Mtindo wa Misiba ya Siku Hizi: Watoto waliozaliwa mijini (1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kupasua ukoo

Inategemea

mna kawaida ya kwenda huko?.
Mna hata pa kufikia?.
Kabisa mkuu, tulishamsindikiza jamaa kuzika babake kijijini mkoa fulani, tulipata taabu sana, tulilala wenye coaster, nje baridi mpaka wenye mifupa, guest ya karibu hakuna, maduka ya mahitaji shida, msalani ndiyo ilikuwa kuchimba dawa, literally! Tanzania ni kubwa jamani, kuna maeneo watu wakiondoka hawarudi na sababu ni valid.

Safari ya kurudi, tulipaki njiani somewhere guest, tukawalipa kutuchemshia maji tuoge, turudi mjini tumeondoa harufu ya kijijini.
Hapana kwakweli!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kuzika mtu mahali au kijijin sio upagani upo ndani ya misaafu mf. Mf Yakob Alifia Misri Ila kuzikwa Kanaani, pia angalia Yusuph nae na kuna wengine wanazikwa kando ya msikiti au kanisa je nao ni upagani?
 
Inategemea wamejengewa misingi gani na wazazi wao, pengine toka kuzaliwa kwao hata huko kijijini hawajawahi kufika, au pengine wazazi wao hawakua na maelewano mazuri na ndugu waliopo kijijini
 
Kwa ufupi sana. Kuna watoto ambao wakishafika mjini na kupatia maisha husahau walipotoka kwa maana ya kupajenga. Sasa wakishakuwa tatizo kubwa hapa mjini wanakuwa na kampani kubwa ya marafiki zao. Linapotekea swala kifo basi huwa ni ngumu sana kuwasafirisha wapendwa wao kwa kuhofia aibu kwakuwa hakuna chochote walichokifanya pale nyumbani cha maendeleo.
 
very complicated

uzuri mkoa A kuliko nyumbani unakujua,ni ww kusuka ama kunyoa
Sasa unaenda kumsalimia/kumuona nani?


Maana wazazi wenyewe hawaishi huko hata kwenda sio kivile...how come we uende tu na haumjui yoyote wala kwa yoyote,zaidi ya kuskia tu kijiji flani kuna flani zaidi sana ulipelekwa mara moja au ndugu wachache uliwaona mara moja mbili tena walivyokuja mjini
 
Mtu amekaa Mkoa A miaka na miaka. Watu "wote" wanaomfahamu wako mkoa A. Kule kwao mkoa B "hakuna" anayemfahamu. Akifa kwa nini apelekwe kijiji cha mkoa "B"? Hata babu yake hakuzaliwa kijiji cha mkoa "B", utakuta na yeye alihamia.
Hapo sasa
 
Sasa shida yote ya nini wakati mjini makaburi yapo mengi tu
 

Naunga mkono hoja hii.
 
Kwani ukizikwa kijijini ulikozaliwa ndio tiketi ya kwenda Mbinguni? 'Ujinga huu' ni sawa na ule wa kujengea kaburi wakati wewe mwenyewe unaishi kwenye chumba cha kupanga.

Yaani unamjengea nyumba marehemu wakati watoto wako walio hai bado wamejibanza kwenye nyumba za kupanga! Tamaduni kama hizi inabidi zipitwe na wakati ili kwanza tukabiliane na changamoto za kiuchumi zenye uhitaji wa juu (pressing needs).
 
Huwa nawashangaa watu 'wanaokompliketi ' mambo ya kuzika
Kwenda kuzikwa kijijini kwenu ni kukomplikate? Nyie ndiyo wale ambao mnakata 10 yrs haujatimba kijijini kuonana na mjomba, shangazi, baba mdogo /mkubwa, babu /bibi na wengine kwenye ukoo....
 
Mleta mada amezungumzia vijana ambao wana uwezo wa kutosha wa kifedha...
 
Kwenda kuzikwa kijijini kwenu ni kukomplikate? Nyie ndiyo wale ambao mnakata 10 yrs haujatimba kijijini kuonana na mjomba, shangazi, baba mdogo /mkubwa, babu /bibi na wengine kwenye ukoo....
Mkuu, mimi nimezaliwa kijijini, nimesoma kijijini na wazazi wangu mpaka leo wako kijijini kwa hiyo there is no way naweza kumaliza miaka hata mitatu bila kwenda. Whether nitazikwa kijijini, makaburi ya kinondoni au maiti yangu ikatoswa baharini mimi naathirika nini? Katika vitu huwa havinipi shida ni hayo masuala ya kuzika
 
Umeongea vizuri sana mkuu. Tabia ya kupenda kuzika nyumbani kwenu imesaidia sana kujenga umoja kwa watu wa Kilimanjaro wanaoishi mijini kwa kuunda vyama au umoja,ambao hutumika kuchangia ili mmoja wao akifariki wanasaidiana kusafirisha kupitia michango yao. Pia huu umoja umetumika sana kujadili maendeleo huko wanakotoka vijijini na wameweza kusaidia sana kuboresha barabara, mashule etc. Pia hii kitu inaongeza connections za kazi, biashara na fursa mbalimbali maana mara kwa mara unakuta wanakutana kwenye hii misiba huko vijijini au mwezi Desemba. Watu ambao wamekimbilia mijini na hawarudi makwao hata kwenye mazishi mara nyingi wamepotezana jumla maana wako miji tofauti tofauti.
 
Nazani uanze utaratibu wa wazazi kuwaambia watoto wao wapi wazikwe hii itasaidia sana kutatua hio migogoro.

Watu wa vijijini wanalalamika tuu ila ukiwaambia wachangie ata tsh 100 ya kusafirisha mwili hawatoi.
 
Hao ni wachache sana, majority wana asili yao walikotoka, hata pale mmojawapo anapoamua kwenda town kutafuta. Hivi ukienda kutafuta maisha town mji wenu kijijini mnauuza au kuutekeleza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…