo anakuwa mgonjwa au ni fix!
Mtu anaweza ugua na kupona mwenyewe (sasa hapa mtu anapata wapi morali ya kwende kupima)
Ugonjwa unamiezi zaidi ya miezi 9, ila hata huko ulipoanzia hawauelewi .
Sasa hiki ni kitu gani.
Inafika hatua watu wanaanza kuchukulia poa.
Uzi tayari
Sent using
Jamii Forums mobile app