#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Kiukweli sijala limao ila majani yake ndo tunachemsha, hata nyungu sijapiga bado.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi sijala limao wala tangawizi nakunywa sana maji hata kipindi nilijihisi mgonjwa kichwa kiliuma sana na mwili ulikuwa umechooka km mwezi mzima wa 3 kwenda wa nne sikumwambia mtu nilipunguza safari nikawa nashinda peke yngu sana ndani.
 
Aksante Mama Tibaijuka kubutua Kombolela

Mie leo nimezurura mjini bila ya Tambala la kufunika pua na Mdomo kama afanyavyo Mwamba wetu

Baada ya kufuturu hapa natandika Limao na matangawizi mpaka yanikome

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu ametushushia ugonjwa, na ametujaalia msimu wa malimao yenye maji mengi kama machungwa, mungu amejibu dua zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wanampenda na kumweshimu raisi Magufuli wachache ndo hujidai manunda mtandaoni.

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Mimi binafsi na familia yangu tumesha yapiga sana malimao ili kujikinga na corona

Na siamini kama kuna mkazi wa hapa dar hajawahi kula limao kwa kipindi hichi cha kupambana na corona na kama yupo ana stahili pongezi kwa jinsi alivyo na roho ngumu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mie sijala ila nmeambiwa Pilipili kichaa pekee ndo tiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijagusa chochote walichopendekeza, bar tu ndo nimeacha kwenda.

semper fidelis
 
Admini asisahau kuwadai na wale "TAUSI" wetu aliowapa jirani zetu.[emoji848][emoji2955]
Screenshot_20200518-235331_Opera%20Mini.jpeg
 
Ni wazi mtakubaliana na mimi kuwa watendaji wengi wa serikali ni wazembe. Kitu ambacho ungekipata ndani ya dakika 2 itakuchukua mwezi yaani ubunifu zero kabisa.

Hebu imagine tungefungiwa hako kagawio ka chakula kule kijijini kwenu ndugu zako wangefikiwa lini? Kifupi njaa ingetumaliza kabla ya corona.

Uamuzi wa Magufuli uliona mbali ila ulipaswa kuboreshwa na si kuacha mambo kuwa holela kama ilivyo leo
 
Ni wazi mtakubaliana na mimi kuwa watendaji wengi wa serikali ni wazembe. Kitu ambacho ungekipata ndani ya dakika 2 itakuchukua mwezi yaani ubunifu zero kabisa. Hebu imagine tungefungiwa hako kagawio ka chakula kule kijijini kwenu ndugu zako wangefikiwa lini? Kifupi njaa ingetumaliza kabla ya corona.

Uamuzi wa Magufuli uliona mbali ila ulipaswa kuboreshwa na si kuacha mambo kuwa holela kama ilivyo leo
Dawa ya corona

Ni kuishi kama vile hakuna corona


Toa kichwani hio kitu basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahospitali mengi hayana mrundikano wa wagonjwa kwa Sasa Kama ilivyokuwa awali kabla corona, ila pia wagonjwa wengi wanaishia kwenye maabara na baadhi ya hospitali za private huku wakilazimisha kutoandikiwa kulazwa.

Hali hii ya wagonjwa kukaa nyumbani haiwezi kuchangia vifo kwa kukosekana matibabu sahihi kwa wagonjwa? Hospitali Kama muhimbili haina wagonjwa wengi wodini Kama awali,ocean road wagonjwa asilimia kubwa wamekuwa discharged pamoja na hospital nyingine.....ni upi mkakati wa wizara kukabiliana na Hali hii?
 
Ni kweli unachosema, hata jana usiku nilikuwa naongea na staf wa mount nae anashangaa ni kwa nn wagonjwa wamepungua saanaa!

Na hata ukiangalia trend ya vifo vya korona kwa sasa ni kama imeshuka hata kwenye mitandao"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Korona sio gonjwa kubwa kwa nchi nyingi za kiafrika.ukifuatilia kwa makini wengi tunacheza wimbo wa nchi za ulaya ambazo zimeadhirika Sana.mwanzo huku mikoni tuliofia Sana watu wanaotoka dar kuikimbia korona lakini mpaka leo WILAYA nyingi hazina hata mgonjwa mmoja.hii unatoka na elimu ya kujikinga inayiendelea kutolewa na serikali.
USHAURI kwa serikali iangalie kwa makini swala la kufungua shule hasa misongamano madarasani,kwenye daladala nk.sababu ugonjwa ukitokea chuo au shuleni utazua taaruki kubwa Sana kwa wazazi.na lawama yote itakuwa juu ya serikali.
Shughuli zingine tuchape kazi.
Watalii karibuni tupo tayari kuwahudumia.
Tiba mbadala inatibu nimeshuhudia.
JPM anakaribia kushinda


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndugu

Kwa ufupi wanasema mwanzoni kama nchi hawakuheshimu wala kuzingatia tahadhari ya kuepuka maambukizi, leo hii taifa linashuhudia idadi kubwa yamaambukizi na vifo, wauguzi sekta ya afya huko ni kama sasa imezidiwa na wagonjwa! ambapo katika masaa ishirini na nne yaliyopita wameripoti idadi kubwa kabisa ya vifo vya watu 1000...hii hali inatisha sana.

Hizi Habari za kuiaga corona hapa Dar zinaleta wasiwasi kwa sasa ni vema basi tungevuta subira kwanza ni kama bado mapema kufikiria kuwa huyu adui corona keshatoweka mjini.
 
Hawa ndugu .. Kwa ufupi wanasema mwanzoni kama nchi hawakuheshimu wala kuzingatia tahadhari ya kuepuka maambukizi, leo hii taifa linashuhudia idadi kubwa yamaambukizi na vifo,wauguzi sekta ya afya huko ni kama sasa imezidiwa na wagonjwa! ambapo katika masaa ishirini na nne yaliyopita wameripoti idadi kubwa kabisa ya vifo vya watu 1000...hii hali inatisha sana.
Hizi Habari za kuiaga corona hapa Dar zinaleta wasiwasi kwa sasa ni vema basi tungevuta subira kwanza ni kama bado mapema kufikiria kuwa huyu adui corona keshatoweka mjini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Toa uchafu wako hapa, kila mtu apambane na hali yake
 
Back
Top Bottom