TANZIA Mtoto wa mwanamziki Davido Afariki Dunia akiwa anaogelea

Hao ni devil worshipper,,hiyo ni sadaka kwa miungu yao
Alooh hivi hizi mambo mnazitoaga wapi? Mbona case za watu kufa kwenye ma pool na mito na bahari ni nyingi tu.. kwa nini mtu tajiri mumfikirie hivi?
 
Ni kweli mkuu ila ninaowasema ni ndugu wa damu ambao niko nao pamoja na hakuna hata fununu ya kusemwa

Binadamu hawana siri mkuu na hakuna kinachofichwa
We work hard bro [emoji123] na ndumba mwiko kwetu
Sioni sababu ya kwenda kutafuta uchawi kwa masikini asiyeweza kutajirisha wanae au jamaa zake hilo tu huwa linanipa ukakasi

Lakini kila mmoja ana maamuzi yake
Lakini sisi tunafanya biashara pamoja wote
 
Uzi wa makafara huu[emoji23]
 
Sio vibaya kuwa navyo
ila hivi vitu swimming pool na bembea ni vitu hatari hasa kwa watoto wadogo
Kuna jamaa alipoteza mtoto baada ya bembea kukatika ikamrusha mtoto kwenye jiwe alipiga paji la uso kimbiza hospital cf hospital 2 days akafariki
Kwa watoto ni vitu vinataka awepo mtu mzima hapo karibu lakini ndo hivyo.
Maji nayo hayakopeshi kama huyamudu
 
Na meza za vioo,hasa coffee table.
 
Ni mawazo yangu na fikra zangu , naomba yaheshimiwe , ni Bora ukadhibitisha uongo wangu alaf na mm nikudhibitishie ukweli wangu .... !!

Sio kila mara unachofikria wewe ukafkr ni sahihi
Ni ngumu sana kuheshimu mawazo ya kipuuzi, sema huyo jamaa alipaswa akupuuze
 
Sio swimming pool.tu hata haya majakuzi ni hatari kwa watoto
Sana, kuna family member aliwahi kupoteza mtoto kutumbukia kwenye ndoo tu mtoto kaingia chooni tu anachezea maji yalikuwa yamejazwa kwenye ndoo. Mimi nakuwa mkali sana kwa mtoto kuingia chooni au kuchezea maji yaliojazwa. Nadhani mzazi yoyote ajifunze kwa watoto wadogo sababu hupendi kusikia yanamtokea mzazi yoyote, Davido maarufu leo tunaongea hapa ila yanatokea sana familia nyingi. Tuwe makini sana
 
Kumbe huyo mwamba alikuwa na mtoto na huyo manzi...

R.I.P mtoto mdogo
 
Hata hilo kuna siku shetani akiamua anatembea nao tu.

India watu walijiachia darajani wakapiga na ma selfie muda ilipofika daraja likaenda chini watu wakanywa maji.

Hakuna ajuaye dk 2 zijazo kitu gani kitatokea.
 
Hata hilo kuna siku shetani akiamua anatembea nao tu.

India watu walijiachia darajani wakapiga na ma selfie muda ilipofika daraja likaenda chini watu wakanywa maji.

Hakuna ajuaye dk 2 zijazo kitu gani kitatokea.
Mkuu daraja la India lilikuwa halijapata hata cheti cha usalama wake, watu wakajazana kupita kiasi
India ni kama sisi tu waafrika
Na kuhusu ajali zinatokea sana ila tahadhari inasaidia kwa asilimia kubwa

Swimming pool zipo za kufunika mkuu na ni gharama zako tu na ni imara ni kama paa la nyumba yako tu kuanguka kwake ni nadra sana
 
Inahitaji akili huru kukuelewa.

Mtu akifungamanishwa na ushabiki hawezi kukubaliana na wewe
 
Davido alivyopewa taarifa alichana nguo yake na kutaka kukimbilia barabarani.
Yaani alichanganyikiwa kabisa.
 
Inahitaji akili huru kukuelewa.

Mtu akifungamanishwa na ushabiki hawezi kukubaliana na wewe
Jamii yetu imejaa wajinga sana, utadhani huku mitaani kwetu watu hawafi, ila Vifo vyetu sie ni vya halali ila Vifo vya watu maarufu na wenye pesa ni Kafara

Sasa sijui ni kwenye maandiko gani tumeambiwa watu wenye hela wanastahili kuishi milele na hawatakiwi kufiwa na watu wanaowazunguka

Huyu aliekazana Leo kusema mtoto ametolewa kafara ndio huyo huyo atakuja kuitwa freemason endapo kupambana kwake kutakutana na bahati na kufanikiwa kuwa mwenye pesa

Huyu huyu anaesema wenzeie wanatoa kafara akipata pesa atakuja kufiwa na ataambiwa katoa kafara na wale wale watu aliokuwa nao katika kundi lao la wajinga

Hii shida inaletwa na umaskini wa maendeleo pamoja na umaskini wa Akili, Leo hii Diamond kutokana na umaarufu wake na anavozungukwa na watu wengi akisema ashiriki kwenye kila msiba basi almost kila mwezi atakuwa anaonekana msibani na hizi story za kutoa watu kafara zitaanza kumuandama

Tofauti ya mastaa wengine na Davido ni moja tu, Davido kakuta pesa chafu kwao tangu anazaliwa kwahiyo hana ulimbukeni wa pesa na hiyo hali inamfanya kuwa na marafiki wale wale miaka yote tofauti na sie ambao mafanikio tunayapatia ukubwani ni kila kukicha kubadili marafiki na kusahau wapi tulitokea

Kama kupata utajiri ni kuuwa watu basi wengi sana wangekuwa matajiri maana Kwa roho zetu za kibongo zilivo kumuuwa mtu uwe tajiri ni dakika sifuri tu, ila kwakuwa sio kweli tunaishia tu kuwasema watu waliotoboa
 
Kuna baharia mmoja namjuwa nyumbani kwake kunduchi kulikuwa na pool
Sasa kuna wakati lile pool juu walilifunika na plastic kubwa kuzuia uchafu nk
Sasa kuna siku mtoto mdogo alidumbukia mule lile fuko likamfungafunga,mtoto alikata moto pale pale
Mpaka leo lile bwawa jamaa kageuza dampo la taka tu

Ova
 
Watu tisa ndani ya nyumba na bado mtoto anazama kwenye swimming pool,haki hichi kifo kina walakini.Ngoja tusubiri hiyo report ya kifo kama itawekwa hadharani na Polisi.Ila hamna watu wanaongoza kwa kutoa makafara kama Wanaijeria nimefika kwao nimeishi nao kwa mda aisee ni balaa zito.Nashangaa hawa wanaobisha kwa ufupi tu jaribuni kugoogle voodoo mjionee hii ni mojawapo ya ndumba maarufu.Tufiakwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…