Niliwahi kwenda pale Agha Khan Primary School, ipo jirani na shule za Zanaki, Olympio na Diamond.
Umasikini ni mbaya tena ni laana, ee Mungu Baba tutoe huku. Wale watoto ukiwatazama wooote unawaona wamenawiri, wana afya, ngozi nyeusi ina mafuta mafuta yenye kupendeza.
Watoto wadogo wameshiba vizuri, uniform imekaa penyewe, imemtight vizuri. Vifungo vya shati vimebana, kiatu cheusi na soksi nyeupeee.
Hakuna mtoto asiyechana nywele, hakuna mtoto akiongea anarusha mate. Watoto wanacheza kistaarabu, muda wa kutoka pale nje hakuna bajaj au boda hata moja inayosubir kumchukua mtoto, nje kuna prado, harrier, benz, alphard n.k hizi IST, Raum, Rumion ambazo sisi tunatambazo nazo basi pale ndo gari za kwenda kuchukulia watoto.
Ukikaa pale kwa lisaa tu hakika utachukia hizi shule zetu za Kayumba. Walimu wapo smart, hakuna mwalimu kavaa kata K, hakuna mwalimu anayevaa suluari za malinda au zile suluari za karume za elfu tatu tatu sijui elfu nne.
Ee Mungu utusaidie.