Nikiangalia waarabu walivoitenda dunia nimekuja kujifunza Kumsikiliza mungu.
Akikwambia tulia kwene ndoa ana maanisha.
Akikwambia oa mke mmoja wewe na mkeo muwe mwili mmoja ana maanisha.
Ukitenda unayoyajua utaiumiza dunia na ukoo wako na kizazi chako.
Mtoto wa nje ya ndoa siyo
Poleni mliozaliwa nje ya ndoa ,, sina budi kuongea ukweli
IBRAHIM ANAAMBIWA MTOTO ATAKAYE MRITHI ATATOKA KATIKA VIUNO VYAKE
Mwanzo 15:4
Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.
ISHMAEL NDIO MTOTO ALIYETOKANA NA VIUNO VYA IBRAHIM
Mwanzo 16:2
Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Mwanzo 16:4
Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
MUNGU ANATOA BARAKA KWA ISHMAEL
Mwanzo 16:11
Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako.
Mwanzo 16:12
Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.
IBRAHIM YUPO SAUDI ARABIA NA ANAMUOMBA MUNGU UWE MJI WA AMANI
Quran 2:126
Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Akasema:
IBRAHIM NA MWANA WE ISHMAEL WANAJENGA MSIKITI WA MAKA
Quran 2:127
Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.
IBRAHIM ANAMUOMBA MUNGU ALETE MTUME PALE SAUDI ARABIA
Quran 2:129
Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Nahi nakupa kama zawadi utabiri wa mtume MUHAMMAD katika mabii wa kale Tema ni jina la mtoto wa Nabii Ishmael baadae likawa jina la mji na huo mji ndio Saudi Arabia ya Sasa
Habakuki 3:3
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
Sasa nyinyi wagalatia endeleeni tu kudanganywa na Wazungu