Mtazamo: Taasisi na mashirika ya Serikali ambayo yana huduma mbovu kwa wateja Tanzania

Unauhakika alimpa nani? Tafadhali milango ipo wazi akidhibitisha hili hatua zinachukulowa mara moja.

Tuache kutoa tuhuma za uongo ambazo hazina taarifa
Tuhuma za uongo?

Nilikuwa nakuona mtu kumbe nawe ni takataka tu, usiamshe hasira zetu, tuna mengi ya moyoni ambayo tumehifadhi kwa rushwa zenu.
 
Huyu admin anazingua tu hapa ukweli anaujua sana
 
Je ulitoa ya huduma gani?Tunawasisitiza malipo yetu yote yanalipwa kwa control number na kila kiasi unacholipa unapatiwa risiti, Tafadhali usifanya malipo kienyeji kisha unalalamika, Kama ulilipa TANESCO njoo tujulishe tukuhudumie
 
Aaah haina haja maana Hela ya sister haitarudi na kifupi alishawekewa umeme within 3days baada ya kutoa hela.....na kazi ilifanyika Kwa speed ya 5G
Bora aliwapa, si wana njaa!!!???? Mtu ukose umeme kisa laki moja?? Bora aliwapa wahuni hawa.
 
Tuhuma za uongo?

Nilikuwa nakuona mtu kumbe nawe ni takataka tu, usiamshe hasira zetu, tuna mengi ya moyoni ambayo tumehifadhi kwa rushwa zenu.
Tunajiamini kuwa tunafanya kazi kwa weledi kama kweli umeombwa rushwa au una changamoto njoo PM nakuahidi kukutembea na kuhakiksha unapata haki yako vinginevyo unakuwa haujatutendea haki kulaumu bila ushirikiano
 
Bora aliwapa, si wana njaa!!!???? Mtu ukose umeme kisa laki moja?? Bora aliwapa wahuni hawa.
usifanye malipo bila kufata taratibu tafadhali, Ni kosa kisheria
 
Taarifa moja ya uongo mliyozushiwa ndo inasafisha shirika lenu kuwa sio wezi na ni shirika la hovyo?
 
Unadhani ni mm tu niliyewahi kuonja joto la jiwe la shirika letu la Umma? Sina haja ya kuja PM maana hakuna asiyejua uozo wa shirika mkuu...
PM kufanya nini kwa mfano? Shirika hovyo saana hili, bora hata DAWASA.
 
Je ulitoa ya huduma gani?Tunawasisitiza malipo yetu yote yanalipwa kwa control number na kila kiasi unacholipa unapatiwa risiti, Tafadhali usifanya malipo kienyeji kisha unalalamika, Kama ulilipa TANESCO njoo tujulishe tukuhudumie
Zilongwa mbali, zitendwa mbalii... Kalagabahoo...
 
Tunashukuru sana, Tunaamini ukitulia utatumie taarifa za tuhuma husika naisis tutatoe ushirikaono
Ndugu yangu elewa kwamba TANESCO kuna shida na watu wengi tumeumizwa.
Nikuulize swali....
Mteja anapofungiwa Umeme waya zingine pale kwenye nguzo zinabanwa na Vishikizio/Vibanio vya chuma kushikanisha na waya wa meter ya mteja na ule wa Nguzo, je kwanin wateja wengine wanawekewa Hivyo vibanio na wengine hawawekewi vibanio hivyo. Yaaani waya zinazungushwa zungushwa tu imetoka hiyo na mvua ikinyesha zikapata carbon umeme unakata kata kwa mteja wakati yule aliyewekewa vibanio anakula goodtime? Tueleze inakuwaje halafu mimi nifunguke hapa hapa na ushahidi??
 
Mimi nasimamia ujenzi sehemu nyingi ndani ya Dar.

Wanapokuja kufunga mita, gar yao inabeba kazi nyingi na hao vibarua wao sijui vishoka wanaitwa. Dereva anaweza akawaacha vibarua point A, kisha wengine awaache point B, ni kama umbali wa mita mia mbili, yaani viwanja viwili vya mpira,na gari inafika kabisa.

Sasa cha ajabu unaombwa uchangie ela ya mafuta ili gari ifike kwako wakufungie umeme. Kuna mambo ya kipuuzi mno, yanakera haswa. Tukianza kuyaandika haya ni kuinua hasira zetu tu.
 
Tunajiamini kuwa tunafanya kazi kwa weledi kama kweli umeombwa rushwa au una changamoto njoo PM nakuahidi kukutembea na kuhakiksha unapata haki yako vinginevyo unakuwa haujatutendea haki kulaumu bila ushirikiano
Nakubali, Ni kweli TANESCO makao makuu mpo serious na utowaji huduma. Tarehe 21 February Kuna changamoto ilitokea hapa Kilindi Tanga tukakaa siku 8 gizani, tukiwapigia TANESCO wilayani wanasema tutume Hela ya nauli ya fundi elfu 50! Juzi tarehe 29 saa mbili asubuhi nikapiga simu TANESCO makao makuu Dodoma nikaeleza Kila kitu, ilipofika saa Saba mchana mafundi wakaja kurekebisha. Big up TANESCO Headquarters. Lakini huku ngazi ya chini kunahitajika mabadiliko makubwa sana
 
Tunashukuru kwa pongezi je unaweza kutusaidia namba ya simu mliyopiga mkaambiwa mtoe hela? Tunaomba tufatulie tujue na kuchukua hatua
 
Tanesco hii ya january?
 
hivi ofisi ya raisi utumishi wa umma na utawala bora nae ni shirika?
haijalishi majibu,ofisi ya raisi utumishi wa umma na utawala bora ni kitengo kibovu sana,chukulia mtu anasumbuliwa uhamisho mwaka mzima,ila akitoa rushwa tu baada ya wiki anahama.
katibu mkuu utumishi chungulia watu wako hapo ofisini wanaharibu kazi.
 
Hivi mfano,police wamekukamata na vitu vyako,mwisho wa siku wanasema vimepotea(wanataka kuvipiga)malalamiko haya ni nani unaweza kwenda kupeleka??
 
Ni kweli wanapenda kuchangisha Hela ya mafuta/ nauli, wakati mafuta ni ya serikali na wanalipwa na serikali. Ila dawa Yao ni kuandaa ushahidi na kuwaripoti makao makuu Dodoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…