Mtoto wa Museveni Kainerugaba atema cheche kuhusu Rwanda na DR Congo. Afrika Mashariki wanyamaza

Mtoto wa Museveni Kainerugaba atema cheche kuhusu Rwanda na DR Congo. Afrika Mashariki wanyamaza

Hii ni kazi ya waKongo wenyewe. Wasipotaka kuifanya ni shauri zao.
Ujuha wao ni kudhani nchi kama Kenya itakwenda kupigana vita kwa niaba yao. Sasa angalia wanavyoachwa kwenye mataa.

Kama hukumbuki ngoja nikukumbushe, jinsi Mseveni na Kenyatta walivyokuwa wakirukaruka kuhusu jeshi la Afrika Mashariki kwenda kwaadabisha wote wanaohusika na mgogoro huko Congo. Yaliyosemwa kwenye mkutano ule wa mwanzo unayakumbuka?
Ilikuwa ni vitisho vya vita kwa yeyote ambaye angekiuka masharti yaliyowekwa na hawa wasanii.

Mara huyo Kenyatta shatuma kikosi huko, kwenda kuanza shughuli. Wanajeshi wanatua tu Goma, kazi ikabadilika, ikawa ni "ulinzi wa amani" na wala siyo mapambano na yeyote atakayekiuka na kuvuka mstari.

M23, wakafurahi na kuchekelea wakiwakaribisha wajeshi wa Kenya.

Kagame naye kaweka ahadi ya kuwaamrisha M23 wasitishe mapigano, hii anamuahidi rafiki yake Kenyatta.

Askari waliokwenda kupigana vita, lengo likawa kulinda uwanja wa ndege Goma na siyo huko vita inakopiganwa.

Na kwa upande wa pili, 'project' ya Kenya (Tshekedi) naye anachanganyikiwa, hajui lengo la jeshi la Kenya kwenda Congo ni lipi hasa!

Kiufupi, itakuwa ni kosa la hali ya juu sana kwa Tanzania kujiingiza kwenye igizo hili ambalo limebuniwa na Kenya.

Congo ni muhimu aelewe kwamba hawezi kumtegemea Kenya, kwa sababu Kenya hawezi kumsaliti Rwanda, na sasa kwa vile Mseveni ni rafiki mkubwa wa Ruto, Tshekedi ajue atazungushwa hadi akili zimruke.

Njia pekee ya kumaliza hili ni kwake na wananchi wake wajifunge kibwebwe kikamilifu kuwakabili Rwanda na Uganda chini ya M7, vinginevyo wataendelea kulia sana.

M23 wataendelea kuwaliza wakati Kagame na Mseveni wakiwa watawala wa nchi hizo mbili.

Kila M23 anapotandikwa, kama alivyofanywa hapo 2012, atakimbilia Rwanda na Uganda, na kwenda kujipanga upya kwa msaada wa hao viongozi wawili.
Mkuu viongozi wa drc na jeshi lao ni wajinga na corrupt sana. Tshisekedi kaondoa viongozi jeshi fardc kaweka watu kabila yake sio wajuzi wa kijeshi bali wahuni wenye kujichubua ngozi na kuvaa micheni shingoni. Si makamanda wala askari wote ni watu waoga kama kunguru.
Wanataka wabakie na mauniform ya jeshi ila vita askari wa kigeni ndio wapigane.
Ile round ya kwanza kuwapiga M 23 bila msaada wa tanzania wasingeweza kitu. Ila huwezi sikia shukrani au kutajwa tanzania isipokua kutukuza jeshi lao lisiloweza kupiga adui.
 
Acheni mambo zenu, kwani wa congo man wako wapi kuipigania nchi yao.
Kazi kushinda kwenye vioo na kujikoboa sura.

Wajikusanye wakaipiganie nchi yao, siyo kucheza muziki na kukata mauno , alafu sisi ndiyo tukawapambanie vita yao.
Mbona wao wanazipambania Teams zetu?
 
EA nchi maskini zote hizi,wimbo wa Vita sijui hua unaimbwa kwa Sababu zipi.

Yaani nchi ambayo unaambiwa Ina Air force Kali hapa E/Africa Ni Uganda kisa eti Ina Sukhoi SU-30 ambayo idadi yake Ni 6(Six only) 😄😄.

Huko Kwny Russia-Ukraine war zishapotea ndege za kivita Zaidi ya 500,vifaru maelfu na bado wanachapana tu.

EA tunge-invest nguvu zetu hata kwny kulima kuhakikisha baa la njaa halisumbui,Vita tuwaachie matajiri.
Hawa viongozi wanaoleta choko choko, wangekuwa wao na familia zao wanaenda 'frontline' kupigana, tungeweza kuwaelewa. Tofauti na hapo, ni kutesa nguvu kazi za familia za watu.
 
Jamaa kaongea ukweli hapo.
wala hakuna uongo. Maelezo yamenyooka Rwanda na Uganda ni mtu na kaka yake
 
Mkuu viongozi wa drc na jeshi lao ni wajinga na corrupt sana. Tshisekedi kaondoa viongozi jeshi fardc kaweka watu kabila yake sio wajuzi wa kijeshi bali wahuni wenye kujichubua ngozi na kuvaa micheni shingoni. Si makamanda wala askari wote ni watu waoga kama kunguru.
Wanataka wabakie na mauniform ya jeshi ila vita askari wa kigeni ndio wapigane.
Ile round ya kwanza kuwapiga M 23 bila msaada wa tanzania wasingeweza kitu. Ila huwezi sikia shukrani au kutajwa tanzania isipokua kutukuza jeshi lao lisiloweza kupiga adui.
Pamoja na ubovu wa jeshi lao huo, lakini nadhani sasa hali imebadilika hasa kutokana na wananchi wenyewe sasa kuchoshwa na hali hiyo mbovu.
Sasa unaanza kuona wananchi wakikabiliana na MONUSC, kwa kujua hawasaidii chochote. Hata hao M23 sasa hawaungwi mkono na wananchi wa maeneo hayo, bali wanatambulika kuwa maadui.

Kwa hiyo hali inabadilika, na itafikia mahali serikali ya Kongo yenyewe ichukue jukumu la kupambana na hawa M23 na wafadhiri wao wakuu, Kagame na Mseveni.
 
Kipindi flani hawa Rwanda na Uganda wasingetamba hivi. Mimi nawaonea huruma sana DR Congo. Hawa miaka mingi wanachezewa.

Toka miaka ile na wakoloni na sasa Waafrika wenyewe kwa wenyewe. Tena wa hapahapa East Africa. Hapana kwa kweli. Ningekuwa na uwezo ningewasaidia Congo. Hawa wapuuzi wanaamini kwa East Africa wao ni untouchable.

Tunajua Ruto si mtu wa Vita. Anaonekana anapenda sana amani. Hajui wakati mwingine amani haipatikani isipokuwa kwa ncha ya Upanga. Basi ndo hivyo. Msome mtoto wa Museveni. Huyu jamaa kichwani empty sana. Basi tu.

View attachment 2434986
Hii itakuwa fake hata hiyo website ya BBC siyo ya kweli kabisa. bbc.in/3VL4f2P
 
Huyu ni mbuzi kama alivyokuwa Mbuzi Idd Amin.
 
Vita ni gharama, kuna kupoteza rasilimali watu, fedha na muda; ukimya unasaidia

Uko sahihi, lkn utulivu wa Mashariki mwa Congo nao ni muhimu.
Wajumbe wengine badala ya kwenda battlefield, wachangie rasilimali zingine.
 
Hata Kama TZ ikiingia uyo Muhooz hana uwezo wa kutuzuia.
1670200294999.png
 
Hivi Tanzania tuna SAMs gani ya kuzizuia hizi....

1670200475432.png
 
Kipindi flani hawa Rwanda na Uganda wasingetamba hivi. Mimi nawaonea huruma sana DR Congo. Hawa miaka mingi wanachezewa.

Toka miaka ile na wakoloni na sasa Waafrika wenyewe kwa wenyewe. Tena wa hapahapa East Africa. Hapana kwa kweli. Ningekuwa na uwezo ningewasaidia Congo. Hawa wapuuzi wanaamini kwa East Africa wao ni untouchable.

Tunajua Ruto si mtu wa Vita. Anaonekana anapenda sana amani. Hajui wakati mwingine amani haipatikani isipokuwa kwa ncha ya Upanga. Basi ndo hivyo. Msome mtoto wa Museveni. Huyu jamaa kichwani empty sana. Basi tu.

View attachment 2434986
Kwani ni uongo?

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Haujui kuwa Kagame alipigana vita vya kumtoa Idd Amini na pia vita ya msituni kumuingiza Mu7 madaraka ma kwamba yeye Kagame ndiye alikuwa mkuu wa kitengo cha usalama nchini Uganda kipindi cha awali utawala wa Mu7.

Sasa hapo kwanini mnamshutumu Jenerali kwaa kusema Ukweli.

Hata kuivamia Tanzania na sawa na kuivamia Uganda.

Kuivamia Uingereza umeivamia Marekani
 
Ni wakati wa tshesekedi kwenda upande wa SADC sasa kuomba msaada wa kijeshi,na ikitokea hivyo Tanzania itakua na monusco,EAC na SADC ndani ya kongo,jeshi la kenya linaweza kuwa mzigo mwingine ndani ya congo maana kenya iko kiinterest zaidi na si kiukombozi so wanaweza kufanya lolote lile ndani ya congo kwa maslahi yao
Hili lina mantiki kubwa zaidi......so long as DRC ni mwanachama wa SADC, aombe usaidizi wa kijeshi na kiulinzi kupitia SADC maana hizi nchi za EA tayari zimeonekana kuwa na makandokando mengi kwenye mgogoro wenyewe.
 
Back
Top Bottom