Mtoto wa kaka yangu wa kwanza (First born) amebamiza 'A' za kutosha za darasa la nne mpaka nimeogopa sana, tutafute pesa Elimu nzuri ni gharama

UPUUZI MTUPU, 2025 kutumia kigezo cha kufanikiwa kukalili majibu ya notes mnashangilia? Kama Taifa tunasafari ndefu sana mpaka watu watakapotambua utofauti wa elimu na kukalili TAKATAKA za darasani.

Kiufupi Tanzania hatuna elimu, bali tuna mfumo wa kipuuzi wa kukalilisha watoto wasome kipi, wajue kipi, wahoji kipi, wawe vipi, yaani tunawasuka watoto wawe ndani ya mfumo ambao wanaaminishwa ndio maisha na ndio ufunguo wa mafanikio.

Baadae vilio ndio hivi Kila mwaka vilaza wapya kutoka vyuo vikuu wanaingia mitaani wakiwa hawana A wala B ya maisha zaidi ya kuilalamikia serikali iwape ajira.
 
Had uanze kumlipia mwanao Ada ya 20mil+ Jua you are well Financially…mostly kwenye biashara so kuja kupambania ajira kwa hili soko…Duhh utakua hauko sawa kichwani.
 
Kila mtu na maamuzi yake mkuu, hela anayo kwanini asipeleke mwanae sehemu nzuri akapata quality education ?
Wote kupata As ama wote kusoma UDSM sio kigezo cha kusema usipatie mtoto wako elimu bora.
Nimesema hyo yote hapo chini
 
Elimu ya Tz ni utapeli aheri hzo 5 Milion kwa mwaka,uwekeze UTT atazikuta huko ukubwani!! Faten wahind na waarabu jns wanai treat elimu kwa hapa bongo.
Shule nyingi nzuri Tz lkn elimu ni kukaririshana kwa kumpa mtoto programmes nyingi ili abebe materials kichwani.
 
Elimu ya sasa ni biashara zaidi, hamna lolote.
 
Em kojoa ukalale
 
Anaweza kumaliza form six na four ya Mwisho bado sana
 
La Nne kupiga A nayo mpaka hela siku hizi? Darasa la nne????? Inamaana elim imekuwa ya kise**e hivi mpaka mtu kupata A darasa la nne imekuwa ni News??
 

Watakutana na Wakwangu wakiwa na Bahasha kutafuta kazi ya mshahara wa laki tano.

Wako kasoma kwa milioni 50 wangu kasoma kwa 1M tu.
genius hawahitaji kupambwa kama hivoo!? hyo elimu ya kumezeshwa haitamsaidia kitu ikiwa ajira zenyewe ndo kama hvo kaka zake tu tupo foleni tunamsubiri aje aunge foleni!? Iweee wasalimie bukoba
 
genius hawahitaji kupambwa kama hivoo!? hyo elimu ya kumezeshwa haitamsaidia kitu ikiwa ajira zenyewe ndo kama hvo kaka zake tu tupo foleni tunamsubiri aje aunge foleni!? Iweee wasalimie bukoba
Ndio hapo aisee
 
Mwalimu analipwa vizuri kuanzia 2M anaachaje kua smart
 
ridhika na ulichonacho hujui mwenzio kafikaje pale moyo wa mtu kichaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…