Mtoto wa Museveni Kainerugaba atema cheche kuhusu Rwanda na DR Congo. Afrika Mashariki wanyamaza

Hao wabanwe kwenye bandari tu over!
Rwanda mizigo yake 90% inapitia Bandari ya DSM na ndio mteja wa 2 anaepitisha mizigo mingi kwny Bandari hio.Swali,Je Kenya angekua tayari kupoteza mteja wa Bandari yake kwa Sababu ya DRC?

Je,Nini kimebadilika Leo ghafla mpk Kenya amekua interested na amani ya DRC?

Je,Tz inafurahia kupoteza influence yake DRC na kumuachia jukumu Hilo Kenya?

Akili kichwani.
 
I second this, As EAC ipitie mikataba yao kama Rwanda wanatakiwa kutoa ushirikiano hata wa kijeshi washurutishwe kufanya hivyo kweny EAC then EAC forces zipigane na M23 not keep on going to blame Rwanda
 
Vita ni gharama, kuna kupoteza rasilimali watu, fedha na muda; ukimya unasaidia
EA nchi maskini zote hizi,wimbo wa Vita sijui hua unaimbwa kwa Sababu zipi.

Yaani nchi ambayo unaambiwa Ina Air force Kali hapa E/Africa Ni Uganda kisa eti Ina Sukhoi SU-30 ambayo idadi yake Ni 6(Six only) 😄😄.

Huko Kwny Russia-Ukraine war zishapotea ndege za kivita Zaidi ya 500,vifaru maelfu na bado wanachapana tu.

EA tunge-invest nguvu zetu hata kwny kulima kuhakikisha baa la njaa halisumbui,Vita tuwaachie matajiri.
 
Congo solution ya matatizo yake italetwa na wacongo wenyewe,wengine wote wanaoenda pale wanafuata Per diem nzuri za UN, Geopolitics Influence,etc.

Imagine nchi Kama Burundi ambayo yenyewe tu nchini kwake hali yake ya usalama Ni tete eti inapeleka wanajeshi wake DRC kuwasaidia, South Sudan yenyewe ambayo inateseka na waasi wa Riek Machari mpk inategemea mission za UN ku-stabilize nchi yao nayo eti imepeleka Askari DRC.

Pale DRC Kuna Askari kutoka kila Kona ya dunia walioko chini ya mission za UN,lkn so far Matokeo Ni 0-0.

Ni mzaha huo.
 
Acheni mambo zenu, kwani wa congo man wako wapi kuipigania nchi yao.
Kazi kushinda kwenye vioo na kujikoboa sura.

Wajikusanye wakaipiganie nchi yao, siyo kucheza muziki na kukata mauno , alafu sisi ndiyo tukawapambanie vita yao.
😄 Mbunge Mnyeti alisema hilo bungeni wakam-maindi kishenzi.
 
I second this, As EAC ipitie mikataba yao kama Rwanda wanatakiwa kutoa ushirikiano hata wa kijeshi washurutishwe kufanya hivyo kweny EAC then EAC forces zipigane na M23 not keep on going to blame Rwanda
DRC ilisema yenyewe haitaki Jeshi la Rwanda kuingizwa Congo Kama mojawapo ya jeshi la East Africa.

Kagame akahojiwa kuhusu wao kuzuiwa kujiunga na jeshi la E/Africa huko Congo akasema 'wao wako very happy, sababu Kama Kuna mtu ataenda kuwasaidia kufanya kazi waliyopaswa kufanya wao(RDF) nchini DRC then kwanini yeye asifurahie'?
 
Ila sisi ngozi nyeusi aliyeturoga atuhurumie aisee walau alegeze kamba kidogo.
Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe hayaishi,watu hawathamini damu za wenzao hata kidogo. Halafu tukibaguliwa kidogo tu tunalialia wakati wenyewe hatupendani.
 
Hakuna watu wabaguzi Kama waafrika mkuu,Ni vile tu sisi tunajua kulia Lia saaana.
 
Wakuu

Watu WENGI wanadhani Muhoz ni kichwa Maji,sio KWELI!

Yule Jamaa anatumia na marais wawili Yaani paka na Mu7 kwa lengo maalumu!!

LAKINI hao wote ni Watoto wa Mama Tanzania Yaani vijana wa nyerere!

Yataisha tu,Huwa wanapiga makelele kwa msim Halafu wananyamaza Maisha yanasonga!
MUNGU ibariki EAC
 
Acheni mambo zenu, kwani wa congo man wako wapi kuipigania nchi yao.
Kazi kushinda kwenye vioo na kujikoboa sura.

Wajikusanye wakaipiganie nchi yao, siyo kucheza muziki na kukata mauno , alafu sisi ndiyo tukawapambanie vita yao.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ni wakati wa tshesekedi kwenda upande wa SADC sasa kuomba msaada wa kijeshi,na ikitokea hivyo Tanzania itakua na monusco,EAC na SADC ndani ya kongo,jeshi la kenya linaweza kuwa mzigo mwingine ndani ya congo maana kenya iko kiinterest zaidi na si kiukombozi so wanaweza kufanya lolote lile ndani ya congo kwa maslahi yao
 
Burundi pale ilipo ipo kwa ajili ya Tanzania,,kukosa TZ burundi zamani sana ingekua mikononi mwa watutsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…