Mtemi Ng'wanamalundi (Mwanamalundi) - Yesu wa Afrika?

Mtemi Ng'wanamalundi (Mwanamalundi) - Yesu wa Afrika?

Tatizo unadhani ujio wa Bwana Yesu duniani ulikuwa kufanya miujiza tu.

1 Yohana 4:10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.

1 Yohana 2:2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.



Nimekumegea kidogo tu hapo.Ila fahamu Tito 2:11-14 "Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema."

Hapa yohana ameefikaje hapa au unadhani wanaojadili jambo hili hawajui habari hizo na kwamba unaamini wewe ndiyo wa kwanza kujua habari za Yesu Pole sana tafakari ujue uliko toka na ujiulize hivi ni kwa nini watakatifu wote ni wazungu tu?????????????? Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako.
 
huwezi kumfananisha bwana yesu na mwanamalundi kwani yesu kristo ni mungu ila alikuja ulimwenguni akiwa na umbo la kibinadamu kuwafundisha wanadamu na kufisha umbo la kibinadamu kwa ajili ya dhambi za wanadamu nikiwemo mimi labda swali kama liko kwamba ni kwa vipi yesu ni mungu haya hapa: 1..... Wafilipi 2:5-11 hapa tunapata maelezo jinsi yesu alivyojifanya mwanadamu na ktk mstari wa 11 tunaambiwa kuwa kila ulimi wapaswa kukiri kuwa yesu kristo ni bwana imeandikwa kwa herufi kubwa na kama una biblia ya union version ya kiswahili nenda kabisa kule mwanzoni uone maana ya bwana inapoandikwa kwa herufi kubwa bila shaka utakuta kuwa hilo ni jina takatifu yaani jehova kama linavyoitwa kwa kiyaudi. 2.....sababu ya pili kuwa yesu ni mungu soma isaya 9:6 " kwa ajili yetu mtoto amezaliwa.............. Ataitwa mshauri wa ajabu,[mungu mkuu], baba wa milele, mfalme wa amani. 3....sababu ya tatu angalia 1timotheo 3:16 "bila shaka siri ya utauwa (uchamungu) ni kuu,mungu alijidhirisha ktk mwili...... Akaönekana na malaika,akaubiriwa ktk mataifa......" 4.....sababu ya nne tazama sisi wanadamu tunapokufa tunaamini ya kuwa mungu ndiye anatoa roho zetu lakini tazama yesu aliitoa roho yake mwenyewe yohana 19:30 takiriaani bibli nzima pamoja na histori yake ilishuudia ujio wa yesu kristo katika mwili lakini ni umoja pamoja na baba, na roho mtakatifu uwezi kutenganisha nafsi hizi 3 tazama 1 yohana 5:7-8 conclusion: Kama unaamini kuwa mungu (yesu) alikuumba na baadae kujitoa kukuokoa bure huwezi kumlinganisha na huyo mwanamalundi ambaye ameoza kaburini akisubiri yesu arudi na apate ujira kadiri ya matendo yake. Wito: Matendo ya mitume 4:12 "wokovu haupatikani kwa mwingine, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu litupaso sisi kuokolewa kwalo isipokuwa jina la yesu" je unakubali kumpokea yesu kristo kuwa bwana na mwokozi wako? Kama jibu ni ndiyo basi mungu azidi kubariki na weka uamuzi wako hapa watu wasipotoke na huyo mwana (mtotomalundi)

Usipotoshe watu kamwe yesu siyo mungu kwa mujibu wake yeye mwenyewe, na BIblia. Na hii hapa ni historia na suala la dini yako hapa halipo kabisa usiwazuie watu kujua yaliyofanyika ndani ya nchi yao kwa kisingizio cha dini kaa pembeni kama hujui kitu. Kwa nataka unijibu kama unajua kufikiri kwa kina kwa nini watakatifu wote ni wazungu, halafu kuna ukweli juu ya watakatifu hao? Pia kuna tofauti gani kati ya watakatifu wakizungu na mizimu ya kwetu? Naomba jibu haraka sana wewe na wenzako msiojua siri ya wazungu.
 
Hadithi za oral tradition haziaminiki kila mtu anakwambia lake
 
Jamani naomba kupata historia ya mtu mmoja aliyeitwa mwanamalunde,kwa wenyeji wa mwanza nadhan ndo watakua wanamkumbuka zaid
 
Huyu mtu ninachojua kumhusu ni kidogo sana

Ninachofahamu ni kuwa alikuwa ni binadamu mwenye uwezo wa ziada,alikuwa ana uwezo wa kurusha kitu juu na kisirudi chini

Alikuwa na uwezo wa kutembea umbali mrefu bila kuchoka

Ngoja nifanye utafiti nijue mengi zaidi

Hii hapa chini ni kati ya zinazosadikiwa kuwa picha yake


images


Inadaiwa alikuwa haachi uso wake wazi!
 
Baada ya kusoma hii thread, Nilitaka kumjua Mwanamalundi... na katika kupekua pekua katika google nikakumba na kitabu hiki..Nimeona tushare pamoja..

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA
 
Kweli bhana bora tumuabudu huyu Yesu wetu Ng'ana Malundi. Kuloko kuabudu huyo Yesu Mzungu pengine wala hatuji hasa kama nasisi pia tunamuabudu yeye.
 
Salaam wakuu,
Nimekua nikisikiasikia kuhusu huyu mtu aliyewahi kuvuma kanda ya ziwa anayeitwa mwanamalundi. Ningependa kufahamu mawili matatu kuhusu huyu bwana na maajabu yake aliyokua akiyafanya.
 
salaam wakuu,
nimekua nikisikiasikia kuhusu huyu mtu aliyewahi kuvuma kanda ya ziwa anayeitwa mwanamalundi. ningependa kufahamu mawili matatu kuhusu huyu bwana na maajabu yake aliyokua akiyafanya.
Alikuwa anakausha mti watu wapasue kuni. Ukimkwaza akisonya tu umekwisha😈
 
mwili wake ulizikwa pale ukiriguru unapita chuo kidogo afu unaenda kijiji kinaitwa nyamle wilayani misungwi kaburi lake mpka leo lina miti ilipandwa juu ya kaburi lake hua inakauka na kichupua kila bda ya dakika 30,afu alizikwa akiwa amekaa kwenye kigoda
 
Pale kijijin kwetu shy kuna sehemu wanasema alipita. kwahiyo kaacha alama za miguu na makalio kwwnye mawe ukienda unayakuta.
 
Alikuwa anamuachia Maziwa freshi mke wake akitaka kusafiri yakiganda atakuwa amekufa yasipoganda hajafa. Pia alifunga shoka ikaning'inia juu ya dari mpaka chini akianza kusafiri kamba inaanza kuvuta shoka inaanza kupanda juu akifika mwisho wa safari na shoka itakuwa imegusa juu, akianza kurudi na shoka inaanza kushuka taratibu akifika nyumban shoka nayo inafika chini. Pia alikuwa anapanda viazi na kuiva kwa siku moja. Ni mengi ila naishia hapo
 
Back
Top Bottom