Mtendaji Mkuu wa TANROADS: Tanzania inashika nafasi ya 9 kwa miundombinu ya barabara na madaraja kati ya nchi 54 za Afrika

Mtendaji Mkuu wa TANROADS: Tanzania inashika nafasi ya 9 kwa miundombinu ya barabara na madaraja kati ya nchi 54 za Afrika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.6.

Aidha, Serikali kupitia TANROADS tayari imekamilisha kwa asilimia 100 miradi 25 ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 1,198 iliyogharimu Shilingi Trilioni 1.68 katika kipindi cha utawala wa Rais Dkt. Samia.

Haya yamebainishwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mohamed Besta wakati wa akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) kwa kiwango cha lami sehemu ya pili inayoanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60).
Screenshot 2024-10-30 093411.png
Eng. Besta ameeleza tangu Rais Samia aingie madarakani ameweka kipaumbele katika ujenzi wa barabara na madaraja ili kurahisisha usafiri na usafirshaji na kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja yenye thamani ya takribani Triloni 4.6.
WhatsApp Image 2024-10-29 at 19.34.07_e8fe8e3a.jpg

WhatsApp Image 2024-10-29 at 19.34.08_fb13771c.jpg
“Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja inaendelea kwa kasi maeneo mbalimbali nchini na hakuna mradi uliokwama kwasababu Serikali ya Rais Samia imekuwa ikilipa wakandarasi kulingana na mikataba,” amesema Besta.

Besta ameongeza kuwa hadi sasa Shilingi Bilioni 101.1 zimelipwa kwa Makandarasi katika miradi 24 ya barabara inayoendelea kutekelezwa pamoja na miradi ya minne (4) ya ujenzi wa viwanja vya ndege nchini.

Kadhalika, Besta ameeleza kuwa ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigogo Busisi) ambalo linagharimu Shilingi Bilioni 717 limefikia zaidi ya asilimia 94.

Amefafanua kuwa kutokana na mafanikio ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja nchini imeifanya Tanzania kuwa nafasi ya 9 kati ya nchi 54 za Afrika kuwa na mtandao bora wa barabara ikipanda kutoka nafasi ya 16 iliyokuwapo katika mwaka 2022 kulingana na Takwimu za mtandao wa Statista.
WhatsApp Image 2024-10-29 at 19.34.09_21db4f98.jpg
 
Wanachofanya ni spinning ya kijinga baada ya taarifa kuibuka kwamba TANROADS ipo hoi kiuchumi.
Na ukweli usemwe hii taasisi Ina hali mbaya sana watumishi wake wanaishi maisha magumu mno.
Mwigulu apeleke hela wizara ya ujenzi aache Janja janja.
Kuanzia TANROADS, TEMESA mpaka TBA hali dhoofu.
TANROADS wanashindwa kulipa wakandarasi, hawana mpaka Pesa za kununulia mafuta na mahitaji mengine madogo madogo achilia mbali posho na stahiki zingine za watumishi.
TEMESA nao inafika hatua hata Pesa ya kuagiza OIL kwaajili ya service ya magari wanakosa.
Hii nchi imekuaje aisee!?!?
 

Attachments

  • IMG-20241029-WA0000.jpg
    IMG-20241029-WA0000.jpg
    159.4 KB · Views: 8
Katika miaka ya hivi karibuni,Tanzania imeonesha juhudi kubwa sana katika kuimarisha mtandao wake wa Barabara za mjini na Vijijini na kupelekea kuingia 10 Bora Afrika ya Nchi Zenye mtandao mkubwa na Bora wa Barabara 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DBtxqsVtgAU/?igsh=MTJ5MTJsZDkyOG10Zw==

Pia soma Tanzania imeshika namba 9 Kwenye 20 Bora ya Nchi zenye Barabara bora Afrika Mwaka 2024. Yazipita Afrika Kusini, Algeria na Nigeria


My Take
Hongera TanRoads,Wizara ya Ujenzi na Serikali ya mama Samia Kwa kutoa kipaombele kwenye ujenzi wa Barabara.

Kazi inaendelea Kwa Kasi 👇👇

View: https://x.com/BusInsiderSSA/status/1852253431278281209?t=8MkHrRRWcBsL3VWZDX-qRw&s=19

Wale ambao hamtaki mezeni Razor barbed wire 👇👇

View: https://youtu.be/1xZXCDAOBvg?si=xQkfHPGdjXSOef0U
 
Kwa namna yoyote ile, kama Tanzania na ubovu wake wote inaingia kumi bora kwa lolote lile, basi Afrika ina umasikini uliokithiri. One of the poorest countries in the world inakuwa kinara wa ubora wa barabara, Afrika ni masikini sana.
 
Kwa namna yoyote ile, kama Tanzania na ubovu wake wote inaingia kumi bora kwa lolote lile, basi Afrika ina umasikini uliokithiri. One of the poorest countries in the world inakuwa kinara wa ubora wa barabara, Afrika ni masikini sana.
Acheni ujinga basi,Tanzania inafanya vizuri sio tuu Kwa Barabara Bali maeneo mengi sana.
 
Ila takwimu hazidanganyi.Tqnzania Ina Barabara nzuri sio tuu Barabara kuu Bali Hadi za Vijijini tuko Bora zaidi.
Siyo kweli tembea ujionee, tanzania barabara kwanza hazina viwango, level zetu ni zambia na mchi kama hizo ,huko southafrica paache kabisa kaa mbali siyo level zetu ,wale wanakimbizana na europe wapo mbali sana
 
Back
Top Bottom