Nashkuru Kwa kunielewesha mkuu, kwahiyo hayo majina ni watu tu ambao wamefariki around Davido tu? Kuna ushahidi wowote wa kuniaminisha kuwa hao ni watu wa karibu sana na Davido kama ilivo Kwa rafiki yake aliefariki mwaka Jana na Mtoto wake?
Kibinadamu tu wewe tangu ukiwa mdogo hadi sasa umepata vifo vya watu wangapi ambao wanakuznguka? Maana neno around ni pana ata kama nitafiwa na jirani yangu huku huyo ni basi ni around me, je Kwa upande wako Ukiwahesabu watafika wangapi hadi Leo hii?
Hivi unajua kama ukiwa na pesa au maarufu unakuwa na connection ya watu wengi sana kuliko mtu fukara?
Mfano Steve Nyerere amezika watu wengi sana ambao wapo kwenye mzunguko wake Kwa sababu yeye ni maarufu na anazungukwa na watu wengi
Mtu ambae amefanikiwa au maarufu anakuwa na marafiki katika kila stage anayopitia, na Kwa sababu anafanikiwa au maarufu mara nyingi mzunguko wake waga haufi tofauti na sie wakina kajamba nani
Vitu vingine ni ujinga tu kudhani kwamba kuna kundi la watu Fulani wao hawatakiwi kufa na kama wakifa basi vifo vyao sio vya halali, kwahiyo davido watu wake wa karibu wanatakiwa kuishi milele?
Ni fikra za kimaskini ndio zinatusumbua na wala sio kingine, na wala sio kwao tu ata kwako IPO siku yatakukuta, we tafuta tu hela na Mungu akusaidie uzipate kuna siku utaitwa FREEMASON na siku ukifiwa na mtu wako wa karibu utaambiwa umtoa kafara
Hesabu za probability zinasema kwamba popote pale penye number kubwa ya watu au vitu basi kuna % kubwa za matukio kutokea kuliko pale ambapo kuna number ndogo
Kwahiyo ukizungukwa na kundi kubwa la watu jua kwamba utashiriki sana kwenye Sherehe za harusi na utashiriki sana kwenye misiba, ila kama huna watu basi kuna matukio wewe utakuwa unayaskia tu Kwa watu