Mtoto wa miaka sita anagoma kwenda shule. Nini kifanyike?

Umeshawahi kujaribu kuchunguza experience yake ya siku za mwanzo shuleni? Sometimes kuna shule zinamfanya mtoto aogope kwenda shule asubuhi. Cases zs bullying, walimu wenye changamoto na hata wazazi, zinachangia sana watoto kukwepa kwenda shule. Kama umeshindwa kuongea na mtoto kugundua tatizo kuna wataalamu wa child psychology / education psychology wanaweza kusaidia.
 
Ingekuwa watoto tunazimana kama baskeli ningemwambia amlete huyo mwanae kwangu, halafu aje amfate baada ya mwezi.
Ati mtoto wa miaka sita anamgomea mzazi na baba anatulia!!
Hakunaga mtoto anamdindia Baba, wengi hudinda kwa mama zao kisha wakikua wanadindia wote hadi jamii
 
Acha uongo, wazungu gani wanafungia watoto wasio taka shule ndani?;
Halafu unaongelea ndege na magari gani haya matoi mnayowapa hao watoto wenu wachezee ndo ajifunzie ugunduzi? Serious?
 
muhamishie mkoani kwa bibi yake atabadika na kubadilishwa na mazingira tu 🐒
 
Serikali iangalie hili swala vizuri maana hali si nzuri.Umri wa vijana kuoa uongezwe angalau 35+ mpaka 40 kijana anakuwa na akili za kiutu uzima.

Nyuzi za kivulana kama hizi zinachosha na imeanza kuzoeleka wavulana waliokimbilia majukumu kuja humu kulalamika vitu vya kijingajinga.
 
Je kwa huku akina mwajuma je?
 
Mkuu si unaona dunia kipindi hiki ilivyo bize na vita?

Huenda huu ni mwisho wa dunia.

Na huyo mwanao ndie yesu kristu mwenyewe amerudi duniani kama alivyoahidi.

Maana yesu nae aliwasumbua sana wazazi wake, mara katoroka, mara yupo sokoni.
 
Tatizo la watanzania wengi wanadhani kupiga ndilo suluhisho na njia ya kumfunza mtoto. Mnakosea sana sana. Mimi nilikuwa na mtoto mdogo wa chekechea ambaye alikuwa kila akiona school bus imekuja anaangua kilio na anakwenda akilia. Sikumpiga bali nilimbembeza na kujua kuwa kumbe darasani kwao waalim wao walikuwa wanachapa viboko sana watoto wadogo wale. Mtoto wako anaweza kuwa na tatizo eg usonji na nyie mnapiga badala ya kwenda hospital.
 
Wabongo noma. Ndiyo maana watoto wakikua wanakuja kugeuka kuwa polisi katili, wanasiasa katili na kila sehemu unakuta makatili. Madhara ya viboko. Hebu fikiria mpaka miaka hii kuna watu wanapiga watoto wanaotumia mikono ya kushoto eti ni mkono wa mavi. Elimu ndogo na lack of exposure.
 
We uliona wapi wazungu wakifanya hivyo??
Kwahiyo bongo zozo alimuweka mwanae ndani akamkuta anakimbia kimbia ndio akaona huyu atakua mwanariadha au sio?

Na vipi wacheza porn wa kizungu ilikuaje kuaje??
 
Mnaacha kutumia akili na teknolojia yote hii bado mnachapachapa hovyo watoto.
Wazee wetu wa zamani hakukua na danganyatoto nyingi, viboko ndio ilikua suluhisho ila kwa kipindi hiki ambacho watoto wanajua mambo mengi wakiwa bado wadogo viboko sio suluhi ya kudumu itamharibu mtoto.

Sio kila kosa la kudunda, hilo la shule ni kumshawishi na kilio chake kisiwatishe. Dogo wakati anaanza shule na miaka minne kasoro ilikua ukimpeleka shule analia kama anauawa vile, ila unamuacha hivyo hivyo, mwisho akazoea akapata marafiki, na ticha akawa rafiki yake.

Mpaka leo std 5 wala hana mawazo ya kuacha shule.
 
Mtoto wa miaka 6 unamtuma na anakujibu " nenda mwenyewe" eeh mwenyezi Mungu naomba nipe uvumilivu jamani. Wewe na mke wako mlimleaje huyo mtoto mpaka anafikia hatua ya kuwajibu kabisa au kukataa shule?

Nina mtoto wa miaka 6 anaingia darasa la pili sasa hivi, changamoto ndogondogo zipo ila anajua nafasi yake kama mtoto ukimtuma na anajua majukumu yake kwa umri wake na ana heshima kwa wakubwa wake.
Miaka 6 ni mkubwa sana jamani halafu kumpiga hakumsaidii zaidi ya kumjengea usugu, mfundishe kwa upendo na upole ingawa "usimnyime viboko" pale inapobidi wazazi ndio mna influence kwa watoto wenu so mjitafakari tabia zenu kabla hamjamnyooshea kidole mtoto wenu.
 
Kizazi Cha kipumbavu hiki,mtoto wa miaka 6 anakushinda na bila aibu unafungua Uzi JF kuomba msaada.

Wazazi wa siku hizi bure kabisa.
 
Tatizo wazazi wengi wanawapa watoto wao kila kitu, lakini wanasahau kuwapa malezi pamoja na kuwafundisha nidhamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…