Mtoto wa miaka sita anagoma kwenda shule. Nini kifanyike?

Mtoto wa miaka sita anagoma kwenda shule. Nini kifanyike?

Nilipokuwa High school kuna jamaa alinambia kuwa haamini kama kweli kafika High school sababu alikuwa akikataa kwenda shule ila familia yake yote ilikuwa ikimbeba mzobe mzobe hadi shule, yaan walikuwa wakimbeba na kwenda kumtupa shulen kila siku
Hahahaha
 
Labda ndo First born.
Itakua nahisi...ila baba yake nae mlaini Sana,ndio suala la kulileta hapa kweli? Sasa mpaka akifika miaka 18 si tutakua tumesoma nyuzi kumuhusu mpaka tumechoka...maana anaonekana "anampenda" Sana mtoto wake.
 
Mnawadekeza saana hao watoto, Matatizo hayo huanzia mbali, kwanza katika malezi ya kila siku mpaka hapo unapompangia majukumu anagoma. Tatizo ni la malezi zaidi.
 
Mpe buku aka jitegemee mambo ni mengi mda mchache, mnadekeza afu mnaleta sifa za ajabu eti kama mtu mzima
wajinga hao kwa hiyo km alilia tumboni mnataka tuamaini nn sasa nendeni kwa waganga maana ndio akili zenu mnataka wote tuwaze vile
 
Tatizo lipo hapo unapoamini kuwa huyo mtoto siyo wa kawaida na kumpa cheo cha kuwa ana akili kama mtu mzima. Tatizo la pili ni hilo la mtoto kukataa kucheza na wenzake. Wazazi wengi hupenda kudhani watoto wao ni wa tofauti kwa kutaja visa mbalimbali ambavyo ni mambo ya kawaida tu kufanywa na mtoto. Matatizo mawili, hachezi na wenzake na hataki shule.

Tatizo linalomsumbua ni hofu. Hataki shule kwa sababu ana hofu. Hachezi na wenzake kwa sababu ana hofu. Hofu imesababishwa na malezi ya kudekezwa kusifiwa na kuonwa kwamba ana akili kuliko wengine kumbe ni wa kawaida tu na watoto wengi wako hivyo.

Ili aende shule na acheze na wenzake, njia mbili zinatumika. Njia ya kwanza ni kumuuliza anaogopa nini kwenda shule, ataeleza sababu zake. Njia ya pili ni mzazi kuwa mkali. Wazazi wote shirikianeni kumpiga kipigo cha kistaarabu mpaka akubali kwenda shule. Isije ikawa mama anapiga akija kwa baba unatetea, shirikianeni wote na acheni kumdekeza. Pia, hofu huweza kusababishwa na upungufu wa vitamin b 12. Itafaa mkimpikia maini ya ng'ombe angalau mara moja kwa mwezi.
 
Itakua nahisi...ila baba yake nae mlaini Sana,ndio suala la kulileta hapa kweli? Sasa mpaka akifika miaka 18 si tutakua tumesoma nyuzi kumuhusu mpaka tumechoka...maana anaonekana "anampenda" Sana mtoto wake.
Hahahaa Anaonekana "anamharibu sana" mtoto wake
 
Wazazi, Wazazi - WAZAZII!!?? Mbona wazazi wamejiweka chini (Inferior) kwa mtoto weo? Kweli ww, esp.Baba; aliamini mtoto anaweza kulia na sauti ikasikika kutoka tumboni kwa mama yake? Hapo kuna tatizo au changamoto kubwa.
Mm nashauri sio apelekwe Ukreni bali Gaza.
Wazazi wa kizazi hiki 😂😂😂😂 yaani watoto siku hizi wameanza kulia kabla hata ya kuzaliwa

Hebu ngoja nichungulie Id ya mwanzisha Uzi
 
Huyo dogo asiwasumbue, mwulize mara mbili mbili kama hataki shule mpeleke kijijini ukamwoneshe watoto wanaolima kwa mkono. Mwambie kama hataki shule kesho mpatie jembe aambatane na madogo kwenda shamba. Akirudi mjini atabeba beg la madaftari bila kuulizwa!
 
Huna kumbukumbu nyuma ya kubaibinye lkn ulichapwa

Si ufikirie nje ya BOKSI kwani lazima uandikiwe kila kitu.. Fanya bidii uwe GT

Viwalimu vile moja mbili mkononi vya kawaida mara chache.. Ila wazazi nooooooope
 
Ni wakiume Kazaliwa 2019 alipotimia miaka 4 nikampeleka nusary ile siku ya kwanza alivyoingia darasani akalia sana

Nikamrudisha abaki hom nikijua bado mdogo

Mwaka wa pili nikampeleka tena shule za serikali yaan chekechea navyo ni hivyo hivyo ni kulia mwanzo mwisho

Walimu wakajua tunamdekeza mama yake akapiga sana viboko lakini hajali lolote

Mwaka huu anatimiza miaka sita lakini suala la shule hataki kulisikia
Mama yake akimwambia suala la shule huwa anajibu huko shuleni kuna kipi cha zaidi??

Ni mtoto ambaye ukikaa naye unaweza hisi umekaa na mkubwa mwenzako akisimamia msimamo wake hata upige kiasi gani hubaki na msimamo huo huo, kama lissu sio muoga hata umtishe vipi?

Kama utatumia ukali kumtuma utajibiwa kwanini usiende mwenyewe

Na huyu hata siku mama yake anakaribia kujifungua ujio wake ulikuwa sio kama nilio uzoea kwa watoto wengine

Na kitu kilichoniacha mdomo wazi siku moja kabla ya kujifungua mama yake tupo tumelala tukawa tunasikia sauti ya kulia ndani ya tumbo masaa 7 mbele wife akasema tumbo linauma ndipo nikampeleka hospitali

Kitu kingine huyu mtoto huwezi mkuta anakudai njaa inauma

Ni mtu wa kukalili vitu kwa haraka sana na huwa hapendi cheza na watoto wenzake tokea utotoni kwake mpaka sasa
Mtoto kulilia tumboni kabla ya kuzaliwa??!!! Hiki kitu kinawezekana?

Shule ni lazima, hadi sasa ameshachelewa shule. Hapo mimi naona kuna uzembe na kudekeza kwa hali ya juu.

Pia, mtoto kujitenga sana na wenzie siyo vizuri sana, ni mojawapo ya dalili za usonji.

Usimzoeshe kutumia smartphone au kutizama TV sana kwa muda mrefu kupita kawaida.
 
Watoto kama hao ndo wanakuja kuwa ma genius badae yaani

Kama hataki shule fanya kama wazungu wanamchukua mtoto alafu wanamfungia ndani wanamuwekea kila kitu magari, ndege meli piki piki na vikorokoro kibaoa..

Mtoto anakua anapelekewa chakula tuu yaani yeye anaishi huko huko mpaka agundue kitu au atatoka akiwa anapenda kiti flan basi ndo watampelekq chuo cha hivo viti moja kwa moja mkuu .
Weee kumbe wazungu ndo huwa wanafanya hivyo?

Jamani jamani stori za kwenye alkasusu ndo zimefikia huku
 
Dogo akapange chumba chake, mwambie shule kwanza hayo mengine atafanya akijitegemea mana ana akiri za kiutu uzima , akikataa basi mwambie tu akapange chumba chake na yeye na afata vile anataka yeye over. [emoji26][emoji26]
 
Back
Top Bottom