Mtindo wa Misiba ya Siku Hizi: Watoto waliozaliwa mijini (1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kupasua ukoo

Mtu amekaa Mkoa A miaka na miaka. Watu "wote" wanaomfahamu wako mkoa A. Kule kwao mkoa B "hakuna" anayemfahamu. Akifa kwa nini apelekwe kijiji cha mkoa "B"? Hata babu yake hakuzaliwa kijiji cha mkoa "B", utakuta na yeye alihamia.
Very strange [emoji23] [emoji23] this simply means that Huwa Jamaa haendagi kwao na mawasiliano hakuna. Kama unaenda kijijini regularly, unashiriki ibada kila ukienda, unajumuika kwenye michango ya maendeleo hata ukiwa town. Wana ukoo wenu mwisho wa mwaka mnakutana kwenye vikao kujadili issues mbalimbali na kusaidiana (pia upo kwenye WhatsApp group la ukoo) yaani kiufupi uko town but you know everything going on kijijini kwenu, makaburi ya ukoo unashiriki kuyatunza na mengine mengi tuu....
 
Kuna rafiki yangu naye yuko njema kifedha, katokea hukohuko Kigoma. Aliwahi kuniambia amemaliza miaka 15 hajawahi rudi huko. Nilibaki kumshangaa tu.
Na this is the main reason, Maana akipeleka msiba huko atafikia wapi? Alishakata connection long time sasa ataanzia wapi kuhusu makaburi, viongozi wa dini, support kwa washikaji etc etc...
 
Angalia last para... Muoge muondoe harufu ya kijijini!!....literally it means huko kijijini hakufai hata kuishi mtu, yaani maisha yako mjini. Huu ni mfano mzuri kwa waliokimbia kijijini kwao na kuja mjini, and they don't want to hear anything about the mother land... Ndiyo maana mtu wa namna hii huwezi kumwambia habari za kuzikwa kwao kwenye makaburi ya familia au ukoo. Lakini kwa jamii ambazo kila mwaka wanaenda vijijini kwao, wamejenga huko, wanaendeleza mashamba, biashara, ufugaji, na wana mawasiliano daily na kijijini kwao, they will always want to be buried [emoji1019] home village.
 
Sawa,ni maamuzi ya mtu. But there is no way nikazikwe makaburi ya manispaa wakati makaburi ya familia walipozikwa babu, Bibi na ndugu weengii wa ukoo wetu yapo na yanasimamiwa vizuri? Huko mjini tunatafuta pesa kwa ajili ya nini hasa? Mimi ndugu na wanaukoo zaidi ya 80 % wako kijijini na uzao wao umetawanyika mikoa mbalimbali,lakini mara nyingi tunakutana kijijini kwani unakuta kila mtu amekuja na familia yake yote. Sasa ikitokea misiba ndiyo kabisa, hata aliyeko Mtwara au Kigoma atakuja.
 
najivunia kwetu na ndivyo itakavyokuwa kwa wanangu

home is best
 
najivunia kwetu na ndivyo itakavyokuwa kwa wanangu

home is best
Sasa huyu nliyemtolea mfano kwao ni wapi,wanapoishi wazazi wake au walipozaliwa wazazi wake...maana yeye anajua wanapoishi wazazi wake tu ila ye hajui walipozaliwa wazazi wake kama anajua ni through story au aliendaga mara moja tu
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwenda kuzikwa kijijini kwenu ni kukomplikate? Nyie ndiyo wale ambao mnakata 10 yrs haujatimba kijijini kuonana na mjomba, shangazi, baba mdogo /mkubwa, babu /bibi na wengine kwenye ukoo....

Kwanini wao wasije mjini kumsalimia, mbona unaangalia upande mmoja tu?
 
Kwanini wao wasije mjini kumsalimia, mbona unaangalia upande mmoja tu?
Hahahahahaaaa, sawa mkuu lakini kati ya mkubwa na mtoto ni nani mwenye wajibu wa kufunga safari kwenda kumsalimia mwenzake kama sio mtoto?
 

Wewe unajua hao mababu zako huko kwenu walihamia tu toka nchi zambali kama wangoni toka south africa na wachaga wengine ni wahamiaji. Unajua makabuli ya mababu wa mababu za mababu zako yalipo? Ukifayilia utakuta walizikwa nchi tofauti huko au mikoa tofauti. Binadamu ni wahamiaji siku zote.
 
Mhhh...
 
Kuyakuza sana mambo ya kuzika nao ni utumwa wa kiimani. Ni andiko/kitabu gani kinasema watu lazima wakazkwe kwao?
 
Ni muhimu sana "kurudi nyumbani", inakupeni amsha kama wanafamilia kutopasahau nyumbani kwenu. Mkizikana makaburi ya kino mtakuwa na huo muda wa kwenda kwenu kweli?

Lakini yote inategemea kama familia mlikuzwa vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…