..kwa kosa la kufadhili magaidi wa m-23.
Hii ni kazi ya waKongo wenyewe. Wasipotaka kuifanya ni shauri zao.
Ujuha wao ni kudhani nchi kama Kenya itakwenda kupigana vita kwa niaba yao. Sasa angalia wanavyoachwa kwenye mataa.
Kama hukumbuki ngoja nikukumbushe, jinsi Mseveni na Kenyatta walivyokuwa wakirukaruka kuhusu jeshi la Afrika Mashariki kwenda kwaadabisha wote wanaohusika na mgogoro huko Congo. Yaliyosemwa kwenye mkutano ule wa mwanzo unayakumbuka?
Ilikuwa ni vitisho vya vita kwa yeyote ambaye angekiuka masharti yaliyowekwa na hawa wasanii.
Mara huyo Kenyatta shatuma kikosi huko, kwenda kuanza shughuli. Wanajeshi wanatua tu Goma, kazi ikabadilika, ikawa ni "ulinzi wa amani" na wala siyo mapambano na yeyote atakayekiuka na kuvuka mstari.
M23, wakafurahi na kuchekelea wakiwakaribisha wajeshi wa Kenya.
Kagame naye kaweka ahadi ya kuwaamrisha M23 wasitishe mapigano, hii anamuahidi rafiki yake Kenyatta.
Askari waliokwenda kupigana vita, lengo likawa kulinda uwanja wa ndege Goma na siyo huko vita inakopiganwa.
Na kwa upande wa pili, 'project' ya Kenya (Tshekedi) naye anachanganyikiwa, hajui lengo la jeshi la Kenya kwenda Congo ni lipi hasa!
Kiufupi, itakuwa ni kosa la hali ya juu sana kwa Tanzania kujiingiza kwenye igizo hili ambalo limebuniwa na Kenya.
Congo ni muhimu aelewe kwamba hawezi kumtegemea Kenya, kwa sababu Kenya hawezi kumsaliti Rwanda, na sasa kwa vile Mseveni ni rafiki mkubwa wa Ruto, Tshekedi ajue atazungushwa hadi akili zimruke.
Njia pekee ya kumaliza hili ni kwake na wananchi wake wajifunge kibwebwe kikamilifu kuwakabili Rwanda na Uganda chini ya M7, vinginevyo wataendelea kulia sana.
M23 wataendelea kuwaliza wakati Kagame na Mseveni wakiwa watawala wa nchi hizo mbili.
Kila M23 anapotandikwa, kama alivyofanywa hapo 2012, atakimbilia Rwanda na Uganda, na kwenda kujipanga upya kwa msaada wa hao viongozi wawili.